Watatu waburuzwa Mahakamani kwa utakatishaji wa Bilioni 2 za NMB

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watu watatu wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka matatu, likiwemo la wizi na utakatishaji wa zaidi ya Sh bilioni mbili mali ya Benki ya NMB.

Washitakiwa hao ni Joseph Nicas (63) Mlinzi na Mkazi wa Kimara, Paston Pangaja (37) Mkazi wa Mbeya na Jacob Mwakyembe (45) dereva ambao wameunganishwa na washitakiwa wengine 20.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni ndugu watano, Manjestus Mselema (44), Bernadetha (45) ambaye ni mama wa nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes (29) hotelia, Oswald Mselema (49) na Olaph Mselema (35) wote ni walinzi.

Walinzi wengine ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor (39) na Sylidion Odil (42). Pia wapo Tulipo Mwamuzi (40), dereva, Grace Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal International Ltd, Godwin (52) fundi mwashi na Anold Erio (25), Florah Mwita (25) mfanyabiashara na Tispo Mwasakieni (27) maarufu kama Ronic Kinyozi na mkazi wa Kawe.

Akisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Yusto Ruboroga, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai washitakiwa hao, Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na Odil na wenzao wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka huu, 2020, maeneo ya jijini Dar es Salaam walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu kufanya kosa la wizi.

Ngukah alidai Juni 8,2020 maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya Benki ya NMB.

Katika mashitaka ya tatu inadaiwa Juni 8,2020 Mbezi Beach, Kinondoni, Dar es Salaam, washitakiwa wote walijipatia Sh 2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi.

Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

Hakimu Ruboroga aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Habari Leo
 
Wanasheria naomba msaada kujua haya;

1. Kwanini kama mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi fulani, mfano hii tajwa hapo juu, kwanini bado inapelekwa kwenye mahalama hiyo?

2. Kutomruhusu mshitaliwa kujibu chochote siyo kwamba ananyimwa haki na mahakama ya kusililizwa..!?
 
Kesi ka

Kesi kama hizo zilipaswa kupelekwa mahakama husika moja kwa moja. Its unfair mtuhumiwa anapalekwa kortini halafu anaambiwa hatakiwi kujibu lolote
 
Sijaelewa hizo hela wameibaje, Wamevunja bank wakaiba au? na kwanini isiwe kesi ya wizi badala imekuwa kesi ya uhujumu uchumi?
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Ndo wale wezi walio endelea kuishi daslam baada ya kuiba mihela ya NMB kweli tunapaswa kufungua chuo cha uwizi huu ni udhalilishaji kbsa
 
Ndo wale wezi walio endelea kuishi daslam baada ya kuiba mihela ya NMB kweli tunapaswa kufungua chuo cha uwizi huu ni udhalilishaji kbsa
Wale nadhani ni wengine maana tukio lao halikutokea mwezi June kama taarifa inavyosema. Lile tukio lilitokea siku za nyuma kidogo lilihusisha walinzi wa kampuni fulani kuiba pesa wakati wanazihamisha kutoka HQ kwenda branch kama sikosei, halafu wakabaki humu humu mjini na kukimbilia kununua magari kwa fujo na nyumba
 
Mpunga mrefu Sana huo. Utagungwa mpunga wenyewe hapo. Watuhumiwa wataendelea kula Bata.

Kasusura style.
 
Wale nadhani ni wengine maana tukio lao halikutokea mwezi June kama taarifa inavyosema. Lile tukio lilitokea siku za nyuma kidogo lilihusisha walinzi wa kampuni fulani kuiba pesa wakati wanazihamisha kutoka HQ kwenda branch kama sikosei, halafu wakabaki humu humu mjini na kukimbilia kununua magari kwa fujo na nyumba
Wajinga sana
 
Back
Top Bottom