Watawala wa Afrika wanazuia viongozi kuwa viongozi

muhubiri mpya

Member
Sep 14, 2019
19
10
Naomba nianze kwa kuwasalimu, habari za wakati huu

Kwa zaidi ya nusu muongo nimekuwa nikifuatilia mijadala ya huku ndani JF nimekuja kugundua kuwa Taiifa hili na Afrika kwa ujumla tuna hazina kubwa ambayo hatuitumii kabisa

Naomba nianze kwa kusema kuna tofauti kubwa ya mtawala na kiongozi, kiongozi anaweza kuwa mtawala lakini mtawala kwa namna yoyote hawezi kuwa kiongozi

Kuna tofauti nyingi sana kati ya mtawala na kiongozi Ila naomba niseme chache tu, mtawala huona kuwa ni yeye pekee anastahili kushika wadhifa "x" wakati kiongozi huona ana wajibu wa kufanya kitu kwa ajili ya kuandaa watu wa kuchukua wadhifa "x", mtawala huwasaidia watu anaowajua na hao ndio hula nao kwenye wadhifa "x" kiongozi hutafuta watu wote ambao wanaweza kuuboresha kwa pamoja wadhifa "x"

Mtawala hujijenga yeye badala ya wadhifa "x" kiongozi hujenga wadhifa "x" badala ya yeye. Leo hii akiinuka kijana yoyote mwenye uwezo wowote kuliko watawala ujiandae kuishi maisha ya mateso ,hicho ndicho kilichotokea kwa Julius Marema wakati akiwa ndani ya ANC, hicho kinachosababisha mawazo ya Tundu Lissu kutokuchukuliwa

Hicho ndicho kilipelekea kuzaliwa kwa ACT-wazalendo baada ya zito kukabwa kila upande ndani ya chadema, hicho ndicho kinachopelekea Robert Kyagulanyi kuteseka ndani ya nchi yake ya Uganda, ndicho kinapelekea Paul Kagame aamini anaayo hati milki ya Rwanda

Ubinafsi na roho hii ya "utawala" inasababisha watu ambao wangekuwa viongozi kutembea mtaani huku watawala wakijifanya viongozi, hii imepelekea wanasayansi wakubwa ambao wapo afrika kufa wakiwa na mawazo ya kuwa wanasayansi, imepelekea watu wenye mawazo makubwa ya kuibadili Afrika kufa na mawazo yao au kuzuiliwa mawazo yao kuonekana na mtu yeyote

Hii ndio inayopelekea watu kuwaogopa watawala wa kiafrika badala ya kuogopa katiba na Sheria za nchi zao, hii inapelekea watu wenye kulijenga Taifa hili kuwa wanafiki sana wakisaidia kuwajenga watawala badala ya kujenga taifa na mfumo kiujumla. MUNGU ibariki Tanzania MUNGU ibariki afrika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom