Watatu wafutiwa mashtaka kesi ya kutorosha wanyama hai

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=1][/h]

twiga.jpg

Na Daniel Mjema, Moshi (email the author)

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), amewafutia mashtaka watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutorosha isivyo halali wanyamapori hai kwenda Doha, nchini Qatar.

Wanyama hao wakiwamo twiga wanne, wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani walisafirishwa Novemba 26 mwaka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo.

Liliwasilishwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Araffa Msafiri, Evetha Mushi na Pius Hilla.
Waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Jane Mbogo, raia wa Kenya ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Equity Aviation Services na maofisa usalama wawili wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Authority (Kadco).
Maofisa hao ni Veronica Benno na Locken Kimaro ambao jopo la mawakili wa Serikali walisema DPP ameamua kuwafutia mashtaka na kuiomba mahakama iwaachie huru, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

Katika hatua nyingine, upande wa mashtaka umebadilisha hati ya mashtaka, kusoma hati mpya na kumwongeza mshitakiwa.

Mshtakiwa huyo ni Michael Mrutu ambaye ni Ofisa Usalama wa Kadco na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa waliobakia katika kesi hiyo kuwa wanne.

Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande hadi Desemba 4 mwaka huu na kutakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang’unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi likiwamo la kusafirisha wanyama kwenda Doha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh170.5 milioni.
Mshtakiwa Ahmed na Hawa wanakabiliwa na mashtaka mengine yakiwamo ya kula njama na kufadhili utoroshwaji wa wanyama hao, kufanya biashara ya wanyamapori bila leseni na kumiliki nyara za Serikali isivyo halali.

Kwa upande wao, Kimath na Mrutu wanakabiliwa na mashtaka ya kuwezesha kufanikisha mpango wa kuwatorosha wanyama hao, kushindwa kuzuia kosa na pia kushindwa kutoa taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao.

Jopo la mawakili wanaoendesha kesi hiyo waliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kwamba jana walikuwa tayari kuanza usikilizaji wa awali.
Hata hivyo washtakiwa waliiomba mahakama iahirishe kuendelea na usikilizaji huo wa awali, kwa maelezo kuwa wanatarajia kukodi mawakili wa kuwatetea na hasa ikizingatiwa kuwa wao hawajui sheria zinazohusu kosa linalowakabili.

Hakimu Kobelo alilikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 4 mwaka huu na kuwataka washtakiwa wahakikishe siku hiyo wanakwenda na mawakili wao, ili mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa awali.
 
huu ni usanii tu ,tunachojua wengine ni kuwa ndege ya jeshi la nchi ingine, ilitua KIA ikachukua wanyama hai bila ya amiri jeshi mkuu kujua wala vyombo vya dola kujua kitu ambacho hakiwezekani, leo wankuja kudanganya watu. ujinga mwingine huu wanafikirei chi nzima ni mkutano mkuu wa ccm
 
Hii ni Hatari sana yaani Wiki Moja tu Tangu akabidhiwe Mikoba ya Mukama ameshawaachia Majangili Wenzake
 
twiga.jpg

Na Daniel Mjema, Moshi (email the author)

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), amewafutia mashtaka watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutorosha isivyo halali wanyamapori hai kwenda Doha, nchini Qatar.

Wanyama hao wakiwamo twiga wanne, wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani walisafirishwa Novemba 26 mwaka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo.

Liliwasilishwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Araffa Msafiri, Evetha Mushi na Pius Hilla.
Waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Jane Mbogo, raia wa Kenya ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Equity Aviation Services na maofisa usalama wawili wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Authority (Kadco).
Maofisa hao ni Veronica Benno na Locken Kimaro ambao jopo la mawakili wa Serikali walisema DPP ameamua kuwafutia mashtaka na kuiomba mahakama iwaachie huru, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, upande wa mashtaka umebadilisha hati ya mashtaka, kusoma hati mpya na kumwongeza mshitakiwa.

Mshtakiwa huyo ni Michael Mrutu ambaye ni Ofisa Usalama wa Kadco na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa waliobakia katika kesi hiyo kuwa wanne.

Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande hadi Desemba 4 mwaka huu na kutakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang'unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi likiwamo la kusafirisha wanyama kwenda Doha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh170.5 milioni.
Mshtakiwa Ahmed na Hawa wanakabiliwa na mashtaka mengine yakiwamo ya kula njama na kufadhili utoroshwaji wa wanyama hao, kufanya biashara ya wanyamapori bila leseni na kumiliki nyara za Serikali isivyo halali.

Kwa upande wao, Kimath na Mrutu wanakabiliwa na mashtaka ya kuwezesha kufanikisha mpango wa kuwatorosha wanyama hao, kushindwa kuzuia kosa na pia kushindwa kutoa taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao.

Jopo la mawakili wanaoendesha kesi hiyo waliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kwamba jana walikuwa tayari kuanza usikilizaji wa awali.
Hata hivyo washtakiwa waliiomba mahakama iahirishe kuendelea na usikilizaji huo wa awali, kwa maelezo kuwa wanatarajia kukodi mawakili wa kuwatetea na hasa ikizingatiwa kuwa wao hawajui sheria zinazohusu kosa linalowakabili.

Hakimu Kobelo alilikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 4 mwaka huu na kuwataka washtakiwa wahakikishe siku hiyo wanakwenda na mawakili wao, ili mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa awali.
Na KINANA aongezwe!! lakini poa ile biashara ni ya dhaifu tu!! haiwezekani dege la jeshi la quatar litue na kuchukua nyara bila ikulu kujua!! CHAMA CHA MAJANGILI NA MAJAMBAZI!!
 
Unareply kwa phrase ndogo una-quote habari kubwa,shame on u mnatuchosha watumiaji wa simu

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Na bado. Waliorahisisha wizi wa mabilioni ya mapesa ya EPA, akina Komu wa BoT wamelipa faini ya milioni tano kila mmoja!
 
Back
Top Bottom