Watatu wafariki katika ajali ya basi la mwendokasi na Pikipiki. Watu 20 mbaroni kwa kuharibu basi la Mwendokasi

Japo sijui kilichotokea, ila kiukweli Bodaboda ndo wanaoongoza kwa kuvunja sheria hapa mjini, Mi kuna mmoja alikua anataka kuniwahi sijui ili afanyaje wakati tayari m chombo ya diesel imeshapamba moto unaanzaje kushindana nayo? wala sikutaka kumkwepesha alivyojaa Yani Mwanga wa milele ulimwangazia pale pale. Na mwingine pale mataa anabahati tu tena anabahati sana
Mkuu kwahiyo ulimuwahisha MTU kwa baba muumba?
 
MIMI YALINIKUTA LAST WEEK ALHAMISI. GARI IMEHARIBIKA JUMATANO USIKU ALHAMISI ASUBUHI NINA KIKAO MAHALI. SI NIKACHUKUA BODA BODA NIWAHI KIKAO MBAYA ZAIDI HATA HATUKUWA NA HELMET. NIKATOKEA EXTERNAL KUPITIA MAKABURINI NIKAIBUKIA SHEKILANGO BUSINESS PARK. BODA BODA WANGU KAYAPITA MAGARI YOTE YALIYOKO KWENYE FOLENI YA KUTOKA MANZESE KUKATA KWENDA SINZA AKAKAA MBELE TAHAMAKI KAPUNGUZA TU MWENDO KIDOGO AKAAMUA KUUNGANISHA BILA KUANGALIA MWENDOKASI ZINAZOTOKA BIG BROTHER. MARA NIKASIKIA HONI KUANGALIA NAONA MWENDOKASI HII HAPA NIKACHANGANYIKIWA NIKARUKA NIKAMPOTEZEA TIMING DEREVA BODA BODA NAYE AKAANGUKA. NILIFUNGA MACHO KAMA SEKUNDE 30 HIVI KUSIKILIZIA MAUMIVU YA MATAIRI.

MUNGU MKUBWA KUFUMBUA MACHO NAONA MWENDO KASI IMESIMAMA. NILIMSHUKURU MUNGU NA DEREVA WA MWENDOKASI KIMOYOMOYO. SIKUWEZA KUZUNGUMZA CHOCHOTE SIKU NZIMA NA HATA KIKAO CHENYEWE NILIKIONA NUKSI SAA SABA TU NILIONDOKA KWA KUSINGIZIA KUUMWA. BAADA YA SIKU MBILI NASIKIA HII AJALI YA MANZESE DAA NIMEZIDI KUKOSA RAHA.

FUNZO KUBWA:
1. SERIKALI NA JAMII NZIMA YA WATANZANIA TUENDELEE KUTOA ELIMU KWA MADEREVA WA BODA BODA. MIMI NI MHANGA NA NI MMOJAWAPO WA WALIOKUWA WANAWALAUMU NA KUWATUKANA BODA BODA BARABARNI. LAKINI NIMEGUNDUA HII HAISADII KWANI KILA SIKU WANAKUJA VIJANA WENGI WAPYA KWENYE HII AJIRA NA HAWAELEWI SHERIA NA HATA UMAKINI HAWANA BARANARANI
2. SIO MADEREVA WOTE WA MWENDOKASI NI WAKOROFI KAMA NILIVYO KUWA NINAAMINI NA HATA WENGI WANAAMINI HIVYO. IWAPO YULE DEREVA WA MWENDOKASI ANGEKUWA NI MKOROFI KWA KWELI ANGEWEZA TU KUTUGONGA NA AKAENDELEA NA SAFARI YAKE KWENDA UBUNGO NA ASINGEKUWA NA KUKOSA LOLOTE KWANI BODABODA WANGU NDIYE ALIYEKUWA NA MAKOSA KWA KUINGIA NJIA YA MWENDOKASI BILA TAAHADHARI YOYOTE. OMBI LANGU KWA WAMILIKI WA MWENDOKASI WAENDELEE KUWAKUMBUSHA HAWA MADEREVA KUWA HUKU BARABARANI WANAKUTANA NA WATU WASIOJUA KABISA SHERIA HASA HAWA BODABODA KWA HIYO WAONGEZE UMAKINI ITASAIDIA KUOKOA MAISHA KAMA AMBAVYO MIMI LEO MAISHA YAMEOKOLEWA NA MWENZAO AMBAYE NI MAKINI.
3. OMBI KWA TANROADS/SERIKALI IANGALIE NAMNA YA KUREKEBISHA/KUONGEZA TAA KWENYE MAGARI YANAYOTOKA BUSINESS PARK KUINGIA MOROGORO ROAD NA IITAMBUE RASMI NA KUITENGENEZA BARABARA YA VUMBI YA KUTOKEA SHUNGA SHUNGA/EXTERNAL KUPITIA MAKABURINI KUTOKEA SHEKILANGO KWA AJILI YA KUPUNGUZA FOLENI MOROGORO ROAD NA WAKATI MWENGINE BARABARA YA MABIBO.

MWISHO KILA MTU KWA IMANI YAKE AWE ANAKUMBUKA KUSALI/KUSWALI KILA WAKATI KADIRI UWEZAVYO KWA SABABU HATUJUI SAA WALA DAKIKA.
 
hakuna anayeweza kufurahia yeyote kupoteza uhai...ila BODABODA hawa sijui wafanywe vipi wawe na adabu,,, wanakufa daily but kesho yake the same......mamlaka husika ziko wapi? mishkaki kama kawa,,, fujo kila mahali....kweli wanatafuta riziki ila wanahitaji elimu..
 
