Watatu wakamatwa kwa kutusi Tume ya kuchunguza vurugu za Oktoba 29

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
962
Reaction score
1,909
Jeshi la Polisi nchini limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kusambaza matusi na maudhui ya kudhalilisha, wakiwemo waliolenga wajumbe wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya vurugu za Oktoba 29, 2025 na baada ya uchaguzi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika mikoa ya Arusha, Iringa na Mbeya, huku msako wa kuwabaini na kuwakamata wengine ukiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo, Jumamosi Mei 2, 2026, uchunguzi unaendelea pia kwa wale waliopokea na kusambaza jumbe zenye matusi, kashfa, uchonganishi, chuki na upotoshaji.

Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi wanaoendelea kutoa taarifa zinazosaidia kukamatwa kwa wahusika, na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote wanaokiuka sheria za makosa ya mtandaoni na sheria nyingine za nchi.

IMG_7602.jpeg
 
View attachment 3582861

Siyo kwamba nao walikuwa wanatoa maomi yao baada ya tume kutoa ripoti yake?
 
Tume ya kishamba, Chande analiwa na waliowakamata wasio na hatia wanaliwa nao.

Hauwezi kumuudhi mtu utarajie akuchekee.
 
Pale matusi(maneno usiyoyapenda)yanakuumiza zaidi ya waliopigwa risasi wakafa na ndugu zao kutoona hata miili ya ndugu zao.Inafurahisha sana.
 
Wanaoiba mabilioni ya pesa za masikini wazomewe[waaibishwe], wanaoisema serikali vibaya wakamatwe na kupewa adhabu kali ikiwemo kifungo au kupotezwa.

Ukiwa kwenye comfort zone huwezi kuelewa.
 
Hawa manjagu ile report ya ujambazi wa CAG vip mbona wapo kimya kabisaa au..
 
Back
Top Bottom