Watawala makatili zaidi kuwahi kutokea barani Afrika

Namba 3 na 4 hapana kabisa idd amin hakuwa katili. Aliweza kuwafanya wanganda weusi kuwa matajiri kwa mda mfupi nenda uganda waulize waganda iddi amini alifanyiwa propogada kuwa katili kwa sababu ya kupenda sana dini yake ndio maana aliondolewa.mabutu aliifanya zaire watu kuishi kwa amani sana na kufanya kazi biashara ila usiingilie serikali zaire ya mabutu na ya sasa hivi ipi bora
Watawala gani makatili zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kwa sababu gani?

Mimi Nafikiri wafuatao

1.Mfalme Leopold II wa Ubelgiji
Alikuwa pia mtawala wa Congo DR ya sasa kati ya mwaka 1885 hadi 1909. Yale yote unayosoma au kusika Hitler aliwafanyia Waisraeli wa Kijuremani na Poland basi Mfalme Leopold aliwafanyia Wakongo.

2. Makaburu wa Africa Kusini(1948-1994)
Hawa walikuwa hawaamini kama Waafrika ni sawa na binadamu wengine. Watu weusi wakazi asilia wa Africa Kusini ambao walikuwa asilimia 90 ya wakazi wote walitumikishwa chini ya kongwa la utumwa na kikundi cha watu weupe wasiozidi asilimia kumi ya idadi ya watu wote kwa miaka 46.Makaburu waliondoa kabisa dhana ya utu wa mtu mweusi.

3. Iddi Amin(1971-1979)
Huyu ni Kiongozi wa Uganda aliyekuwa Katili na mwehu.Alifanya kila ushenzi katika utawala wake.Alikuwa anaamini yeye ndiye mtu pekee asiye mzungu mwenye akili kuliko wazungu wote na anayeogopwa nao.Aliua viwete alifukuza Waasia wote Uganda. Akimpenda mke wako anakuua anamchukua.

4.Mobutu Seseko(1965-1997)
Huyu alikuwa Rais wa Congo DR aliyependa maisha ya starehe tu bila kujali raia wake wako katika hali gani.Alikuwa anafanyia shopping zake Paris. Aliingizwa katika siasa za juu za Congo na Lumumba ila baadaye alihusika kikamilifu katika Mipango ya kuuwawa kwa Lumumba.

5. Yahya Jammeh wa Gambia(1994-2017)
Huyu itoshe kusema ni mwendawazimu aliyeyafikia madaraka makubwa ya nchi ndio maana hata kuondolewa kwake ilikuwa kirahisi sana ukilinganisha na madikteta wengine. Pamoja na ukatili mwingi aliofanya aliwaaminisha wagambia anayo dawa ya jadi kutibu Ukimwi na maelfu wa waathirika waliangamia katika utawala wake.

6. Jean Bedel Bokassa
Aliitawala Jamuhuri ya Africa ya Kati(CAR) Kati ya mwaka 1966 hadi 1979.Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi na baadaye alijitangaza yeye ni Mfalme.Wakati wa kujiapisha aliagiza kofia ya kifalme,farasi, champagne na hata maua kutoka Ufaransa.Huyu wapinzani wake walikufa vifo vibaya sana vya kulishwa simba na mamba.Na wakati mwingine aliua familia yote ili kuzuia kulipiza kisasi.

7. Mengistu Haile Mariam
aliitawala Ethiopia kati ya mwaka 1974 hadi 1991 alipopinduliwa na Meles Zenawi. Katika utawala wake wa miaka 17 Alifanya mauji ya kimbari, ubakaji nanjaa kwa maelfu ya raia. Karatasi yake ya mashtaka na ushahidi ilikuwa ya kurasa 8000. Yupo hai anaishi uhamishoni Zimbabwe.

8. Sani Abacha
aliitawala Nigeria kwa miaka mitano tu kati ya 1993-1998 lakini Wanaigeria waliweza kuuishi jehanamu yao kwa kipindi hiko kifupi.Pamoja na mateso na mauji mengine mengi alimtesa na kumuua mfanyabiashara maarufu Moshood Abiola mshindi wa Urais mwaka 1993 kabla ya mapinduzi, alimuua mwanaharakati maarufu wa mazingira Ken Saro-Wiwa.Wakati wa utawala wake magereza zilifurika na wapinzani wake. Aliiba zaidi ya Tirioni 1 za hela ya madafu na kuzificha ughaibuni. Alikufa mwaka 1998 kifo cha utata akiwa na makahaba watatu.

9. Teodoro Obianga Nguema
Rais wa sasa Equatorial Guinea tangu mwaka 1979.Taifa lake ni mojawapo ya nchi zenye mafuta mengi zaidi barani Africa ila zaidi ya theluthi mbili ya Raia wake wanaishi katika umaskini topevu.Yeye ndiye Alfa na Omega Guinea huwezi ukazungumza chochote dhidi yake hadharani ukabaki salama. Amemfanya mmoja wa watoto wake kuwa makamu wake wa Rais pia. Propaganda za vyombo vya habari zinamuelezea yeye kama mungu katika nchi hiyo.

