Watatu mbaroni kwa kukutwa na kobe 508 kinyume na sheria

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
760
1,000
Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, linamshikilia raia mmoja wa china na wa Zanzibar wawili wakiwa na kobe wapatao 508 kinyume na sheria.

Watatu hao Huang Xiaohua Huang(44), Makidadi Said Nangaliwe(32) mkazi wa mwera na Hassan Ramadhan Kondo (35), mkazi wa mombasa Unguja wamekutwa wamehifadhi kobe zaidi ya mia tano kwenye nyumba waliyokodisha maeneo Mombasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sendoyeka, amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuwaingiza kobe kutoka Madagascar na kuwahifadhi zanzibar na baadaye kuwasafirisha kwenda kuwauza Vietnam.

Watuhumiwa hao akiwemo raia huyo wa China Haung, aliyekutwa na hati ya kusafilia yenye namba E. 60903207, walikamatwa April 30 mwaka huu saa 8 mchana katika nyumba namba SH/MA/A/117 iliyoko maeneo ya Mombasa wakiwa na kobe hao.

Kukamatwa kwa watuhumiwa kwao kunafuatia taarifa za kiintelejensia kutoka Tanzania Bara, kwamba kuna watu wanafanya shughuli hizo, ndipo polisi kwa kushirikiana na ofisi ya maliasili wakafanikiwa kuwakamata.

Kamanda Sedoyeka amesema kwasasa watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya kukamilisha upelelezi ili kufikishwa Mahakamani.
 

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
6,107
2,000
Wasoma heading kwenye uzi kama huu huwa wanacomment hivi, " Hivi kuna watu bado wanatumia kobe na fast charger zote hizi?"...
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,015
2,000
Sheria inasemaje, Je kobe watarudishwa Madagascar ?watataifishwa au watachomwa kama wale vifaranga wa Kenya
 

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,157
2,000
Sheria ifuate mkondo wake hata Global Codes of the ethics of Tourism ,inaelezea jambo hili usisafirishe wala kutumia bidhaa zitokanazo na wanyama hasa walio hatarini kutoweka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom