Watawala wetu na maadili ya watoto na vijana wetu

Ndalama

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
8,787
6,532
Salamuni wanajamvi,

Awali ya yote Mods naomba huu uzi usichanganywe na nyuzi nyingine ili wana jamvi wajadili kwa mstakabali wa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Hivi karibuni tumeshuhudia uteuzi wa wakuu wa Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini, kama ilivyo ada haitegemewi kuwa jamii nzima itafurahia uteuzi wa mteuliwa mmoja au mwingine kwa sababu mbalimbali zikiwepo za kibinadamu au historia ya kiutendaji ya mteuliwa.

Kuna teuzi nyingine kwa kweli zinatia mashaka sana, inapotokea mteuliwa kuwa na kasoro au hitilafu za wazi katika jamii na jamii kuanza kuhoji uhalali wa huo uteuzi inakuwa inatia mashaka sana na umakini katika uteuzi.

Mfano akateuliwa mtu ambaye tayari ameshatia doa katika staha yake unabaki kujiuliza hivi hawa viongozi wetu wanapoteua huwa wanafikiria nini? kama mtu ametokea kuwakosea heshima watu waliomzidi umri bila kujali wana uhusiano gani kiuhalisia hapaswi kuwekwa sehemu yoyote ya uongozi ambayo watu wengine wanapoona wanahoji hivi kwa matendo aliyofanya huyu mteuliwa kweli anafaa kuwepo hapo?

Watu wengi wamekuwa mahali fulani kimaisha kwa kutiwa moyo(kuwa Inspired) na wengine sasa mtovu wa nidhamu kupewa nafasi kubwa katika jamii inatupa tafsiri gani? Ninajiwa na hofu kuwa watawala wetu wanachangia sana kuporomoka kwa maadili ya jamii maana vijana wetu wataona huu ni utaratibu wa kawaida, unamkosea mtu mzima adabu halafu kesho unapewa pongezi kwa kupewa cheo.

Sasa hivi kuna vikaragosi vinasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa ukitaka kuwa fulani basi fanya kitendo fulani cha ukosefu wa maadili.

Chondechonde watawala wetu wa kijamii msiwape viongozi wetu wa kidini kazi kubwa ya kuwajenga waumini wao kimaadili halafu ninyi mnayabomoa huko ni kama kupishana lugha katika ujenzi unaomba mchanga unaletwa nyundo

Baba wa taifa katika hotuba zake aliwahi toa mfano wa kiongozi mmoja aliyetuhumiwa kutoka na makahaba, ile tuhuma tu ilitosha kuvuliwa madaraka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom