Watawala wamebariki hizi faini za kionevu zinazofanywa na TRA mabarabarani?

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Kinachoendelea Tanzania kwa Sasa kinafikirisha kiasi cha kujiuliza hivi hao wanaoitwa wanyonge na watawala ni wakinanani?

Ndugu zangu kunadereva wa lorry kubwa(semi) amepigwa faini ya milioni tatu(3000,000/=) na TRA kisa amepakia gunia 25 za parachichi na walipomtaka risiti za kielekroni za transport hakuwanazo. Hivi gari la 30tones limepakia 2tones wameshindwa kujua kwamba ni dereva tu anabangaiza?

Mishahara yenyewe laki tatu dereva wa transit anasafiri kwenda kongo wakati mwingine hata mwezi mzima bado yupo njiani,siku anarudi anabahatisha japo vigunia kadhaa vimemponza ajira yake.

Huyu dereva alipofika dar ameshusha mabegi yake kaachafunguo za gari kwenye gari kaondoka bila ya kuaga kwani ile faini imeingizwa kwenye TIN no za tajiri hivyo aliogopa siku tajiri akijua huwenda akadaiwa.

Kuna mambo yanahitaji hekima wakati fulani kwani kama kila jambo likitazamwa kisheria naamini hata Magufuli kwa sasa asingekuwa uraiani muda huu angekuwa magereza. Hizi magereza zisingetosha kwani maisha yetu ya kawaida yangehamia magereza.

Nakumbuka Jakaya alishawahi kuwauliza tanroad kipindi kile cha bomoabomoa naomba nimnukuu,"Hivi kama itatokea kuna eneo la kihistoria za kale lipo kwenye hifadhi ya barabara nalo mtabomoa?"

TRA imekuwa kazi ya laaana kwani imekuwa kazi ya kuumiza na kutesa watu,tambueni mmetesa zaidi ya huyu dereva kwani huyu dereva anategemewa na familia yake na wote hawa mmewaweka kwenye taabu kisa kuwafurahisha watawala.

Nimalizie kwakusema hii faini aliopigwa huyu dereva haiendani kabisa na kosa lake kama haya ndio maagizo kutoka juu basi watawala wajue raia wanajutia wao kuwepo madarakani.
 
Nadhani mleta uzi ingekuwa vizuri pia kujua ni eneo lipi dereva huyu lilipomkutia ili wahusika pengine waone kama hao maofisa waliokuwepo hapo walifanya kazi kwa mujibu wa sheria au la ili sheria ifate mkondo wake. Mimi ndiyo maana sasa hivi hata biskuti nadai risiti yangu sitaki shida na mtu
 
NO BIG NO mazao hayatozwi Kodi iwe ya Halmashauri au ya TRA
Mleta Mada ungetuelekeza ni wapi hapo walipomkamata na mzigo huo wa maparachichi tena yaliyooza, maana mmiliki wa parachichi ni lazima na yeye atakuwepo kwenye hilo Semi
Dereva mzigo bado haumuhus km atamtaja mwenye mzigo
ila km kakamatwa kwenye mzani wa TANROAD basi TRA wana makosa
 
NO BIG NO mazao hayatozwi Kodi iwe ya Halmashauri au ya TRA
Mleta Mada ungetuelekeza ni wapi hapo walipomkamata na mzigo huo wa maparachichi tena yaliyooza, maana mmiliki wa parachichi ni lazima na yeye atakuwepo kwenye hilo Semi
Dereva mzigo bado haumuhus km atamtaja mwenye mzigo
ila km kakamatwa kwenye mzani wa TANROAD basi TRA wana makosa
Rudia soma tena nilichoandika hujaelewa,kilichotakiwa ni risiti ya transport ambayo wanaotakiwa kutoa ni wamiliki wa malori kwa nauli wanayolipwa kwakisafirisha mzigo.

Lakini pia japo ni nje ya mada kwa faida yako,mazao yasiotozwa kodi ni inferior goods mfano matunda lakini mazao mengine kama mahindi,maharage na yote yasiooza lazima ulipe ushuru na lazima uwe na leseni ya biashara kinyume chake ukijichanganya huko road ni tatizo.

Huu ndio utawala wa wanyonge.
 
Sijaelewa..hapo ulitaka tra wapindishe sheria ili kodi ya serikali ipotee au unalalamika nini?
 
Hao Wana toza watu hizo faini wametumwa tu Wala hawajui kinachoendelea hazina.
Hata ukiwauliza kinachoendelea Ngurdoto au Dangote au New Habari corporation maskini hao hawajui. Hata waziri wao mpya hawamjui. Yaani wapo wapo tu. Wanawaza beer, rushwa na ngono zembe
 
Back
Top Bottom