Watawala wa CCM wawe wazi kubadili mfumo wa kuendesha nchi, ujanja ujanja hautaisaidia Tanzania

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Kwa miaka hii minne Utawala wa CCM unashindwa kujipambanuwa. Kuna msigano wa wazi wa itikadi ipi hasa inafaa kufuatwa na mfumo upi hasa unapaswa uwe ndio mfumo wetu wa Utawala.

Watu wengi wanaamini ni mfumo mpya " ulibatizwa jina na kuitwa " MAGUFULIZATION"

Sijui mfumo huu unalenga nini. Hata CCM iliyozoeleka haielewi nchi inatawaliwa kwa Mfumo gani.

Kwa mtazamo wangu watawala wanataka mabadiliko lakini hawajui waanzie wapi. Kunaonekana mfumo wa Mpito ambao unaelea. Jaribu kupitia hapa chini.

Utawala ulijaribu kutaka kupambana na ufisadi kuna mambo kadhaa yalifanywa ikiwemo kuanzishwa mahakama. Lakini misingi ya kikatiba imeachwa vile vile. Hatima yake imefeli inaonekana ni kukomoana tu.

Watawala walizuia Vyama kufanya siasa wakiamini Watanzania hawapaswi kuabudu siasa badala ya kujikita kufanya shughuli za kutafuta kipato KILA BAADA YA UCHAGUZI KUISHA"well" lakini tumewaona viongozi wa CCM wao wenyewe wakifanya siasa. kUMBE ILIKUWA JANJA YA KUVIZUIYA VYAMA VYA UPINZANI NA KUINUFAISHA CCM. HAKUKUWA NA DHAMIRA SAFI KUNA HADAA.

Utawala wa CCM ulipitisha sheria kadhaa zililalamikiwa kuanzia kwa wadau wa ndani ikiwemo sheria za HABARI NA MITANDAO, vyama vya siasa na sheria nyengine.

Tanzania chini ya CCM ilibadilisha sheria za mambo ya madini na kuweka elementi za Kudhibiti. Yote hayo yaliashiria kutaka kuipeleka Tanzania pahala pengine kabisa. Lakini ukweli unabaki hakukuwa na Maandalizi. Mbinu zilikosekana. Kila kitu sasa hakiko sawa.

Angalia chaguzi zetu na mvurugano uliopo. Watawala wanalazimisha kuondowa siasa kwa makosa ya kufanya hujuma na kuharibu taratibu zilizowekwa. Dhamira haiendani na wakati kwa sababu taratibu za kuleta mageuzi hazifuatwi na utawala wa CCM. Hatima yake kunaonekana Vurumai na Uhuni.
Hata majaribio ya kuchukuliwa Wapinzani yalilenga kuunda siasa mpya ya Tanzania eti kumuunga Mkono Magufuli ili kuibadilisha Tanzania. Katika hali hio ilizaliwa CCM iliyobatizwa jina "CCM mpya"
Hata kwenye CCM kuna kutoelewana kuhusu itikadi ya chama na itikadi ya Mwenyekiti. Kwa sababu mfumo uliopo hauna baraka za chama kama taasisi. Hatima yake kuna hofu ya virusi ndani ya CCM.

Angalia Mahakama zinavyocheza siasa za Watawala, Hakuna muruwa wa misingi ya haki zaidi ya ghiliba za kisiasa kuingia mahakamani. Mahakama inataka kusukuma ajenda ya watawala ya mabadiliko lakini haijuwi isimamie wapi hii ni kwa sababu kuna ujanja ujanja mwingi na hatua za awali zilikosewa.

KILICHOKOSEWA.
Ninaweza kusema Utawala wa CCM wa sasa una wazo zuri kuhusu Tanzania " Good idea" isipokuwa wamekosa pa kuanzia.

Wamekosea kipaumbele. Kipaumbele kilipaswa kuwa Katiba mpya ili kuipa misingi dhana ya mabadiliko. Tungemkumbuka Magufuli na Utawala wake kama Baba wa MABADILIKO LAKINI HIO FURSA ALIITUPA Mwenyewe. Hatima yake alitumia reshufle ya sheria ndogo ndogo ambazo zimeonekana kama udikteta kwa sababu zinapingana na hali iliyopo. Huwezi kuanza kubadili sheria fulani ukaweka mkandamizio wakati kuna sheria nyengine ziko wazi zinaruhusu mambo yaendelee kwa utaratibu uliopo. Huko ni kusababisha vurugu na Machafuko. Hio ndio nafasi ya sasa iliyopo. Unatumia amri ya Rais kuzuiya siasa wakati sheria ya vyama inaruhusu siasa kufanyika. Hili ni vurugu.