10.Hissene Habre (1982-1990)
Inakadiriwa aliua watu zaidi ya elfu arobani na alitumia njia zozote za mateso kwa wapinzani wake.Katika utawala wake watu walinyongwa na vipago, walichomwa kwa gesi, waliuwawa kwa kunyimwa oksijeni n.k.
 
Jammeh hakuwa tu katili wa kawaida alikuwa ni mchawi pia.Ukisikiliza clips za Iddi Amin sio vigumu kukataa kwamba asingeweza kufanya hayo yote unayodai ni uzushi.Alikuwa aina fulani ya mwendawazimu.
Yahya Jameh akuwa katili,umemzushia.
Ata Iddi Amin kunachumvi za uzushi ziliongezwa,kama kula nyama za watu,kuwakusanya viwete na kuwatupa mto Kagera n,k
 
Mobutu alikuwa mtu poa sana
Tofauti ya Mobutu na hao wengine, yeye alikuwa sio muuaji na kuwafanyia ukatili watu wake bali yeye alikuwa mla bata mno kupindukia mfano watoto wake wanatoka kinshasa wanaenda Paris shuleni kisha usiku wanarudi kulala kinshasa
 
Mobutu alihusika na kifo cha Lumumba moja kwa moja.
Tofauti ya Mobutu na hao wengine, yeye alikuwa sio muuaji na kuwafanyia ukatili watu wake bali yeye alikuwa mla bata mno kupindukia mfano watoto wake wanatoka kinshasa wanaenda Paris shuleni kisha usiku wanarudi kulala kinshasa
 
Yahya Jameh akuwa katili,umemzushia.
Ata Iddi Amin kunachumvi za uzushi ziliongezwa,kama kula nyama za watu,kuwakusanya viwete na kuwatupa mto Kagera n,k

Obote aliua watu wengi zaidi kuliko Idi Amin. Yeye alikuwa anfanya genocide (mumewahi kusikia kuhusu Loweero triangle?).

Shida ya Idi Amini ilikuwa misifa ya kijinga (aliwahi kuwaambia wazungu wambebe) na pia hakupenda wasomi. Mambo hayo ndiyo yaliyofanya akapigiwa propaganda hasa na waingereza aliwadhalilisha kwa kuwaambia wambebe.

Mwenzake Obote alikuwa anaua kimya kimya.
 
Hakika umenena.
 
Watawala gani makatili zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kwa sababu gani?

Mimi Nafikiri wafuatao

1.Mfalme Leopold II wa Ubelgiji
Alikuwa pia mtawala wa Congo DR ya sasa kati ya mwaka 1885 hadi 1909. Yale yote unayosoma au kusika Hitler aliwafanyia Waisraeli wa Kijuremani na Poland basi Mfalme Leopold aliwafanyia Wakongo.

2. Makaburu wa Africa Kusini(1948-1994)
Hawa walikuwa hawaamini kama Waafrika ni sawa na binadamu wengine. Watu weusi wakazi asilia wa Africa Kusini ambao walikuwa asilimia 90 ya wakazi wote walitumikishwa chini ya kongwa la utumwa na kikundi cha watu weupe wasiozidi asilimia kumi ya idadi ya watu wote kwa miaka 46.Makaburu waliondoa kabisa dhana ya utu wa mtu mweusi.

3. Iddi Amin(1971-1979)
Huyu ni Kiongozi wa Uganda aliyekuwa Katili na mwehu.Alifanya kila ushenzi katika utawala wake.Alikuwa anaamini yeye ndiye mtu pekee asiye mzungu mwenye akili kuliko wazungu wote na anayeogopwa nao.Aliua viwete alifukuza Waasia wote Uganda. Akimpenda mke wako anakuua anamchukua.

4.Mobutu Seseko(1965-1997)
Huyu alikuwa Rais wa Congo DR aliyependa maisha ya starehe tu bila kujali raia wake wako katika hali gani.Alikuwa anafanyia shopping zake Paris. Aliingizwa katika siasa za juu za Congo na Lumumba ila baadaye alihusika kikamilifu katika Mipango ya kuuwawa kwa Lumumba.

5. Yahya Jammeh wa Gambia(1994-2017)
Huyu itoshe kusema ni mwendawazimu aliyeyafikia madaraka makubwa ya nchi ndio maana hata kuondolewa kwake ilikuwa kirahisi sana ukilinganisha na madikteta wengine. Pamoja na ukatili mwingi aliofanya aliwaaminisha wagambia anayo dawa ya jadi kutibu Ukimwi na maelfu wa waathirika waliangamia katika utawala wake.

