Watawala wa afrika mnajifunza nini kuhusiana na hukumu ya charles taylor? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watawala wa afrika mnajifunza nini kuhusiana na hukumu ya charles taylor?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jun 2, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwenzako akinyolewa wewe tia maji,msemo huuu uliotumiwa na wahenga ulikuwa na fundisho kubwa kwa watu au jamii mbalimbali ambazo zenye zilijiona kuwa ziko sahihi kwa kila jambo na kuwacheka wale waliogubikwa na matatizo.Msemo huu leo hii umejidhihirisha kwa hukumu iliyotolewa kwa aliyekuwa rais wa Liberia bwana Charles Taylor kutokana na kutumia madaraka yake vibaya na kusababisha mauaji ya halaiki ya watu wake.

  Kila mmoja ni shuhuda kwa matukio yaliyotokea huku Liberia kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababishwa na uroho wa madaraka na kukandamiza haki za watoto kuwaingiza jeshini kwa mafunzo ya kivita na kushiriki vita hivyo(civil war)

  Angalizo kubwa kwa watawala wetu wa leo kwa nchi zetu za kiafrika linatakiwa liangaliwe kwa makini na kuwa somo kwa viongozi wetu waliodhani utawala ni haki yao ya msingi kwa kutumia nguvu kubwa bila kujali damu za wahanga wa kivita zikiteketea bila huruma.

  Ule wakati wa udiktekta wa kina Bokasa umepita,kwani ataye hukumu kwa upanga naye atahukumiwa kwa upanga.Hukumu hii iwe changamoto pia kwa viongozi wa chama cha mapinduzi kutokana na kauli zao za kutoachia nchi kwa makaratasi wakati wao waliipata kwa mtutu wa bunduki.Tamko hili liliwahi kutolewa na aliyekuwa rais wa serikaliya mapinduzi ya Zanzibar mh. Amani Abed Karume.

  Hukumu hii si changamoto kwa watawala tu bali iwe somo lenye tija kwa chaguzi zetu ambazo zimejaa ulaghai kwa kuwapendelea walioko madarakani na kuwanyima haki kwa makusudi tu wapinzani wao serikali.

  Iwe pia ni changamoto katika harakati za kuelekea kuunda katiba mpya kwa kutokuiingiza nchi kwenye majanga ya vita ambayo yataigharimu nchi.Mchakato huu wa katiba usihodhiwe kwa manufaa ya watu wachache bali manufaa ya wananchi wote na iwe zao la amani na nusura kwa watawala wetu kuepuka hukumu ya mahakama ya the HAGUE.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wanaweza wasijifunze chochote kwa kuona wao hayawezi kuwapata. Ni ajali kazini.
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wameona yanaweza kuwapata na wao, wameanzisha mchakato wa kuanzisha Mahakama yao Mjini Arusha, wateteua Ocampo wao ili sinema iishe kiaina!

  Membe anapiga kelele huku na huko utafikiri alikuwa na agenda ya siri ya kuanzisha tifu iwepo magamba wakishindwa uchaguzi. Aliyekuwa ana-injinia future plan ya "mtandao" ni RA aliyevua gamba, huyu BMembe ana hangaika bure tu hana sustainable strategies.
   
 4. B

  Blessing JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua Poti watawala wa Africa can never learn from Charles Taylor's issue because ABSOLUTE POWER CORRUPTS ABSOLUTELY and it is a Synthrom that African Leaders never learn. Unajua ukionja asali na ilivyo tamu, ni vigumu sana kuacha kulamba. Look at Mubarak pia na pesa zote anlikua nazo ? It looks kwamba Shetani anafunga ufahamu zao to think. Just imagine unakua na mali kemkem and then end up in jail for life kweli ni hasara. JK aone kwenzake na kujifunza anavyo tupeleka. Kwanza ana mali kemkem mara petrol station, maduka ya Home Shopping Center ambae container moja tu inakaguliwa out of hundreds of containers nakupitisha bila kulipia kodi jamini. Anavyofanya he thinks Tanzanians are dump and blind sio??? na kua na Clearing and Forwarding yake jamani ??? JK na familia yake wajuie kua wa Tanzania wanajua zote he is doing behind close doors to fool the Tanzanians looking like Mr. President Clean while he is Mr. President FISADI CHAFU.
   
Loading...