Watatu wafariki katika ajali ya basi la mwendokasi na Pikipiki. Watu 20 mbaroni kwa kuharibu basi la Mwendokasi

Je kama aligongewa kwenye zebra bado bodaboda atakuwa na makosa...isije ikawa tunamhukumu bodaboda kwa sababu ni taahira kumbe yeye ndiye mwenye haki maana kwenye barabara ya mwendo kasi kuna zebra pia..
Chombo cha moto hakiruhusiwi kuvuka kama abiria au baiskeli
 
Ndio nikauliza kama amegongewa kwenye zebra haijalishi alikuwa anakokota au anaendesha, dereva wa mwendokasi alitakiwa kusimama kwenye zebra ndio maana zikawekwa na kama zinamatumizi mengine tofauti na zebra lines tuzijuazo je elimu imetolewa??? Maisha ya kila binadamu hata kama ni chizi lazima yalindwe na haki itolewe..
Chombo cha moto hakiruhusiwi kuvuka zebra kama afanyavyo watembea miguu
 
Je kama aligongewa kwenye zebra bado bodaboda atakuwa na makosa...isije ikawa tunamhukumu bodaboda kwa sababu ni taahira kumbe yeye ndiye mwenye haki maana kwenye barabara ya mwendo kasi kuna zebra pia..
Yeye alipita akiwa anaendesha badala ya kukokota, dereva wa mwendokasi kaona kwenye zebra peupe kanyoosha mara paaap boda ikatoka huko speed inataka kuwahi kupita ndio akapitiwa,
 
Nani alikufundisha kuwa zebra ni kivuko cha bodaboda? Labda kama alikuwa anakokota, kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa maelezo
Kama angepita anakokota asingegongwa na je wale aliokuwa kawapakia, atakuwa kaingia tu hata panya akitaka katiza njia lazima aangalie usalama, wale wanajijuaga wenyewe na akili zao
 
Kwa hiyo asiposhusha abiria wake kwenye zebra haki yake ya yeye kuwepo na kugongewa kwenye zebra inaondoka???
Ndio kwa sababu kwenye zebra mvukaji anatakiwa avuke kwa tahadhari pia, yeye kapita akiendesha, kumbuka unaweza ona kwenye zebra hakuna mtu anataka kuvuka mara ghafla unaona boda hii hapa maana akiwa anaendesha anakua kwenye kasi,
Kuna mmoja alinusurika kugongwa pale tiptop na gari ya serikali yeye katoka upande wa kulia ukiwa unaenda kkoo huku anaendesha kavuka kwa kasi sana upande aliotokea na upande pili hivyohivyo, sema yule dereva wa STK alikanyaga brek kidogo akapita. Na ndio maana wakaweka vibao kabisa usivuke na boda, bajaji au baiskeli unaendesha ni kosa kisheria
 
Yaah haiwezekani gari imesimama kushusha abiria alafu jamaa aone bodaboda inavuka akanyage mafuta...!!
Kuna siku nilikuwa naenda kimara kwa kutumia mwendokasi..gari yetu ikawa imesimama inashusha abiria sasa boda boda akaoma gari imesimama avukee aisee kumbe upande mwingne hajaona kuna Mwendokasi Express iko fire balaaa yeye aliona tu gari yetu iliyokuwa imesimama alikoswa koswaa balaa siku ilee Yule jamaa wa boda boda nadhani alienda msikitini kama sio kanisani kushukuru na kutoa sadakaa...ASINGEPONAAAAA AISEE..!
Hata hapo wenzie wangelaumu mwendokasi yaani sijui wapo vipi wale watu wakati wavuka kwa miguu wanavuka kwa amani zote sio hao
 
Hata hapo wenzie wangelaumu mwendokasi yaani sijui wapo vipi wale watu wakati wavuka kwa miguu wanavuka kwa amani zote sio hao
Acha tu mkuu wanapenya penya sana yani...! Alafu huwa wanafanya makadirio sio kabisa... Huyo nadhani alipiga hesabu mbaya labda aliona mwendokasi ipo mbali alijua ataiwahi... Hao wadada wa watu jamani khaa ukute walikuwa wanaenda kwenye shughuli labda..Mungu awapumzishe kwa amani na dereva...
 
Jeuri ya bodaboda inasababishwa na malezi mabaya waliyoyapata kutoka kwa askari wa barabarani. Kwa mfano sijajua ni sheria ipi inayowaruhusu bodaboda kupita kwenye taa nyekundu bila kusimama, tena anapita huku trafiki anamwangalia bila kuchukua hatua yoyote.

Hili lililotokea ni mwendelezo wa malezi mabaya kiasi ambacho huwa wanajiamini kuwa wanaweza kufanya lolote bila kusumbuliwa na askari wa barabarani. Kuna siku Mwenyezi Mungu apishie mbali, bodaboda wengi watakuja kugongwa kwenye taa na mabasi ya mwendokasi. Labda likitokea hilo ndio umuhimu wa kuwalazimisha bodaboda kuheshimu taa za barabarani utaonekana.

Hata hivyo kwa upande mwingine, madereva wa mwendokasi nao wana ulimbukeni na ushamba wa kujiona wana 'licence to kill". Akishapewa kibarua cha kuendesha basi la mwendokasi anajiona kama anaendesha "bullet train". Hawa marehemu waligongwa kwenye zebra cross. Je dereva wa mwendokasi haruhusiwi kupunguza mwendo anapokaribia sehemu ya kuvuka kwa miguu? Kama mtu huyu alishindwa kuwaona wanaovuka wakiwa wamepakizana, tuna uhakika gani kuwa wangekuwa wanavuka kwa miguu asingewagonga?

Tuassume kuwa dereva wa bodaboda angekuwa anakokota pikipiki yake wakati anakatiza kwenye kivuko cha miguu angesalimika pamoja na abiria wake kwa kuwa dereva wa mwendokasi angesimama kuwapisha, je dereva huyu wa bullet train aliamua kuongeza mwendo na kuwagonga kwa makusudi kwa kuwa walivunja sheria? Je adhabu ya bodaboda anayekatiza kwenye zebra cross bila kushuka kwenye pikipiki yake ni kifo???
Hapo sasa ndipo penye Point ya msingi nnayoiona, mpaka kufikia raia kuamua kutaka kumdhuru huyo dereva na kuiharibu hiyo gari kwa mawe

Nikwakua inavyoonekana kulikua kunauwezekano wa dereva wa mwendo kasi kuiokoa hiyo ajali ila kwasababu ya roho mbaya yake akaamua kumhukumu huyo boda boda kwa kumburuza poor tanzanians
 
Madereva wa boda boda wanahitaji mafunzo, hawatulii kabisa barabarani, wanakera nikiona yupo nyuma yangu nakuwa muangalifu zaidi, wanakugonga wewe mwenye gari na mob yao inakuua
Ni kweli kabisa tena Nahisi serikali inaenda kushindwa Na hawa jamaa Na itakua tatizo kubwa huko mbeleni
 
Back
Top Bottom