Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,681
- 40,623
Kila Jumamosi wananchi wa Sierra Leona wanatumia siku hiyo kufanya usafi wa nchi yao na kuirudishia sura nzuri hasa baada ya uchafu uliokithiri kufuati vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siku hiyo hakuna magari madogo n.k na watu wanajitolea na wengine hulipwa katika jitihada za kuondoa uchafu, kuzibua mifereji, kuondoa taka katika mitaa ya miji ya nchi hiyo.
Wananchi wa Sierra Leone ambao ni weusi kama sisi (if you didn't notice) wanafanya hivyo kwa sababu viongozi wao na wao wenyewe wamehamasika katika kuhakikisha kuwa nchi yao inapendeza.
Sasa najiuliza hivi viongozi wetu sisi wameweza kuhamasisha nini katika kufanya miji yetu iwe safi na mazingira yetu kuwa bora? Kwanini kila kitu lazima kifanywe kwa malipo? Hivi ule moyo wa kujitolea ambao tuliiona hasa miaka ya sabini ambapo wananchi walikuwa wanajitolea hata kulima mashamba (nakumbuka kule kijijini tulikuwa na shamba lililoitwa la "kujitolea").
Nakumbuka tuliwahi kujaribu kuwa na jumamosi za kufanya usafi wakati wa Ally Hassan Mwinyi sijui tuliishia wapi? Hivi kweli kila kitu lazima kifanywe na serikali au NGO? Ni lini wananchi wataacha kulilia "manispaa" na kuanza kufanya "vitu vyao"? Na ni lini watawala wetu wataamua kuongoza katika jitihada za kufufua moyo wa kujitolea?
Au mambo ya kujitolea na kufanya vitu kwa sababu ya mapenzi ya vitu vile ni baraka ya wazungu na bahati ya watu wa magharibi? Binafsi sijui ni nini kwani hata fisadi meya wetu hapa the D mara moja wanashiriki katika jitihada za kusafisha jiji la Detroit.
Labda nafananisha Tanzania na Marekani sana.. but what about Sierra Leone, yaani hata Siera Leone wanatuzidi kwenye mambo haya?