Mkuu waliwekewa utaratibu wa kuvuka kwa sharti la kukokota pikipiki zao na kushusha abiria na wale waliovuka kwa kuendesha walikamatwa.. Kosa lake huyu ni kubeba mshikaki lakini dereva wa mwendo kasi naye anakosa la kujibu kwa kuendesha gari kwenye zebra crossing bila tahadhari..
Sheria iliyoandikwa haitambui chombo cha moto kuvuka kwenye zebra hilo ni tamko sio sheria...pikipiki inapaswa kupita kwenye njia yake kama anapaswa kuvuka upande wa pili apite linapopita gari.Sheria hubadilishwa kwa utaratibu rasmi.
 
Madereva wengi wa bodaboda hawafuati sheria za matumizi sahihi ya barabara, ama hawakufundishwa, ama wanakosea kwa makusudi na wanadharau. Kwahiyo ili kukomesha tabia zao za kishenzi, askari wa usalama barabarani, waendelee kuwakamata wahalifu na kuwafikisha mahakamani, ili waendelee kupewa adhabu kali.
 
MIMI YALINIKUTA LAST WEEK ALHAMISI. GARI IMEHARIBIKA JUMATANO USIKU ALHAMISI ASUBUHI NINA KIKAO MAHALI. SI NIKACHUKUA BODA BODA NIWAHI KIKAO MBAYA ZAIDI HATA HATUKUWA NA HELMET. NIKATOKEA EXTERNAL KUPITIA MAKABURINI NIKAIBUKIA SHEKILANGO BUSINESS PARK. BODA BODA WANGU KAYAPITA MAGARI YOTE YALIYOKO KWENYE FOLENI YA KUTOKA MANZESE KUKATA KWENDA SINZA AKAKAA MBELE TAHAMAKI KAPUNGUZA TU MWENDO KIDOGO AKAAMUA KUUNGANISHA BILA KUANGALIA MWENDOKASI ZINAZOTOKA BIG BROTHER. MARA NIKASIKIA HONI KUANGALIA NAONA MWENDOKASI HII HAPA NIKACHANGANYIKIWA NIKARUKA NIKAMPOTEZEA TIMING DEREVA BODA BODA NAYE AKAANGUKA. NILIFUNGA MACHO KAMA SEKUNDE 30 HIVI KUSIKILIZIA MAUMIVU YA MATAIRI.

MUNGU MKUBWA KUFUMBUA MACHO NAONA MWENDO KASI IMESIMAMA. NILIMSHUKURU MUNGU NA DEREVA WA MWENDOKASI KIMOYOMOYO. SIKUWEZA KUZUNGUMZA CHOCHOTE SIKU NZIMA NA HATA KIKAO CHENYEWE NILIKIONA NUKSI SAA SABA TU NILIONDOKA KWA KUSINGIZIA KUUMWA. BAADA YA SIKU MBILI NASIKIA HII AJALI YA MANZESE DAA NIMEZIDI KUKOSA RAHA.

FUNZO KUBWA:
1. SERIKALI NA JAMII NZIMA YA WATANZANIA TUENDELEE KUTOA ELIMU KWA MADEREVA WA BODA BODA. MIMI NI MHANGA NA NI MMOJAWAPO WA WALIOKUWA WANAWALAUMU NA KUWATUKANA BODA BODA BARABARNI. LAKINI NIMEGUNDUA HII HAISADII KWANI KILA SIKU WANAKUJA VIJANA WENGI WAPYA KWENYE HII AJIRA NA HAWAELEWI SHERIA NA HATA UMAKINI HAWANA BARANARANI
2. SIO MADEREVA WOTE WA MWENDOKASI NI WAKOROFI KAMA NILIVYO KUWA NINAAMINI NA HATA WENGI WANAAMINI HIVYO. IWAPO YULE DEREVA WA MWENDOKASI ANGEKUWA NI MKOROFI KWA KWELI ANGEWEZA TU KUTUGONGA NA AKAENDELEA NA SAFARI YAKE KWENDA UBUNGO NA ASINGEKUWA NA KUKOSA LOLOTE KWANI BODABODA WANGU NDIYE ALIYEKUWA NA MAKOSA KWA KUINGIA NJIA YA MWENDOKASI BILA TAAHADHARI YOYOTE. OMBI LANGU KWA WAMILIKI WA MWENDOKASI WAENDELEE KUWAKUMBUSHA HAWA MADEREVA KUWA HUKU BARABARANI WANAKUTANA NA WATU WASIOJUA KABISA SHERIA HASA HAWA BODABODA KWA HIYO WAONGEZE UMAKINI ITASAIDIA KUOKOA MAISHA KAMA AMBAVYO MIMI LEO MAISHA YAMEOKOLEWA NA MWENZAO AMBAYE NI MAKINI.
3. OMBI KWA TANROADS/SERIKALI IANGALIE NAMNA YA KUREKEBISHA/KUONGEZA TAA KWENYE MAGARI YANAYOTOKA BUSINESS PARK KUINGIA MOROGORO ROAD NA IITAMBUE RASMI NA KUITENGENEZA BARABARA YA VUMBI YA KUTOKEA SHUNGA SHUNGA/EXTERNAL KUPITIA MAKABURINI KUTOKEA SHEKILANGO KWA AJILI YA KUPUNGUZA FOLENI MOROGORO ROAD NA WAKATI MWENGINE BARABARA YA MABIBO.

MWISHO KILA MTU KWA IMANI YAKE AWE ANAKUMBUKA KUSALI/KUSWALI KILA WAKATI KADIRI UWEZAVYO KWA SABABU HATUJUI SAA WALA DAKIKA.
Pole sana na mshukuru Mungu kwa hilo, bodaboda hata sijui wako vipi yaani huwa wanatukwanyua sana hata uwe kwa miguu ni shida tupu
 
Back
Top Bottom