Watawala tafakarini kauli zenu, msijivune na kuwa na kiburi

soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,113
2,329
Katika maandiko matakatifu tunasoma (Kitabu cha Daniel) tunasoma habari ya Mfalme Nebukadreza and Mfalme Belshaza (mtoto wa Nebukadreza) jinsi ambavyo walifanikiwa ktk tawala zao, kwa kuwa na himaya zenye nguvu na mali nyingi, walijawa na kiburi na kujiona wao ni wao na hakuna mfano wao, walimchukiza Mungu kwa kuwa walipendeza watukuzwe wao, na hata kutumia vyombo vya nyumba ya Bwana kwa ulevi na karamu za anasa. Mwenyenzi Mungu alichukuzwa na matendo yao na aliwapiga barabara kutokana na kiburi cha ukuu wao na dharau zao...hili ni fundisho kwa watawala wetu wa sasa ... ambao kwa kauli zao wanajisahau hata kujipa hali ya kutojaribwa angali ni wanadamu, au kuwa na vyeo au kufikiria kupangiwa majukumu ya kiutawala mbinguni!!

Mfalme Belshaza alifanya dharau kwa kutumia vyombo vya hekalu la Bwana kwa kwenyea divai. Akiwa karamuni mara kilitokea (Daniel 5:25) kitanga cha mkono na kuandika ujumbe ukutani, maandiko yaliyoandikwa ni haya; "MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI". Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na waajemi. Usiku uo huo Mfalme Belshaza aliuawa na Dario Mmedi aliutwa ufalme wake.

Hivyo, viongozi wetu msilewe madaraka hata kukufuru au kujiona mko juu ya kila kitu. Kumbukeni ni ninyi watumishi wa wananchi, mnawajibika kwa wananchi na mko kwa ajili ya kuwatumikia sio kuwatisha na kuwaogofya. Kula yenu na mishahara yenu ni jasho la wananchi, sio pesa zenu, hii nchi na ya umma wa watanzania, mkoa wowotw ule ni wa wakazi wote wanaokaa kwenye huo mkoa, ofisi za serikali ni majengo yaliyojengwa kwa kodi za wananchi, sio mali ya mtu mmoja. Hivyo jiheshimuni kwa kauli zenu...maana sauti ya watu wengi ni sauti ya Mungu, kilio na manung'uniko ya watu wengi ni chukizo kwa Bwana.

Kuna maisha baada ya madaraka, hivi imagine unamaliza muda wako unapita mtaani unazomewa, je yatakuwa maisha magumu na yenye uchungu kiasi gani? Tamani kuwa mtu wa kukimbiliwa na watu kujiselfia. Msiombe kabisa iwakute hii kelele ya, huyoo huyooo, na matusi juu.
 
Miungu watu Ndiyo maana Watu Wasiojulikana awamu hii wana Nguvu sana 'Wana Dundazii!"
 
Naunga mkono hoja
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.
P.
 
Back
Top Bottom