Watawala wanaona raha kuwafunga akina Lema

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Watawala wanaona raha kuwakomesha wananchi kwa kuwafunga akina Lema ambao ni wawakilishi wao, na waliochaguliwa kwa kura nyingi sana, tunaona Lijualikali kaenda jela miezi 6 bila sababu ya msingi wakati kosa Lake lina faini inauma na kusikitisha ni wapi demokrasia yetu inapoelekea.
 
Akina LEMA na Lijualikali wao wanajifunga wenyewe kwa kutokujua sheria za nchi hii au kwa viburi vyao. LEMA amesalia rumande hadi leo kwa kukosa dhamana chini ya Kifungu cha 148 cha Kanuni za Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa kuwa tayari alishakiuka dhamana za makosa aliyokuwa amedhaminiwa hawali. Lijualikali amefungwa jela kwa kukiuka Kifungu cha 89 cha Sheria ya Makosa ya Jina, Sura ya 16 kwa kutenda kosa la uvunjifu wa amani katika kikao cha kumchagua meya. Sheria nilizozitaja, zimeweka wazi adhabu zinazopaswa kutolewa mtu akikutwa na hatia, lakini mwisho wa yote, mahakama hasa hakimu ndiye mwenye mamlaka ya adhabu gani aitoe baada ya mtuhumiwa kujitetea. Hakimu anaweza kukupa adhabu zote mbili, kifungo na faini au faini tu au kifungo tu inategemea na uzito wa utetezi wako pia na historia na tabia yako katika kutenda makosa katika jamii. Hivyo, sheria ndiyo inayowafunga hawa watu na siyo utashi wa kisiasa. Hata wewe kama utafanya makosa kama ambayo wamefanya akina Lema na Lijualikali, utafungwa kwa vifungu hivi nilivyovitaja hapo juu.
 
Unapomweka mwanasiasi ndani unamtengenezea CV yake. Unamjenga kwa waliomchagua! Utaona hili siku atakayotoka lema kwa kuwa siku hiyo ipo.
 
Akina LEMA na Lijualikali wao wanajifunga wenyewe kwa kutokujua sheria za nchi hii au kwa viburi vyao. LEMA amesalia rumande hadi leo kwa kukosa dhamana chini ya Kifungu cha 148 cha Kanuni za Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa kuwa tayari alishakiuka dhamana za makosa aliyokuwa amedhaminiwa hawali. Lijualikali amefungwa jela kwa kukiuka Kifungu cha 89 cha Sheria ya Makosa ya Jina, Sura ya 16 kwa kutenda kosa la uvunjifu wa amani katika kikao cha kumchagua meya. Sheria nilizozitaja, zimeweka wazi adhabu zinazopaswa kutolewa mtu akikutwa na hatia, lakini mwisho wa yote, mahakama hasa hakimu ndiye mwenye mamlaka ya adhabu gani aitoe baada ya mtuhumiwa kujitetea. Hakimu anaweza kukupa adhabu zote mbili, kifungo na faini au faini tu au kifungo tu inategemea na uzito wa utetezi wako pia na historia na tabia yako katika kutenda makosa katika jamii. Hivyo, sheria ndiyo inayowafunga hawa watu na siyo utashi wa kisiasa. Hata wewe kama utafanya makosa kama ambayo wamefanya akina Lema na Lijualikali, utafungwa kwa vifungu hivi nilivyovitaja hapo juu.
Bwana mkubwa hapa nadhani unaongelea kitu kingine zaidi ya sheria! unatakiwa ufahamu kuwa hakuna sheria inayosimama peke yake bila kuwa na rejea ya sheria nyingine na pia hakuna hukumu inayosimama peke yake bila kuwa na rejea ya nyingine.
Lakini kwenye kesi hizi mbili tusisahau kuwa mamlaka ya hakimu yanaweza kuwa influenced na aina ya mshitakiwa sio aina ya utetezi. kinachoonekana hapa ni washitakiwa kutoka upinzani si uzito wa kosa au kifungu gani cha sheria kosa linakoangukia. kwa sababu ukienda maktaba pale mahakama kuu hutopata rejea yoyote ya hukumu ya aina hii kutolewa hapa nchini, kama unakataa hili nenda ukahakiki mwenyewe.

Nakubaliana na ndugu Tundu Lisu alivyosema kuhusiana na kesi hizi kuwa ni za aina yake!
 
Back
Top Bottom