gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
Kinachoendelea Tanzania kwa Sasa kinafikirisha kiasi cha kujiuliza hivi hao wanaoitwa wanyonge na watawala ni wakinanani?
Ndugu zangu kunadereva wa lorry kubwa(semi) amepigwa faini ya milioni tatu(3000,000/=) na TRA kisa amepakia gunia 25 za parachichi na walipomtaka risiti za kielekroni za transport hakuwanazo. Hivi gari la 30tones limepakia 2tones wameshindwa kujua kwamba ni dereva tu anabangaiza?
Mishahara yenyewe laki tatu dereva wa transit anasafiri kwenda kongo wakati mwingine hata mwezi mzima bado yupo njiani,siku anarudi anabahatisha japo vigunia kadhaa vimemponza ajira yake.
Huyu dereva alipofika dar ameshusha mabegi yake kaachafunguo za gari kwenye gari kaondoka bila ya kuaga kwani ile faini imeingizwa kwenye TIN no za tajiri hivyo aliogopa siku tajiri akijua huwenda akadaiwa.
Kuna mambo yanahitaji hekima wakati fulani kwani kama kila jambo likitazamwa kisheria naamini hata Magufuli kwa sasa asingekuwa uraiani muda huu angekuwa magereza. Hizi magereza zisingetosha kwani maisha yetu ya kawaida yangehamia magereza.
Nakumbuka Jakaya alishawahi kuwauliza tanroad kipindi kile cha bomoabomoa naomba nimnukuu,"Hivi kama itatokea kuna eneo la kihistoria za kale lipo kwenye hifadhi ya barabara nalo mtabomoa?"
TRA imekuwa kazi ya laaana kwani imekuwa kazi ya kuumiza na kutesa watu,tambueni mmetesa zaidi ya huyu dereva kwani huyu dereva anategemewa na familia yake na wote hawa mmewaweka kwenye taabu kisa kuwafurahisha watawala.
Nimalizie kwakusema hii faini aliopigwa huyu dereva haiendani kabisa na kosa lake kama haya ndio maagizo kutoka juu basi watawala wajue raia wanajutia wao kuwepo madarakani.