Watatu wapoteza maisha kwa kufukiwa na kifusi Arusha

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Watu watatu wamefariki Dunia na wengine watatu wamejeluhiwa baada ya kuangukiwa na Kifusi wakati wanapakia Molamu katika Machimbo ya Molamu yaliyopo Kisongo Wilayani Arusha.

Machimbo hayo yalishawahi kuuwa RAIA wengine na kufungwa na aliyekuwa mkuu wa Arusha ,Magesa Mulongo ,hata hivyo yalifunguliwa kinyemela bila kuwekwa sawa kwa miundo mbinu.

Viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Kimanta wamefika katika eneo la tukio mapema asubuhi ya leo.

====

Watatu wafukiwa na kifusi na kufariki dunia.

Watu Watatu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya moramu yaliyopo eneo la Kisongo mkoani Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta ametembelea eneo la tukio na kuwaagiza Wataalam wa madini mkoani humo kwenda katika machimbo hayo na kutoa elimu ya njia salama ya kuchimba moramu hiyo.

Amesema amebaini njia inayotumika hivi sasa si salama kutokana na kutokuwa na utaalamu wa kutosha.

Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha amewataka Wachimbaji wa moramu katika eneo hilo kuendelea na shughuli za uchimbaji huku wakichukua tahadhari.

Eneo hilo la machimbo ya moramu la Kisongo lina wachimbaji zaidi ya mia tano.

FB_IMG_1620035286318.jpg
FB_IMG_1620035280670.jpg
FB_IMG_1620035274553.jpg
 
Back
Top Bottom