Walikosea kubuni mbinu za kuwaweka watanzania pamoja kwanza " National Agenda" Tulishauri kwenye hatua za mwanzo kabisa kwa nini Rais asingewaita Viongozi wa vyama kutoa idea ya mabadiliko na kuweka misingi ya nini anakikusudia badala yake akaamuwa kufanya "competition" ya kumega baadhi ya wapinzani? Hali hii inaleta msigano
Hata kesho Rais akiamuwa anaweza KUWEKA MISINGI YA KWELI YA MABADILIKO. Kwenye hili angetowa Plan zake na kuomba kuungwa mkono na vyama vyote kisha hatua za kisera na kisheria ikiwemo Katiba ingepata nafasi. Rais na watawala wenzake waliiangalia CCM tu bila kujali Watanzania na Tanzania kwa Ujumla. Hatima yake dhana ya mabadiliko inaelea katikati ya kutotii sheria, ubabe, Hujuma na kupotezana.

NINI KINGEPASWA KUFANYWA?
Tangaza National Agenda, Ita wadau muhimu mezani, Anzisha mchakato wa maoni shirikishi, Tunga sera, Badili Katiba , wezesha, simamia mabadilko ya msingi.

Kupitia hatua hizo unazingatia haki za watu, ubinadamu na utu na Mwishowe unafanikiwa.

Yote hayo yalenge kudumisha UMOJA kama Msingi Mkuu wa watanzania. Kinachoendelea kwa sasa ni vurugu,


Hakuna uwazi hakuna ukweli nwa dhamira huko ni kukaribisha vurugu kwenye nchi.

Kama kumekusudiwa mabadilko ya uendeshaji wa nchi taratibu zifuatwe na sio ujanja ujanja kama huu unaofanywa sasa.

Tukiwa na Dhamira ya kweli Tanzania itabadilika.

Kishada.
 
Changes is a Process.

IMG_20200121_094540_1579589250999.jpeg
IMG_20200121_094600_1579589214157.jpeg



Unforgetable
 
Kila kitu kiko kwenye mstari wewe, Uchumi unakua zaidi ya 7% na hali ya maisha ya watanzania imeimarika kuliko wakati wowote ule, watoto wetu wanasoma bure sasa, watoto wanafaulu huko mashuleni balaa ( A+ za kutosha), wagonjwa mahospitalini madawa yakutosha na hawalali chini tena, mavivuko yakutosha, SGR, Stieggler gorge, maflyover kila mahala.
 
Kila kitu kiko kwenye mstari wewe, Uchumi unakua zaidi ya 7% na hali ya maisha ya watanzania imeimarika kuliko wakati wowote ule, watoto wetu wanasoma bure sasa, watoto wanafaulu huko mashuleni balaa ( A+ za kutosha), wagonjwa mahospitalini madawa yakutosha na hawalali chini tena, mavivuko yakutosha, SGR, Stieggler gorge, maflyover kila mahala.
Hii statement sijui ina maana gani " the moment denies the context' Nadhani inahusika hapa.
 
Ili Tanzania itoke kwenye hili tope

1. CCM ife, maana ndio tope lenyewe

2. Katiba mpya kutengezwa ilikuendana na wakati

3. Taasisi kuu muhimu ziwe huru kabisa (hii inayojitaa inamzizi mrefu ndio chanzo cha Fujo zote tuzionazo.)
- mahakama but
- bunge but

Hatimae hatuelewi tunaenda wapi, kwanini na tunataka nini.

CCM ndio tatizo kuu kimsingi
 
Kila kitu kiko kwenye mstari wewe, Uchumi unakua zaidi ya 7% na hali ya maisha ya watanzania imeimarika kuliko wakati wowote ule, watoto wetu wanasoma bure sasa, watoto wanafaulu huko mashuleni balaa ( A+ za kutosha), wagonjwa mahospitalini madawa yakutosha na hawalali chini tena, mavivuko yakutosha, SGR, Stieggler gorge, maflyover kila mahala.
Hata jangwani flyovers hakuna balaa tena la mafuriko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom