Watatu wasimamishwa kufuatia sakata la matumizi mabaya ya fedha za ukarabati wa shule ya Omumwani

mnyawusi

Senior Member
Apr 1, 2012
169
254
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Diwani Athuman amewasimamisha kazi watimishi watatu wa Manispaa ya Bukoba ili kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya ukarabati wa Omumwani sekondari.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Walioshinikiza hzo fedha zipelekwe huko ni nani maana atakuwa ni kiongozi ndani ya chama
 
Hizi pesa za rambi rambi hakika zitazua makubwa zaidi. Tatizo matumizi yake yalishakosewa toka mwanzo na zitaleta laana kwa kila ngazi na kwa kila mhusika.

Yetu masikio.
 
Hili jukwaa sasa ni habari mbaya tupu hamna raha tena! ni utumbuaji katika levels zote. Ahhh wacha nitafute lunch yangu mie.
 
Kwa Wakristo tunatambua kuwa Yuda Iskariote alipopata mapato haramu kwa kumuuza Yesu alijinyonga/ alijitundika kwa sababu ya laana ya kumsaliti mtu asiye na hatia. Wale wahanga wa tetemeko hawana hatia lakini watu wamejipatia kipato haramu kupitia wao wakiwemo wamiliki wa Shule hii iliyopewa fedha za waathirika. Wasipotubu wao, viongozi (akiwemo mwenyekiti wao) na chama chao laana yaweza watafuna ujue!
 
Back
Top Bottom