6. Jean Bedel Bokassa
Aliitawala Jamuhuri ya Africa ya Kati(CAR) Kati ya mwaka 1966 hadi 1979.Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi na baadaye alijitangaza yeye ni Mfalme.Wakati wa kujiapisha aliagiza kofia ya kifalme,farasi, champagne na hata maua kutoka Ufaransa.Huyu wapinzani wake walikufa vifo vibaya sana vya kulishwa simba na mamba.Na wakati mwingine aliua familia yote ili kuzuia kulipiza kisasi.

7. Mengistu Haile Mariam
aliitawala Ethiopia kati ya mwaka 1974 hadi 1991 alipopinduliwa na Meles Zenawi. Katika utawala wake wa miaka 17 Alifanya mauji ya kimbari, ubakaji nanjaa kwa maelfu ya raia. Karatasi yake ya mashtaka na ushahidi ilikuwa ya kurasa 8000. Yupo hai anaishi uhamishoni Zimbabwe.

8. Sani Abacha
aliitawala Nigeria kwa miaka mitano tu kati ya 1993-1998 lakini Wanaigeria waliweza kuuishi jehanamu yao kwa kipindi hiko kifupi.Pamoja na mateso na mauji mengine mengi alimtesa na kumuua mfanyabiashara maarufu Moshood Abiola mshindi wa Urais mwaka 1993 kabla ya mapinduzi, alimuua mwanaharakati maarufu wa mazingira Ken Saro-Wiwa.Wakati wa utawala wake magereza zilifurika na wapinzani wake. Aliiba zaidi ya Tirioni 1 za hela ya madafu na kuzificha ughaibuni. Alikufa mwaka 1998 kifo cha utata akiwa na makahaba watatu.

9. Teodoro Obianga Nguema
Rais wa sasa Equatorial Guinea tangu mwaka 1979.Taifa lake ni mojawapo ya nchi zenye mafuta mengi zaidi barani Africa ila zaidi ya theluthi mbili ya Raia wake wanaishi katika umaskini topevu.Yeye ndiye Alfa na Omega Guinea huwezi ukazungumza chochote dhidi yake hadharani ukabaki salama. Amemfanya mmoja wa watoto wake kuwa makamu wake wa Rais pia. Propaganda za vyombo vya habari zinamuelezea yeye kama mungu katika nchi hiyo.

10.Hissene Habre (1982-1990)
Inakadiriwa aliua watu zaidi ya elfu arobani na alitumia njia zozote za mateso kwa wapinzani wake.Katika utawala wake watu walinyongwa na vipago, walichomwa kwa gesi, waliuwawa kwa kunyimwa oksijeni n.k.
Daaah...! brother....em sema corona ipo, uone hiyo orodha yako kama haijabadilika
 
Uongo. Nyumba ipi ilikuwa dhahabu tu hadi vitasa? Nyumba ya wapi hiyo ilijengwa kwa dhahabu? Huu uongo wa vijiweni.

watu wanaamini sana story za vijiweni ndio maana jamaa aliwapuuza mpaka anakufa hakuwa anapoteza muda kuwajibu, he had a humble but expensive lifestyle.
 
Obote aliua watu wengi zaidi kuliko Idi Amin. Yeye alikuwa anfanya genocide (mumewahi kusikia kuhusu Loweero triangle?).

Shida ya Idi Amini ilikuwa misifa ya kijinga (aliwahi kuwaambia wazungu wambebe) na pia hakupenda wasomi. Mambo hayo ndiyo yaliyofanya akapigiwa propaganda hasa na waingereza aliwadhalilisha kwa kuwaambia wambebe.

Mwenzake Obote alikuwa anaua kimya kimya.

umesema kweli, Idd amin alikuwa mpole sana yule jamaa alipenda kuongea utani muda wote
wale watu wanaotajwa kuuwawa na Amin ni waliopanga kumuua au waliotishia uhai wake so as Mobutu na viongozi wengine wengi tu
 
Tofauti ya Mobutu na hao wengine, yeye alikuwa sio muuaji na kuwafanyia ukatili watu wake bali yeye alikuwa mla bata mno kupindukia mfano watoto wake wanatoka kinshasa wanaenda Paris shuleni kisha usiku wanarudi kulala kinshasa

umesema ukweli ila kuhusu watoto wake, mobutu hakuishi kabisa na wanae , waliishi ulaya wakilelewa na wazungu, yeye hakutaka kuishi na wanae.
kinshasa walienda wakati wa likizo na hata hiyo likizo muda mwingi hawakumuona na hata walipomuona alikuwa busy na kazi, mwanae anaitwa Nzaga Mobutu anasema amekuja kuwa karibu na baba yake miaka ya mwishoni wakati Mobutu anakaribia kufariki
 
watu wanaamini sana story za vijiweni ndio maana jamaa aliwapuuza mpaka anakufa hakuwa anapoteza muda kuwajibu, he had a humble but expensive lifestyle.
Ubaya wanakuja kuandika huku wakiamini watu wote wa JF Hawajielewi kama wao. Eti alijenga kumba la dhahabu mpaka vitasa.
 
Back
Top Bottom