Watatu kizimbani kwa kutishia kumuua mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watatu kizimbani kwa kutishia kumuua mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, May 8, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Shangwe Thani, Shinyanga; Tarehe: 7th May 2011

  WATU watatu akiwemo mgombea ubunge aliyeangushwa katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wakikabiliwa na mashitaka ya kutishia kwa maandishi kumuua Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM).

  Tukio hilo la Kishapu limekuja siku chache baada ya kutokea kwa tukio kama hilo katika
  Jimbo la Busega mkoani Mwanza ambako watu saba wakiwemo viongozi wa CCM, walikamatwa wakidaiwa kupanga njama za kutaka kumuua Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega, Dk. Raphael Chegeni.

  Waliopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga, John Chaba ni aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo lakini akaanguka katika kinyangÂ’anyiro cha kura za maoni za CCM, Bonda William, ambaye ni Mhasibu katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Wengine ni Costantine Deus na Nestory Elias.

  Washitakiwa wote watatu kwa pamoja walifikishwa katika Mahakama hiyo juzi wakikabiliwa na mashitaka matatu.

  Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka, Thabiti Kilangi kuwa washitakiwa kwa pamoja wilayani Kishapu mkoani hapa walimtenda makosa matatu Mbunge Nchambi.

  Aliyataja makosa hayo kuwa ni kutoa lugha ya matusi kinyume cha kifungu namba 82 kifungu kidogo cha kwanza A cha kanuni ya adhabu, kutishia kuua kwa maandishi kinyume cha kifungu namba 214 kifungu kidogo cha kwanza B cha kanuni ya adhabu na kula njama kuvunja heshima ya mtu kinyume cha kifungu namba 386 kifungu cha kwanza B cha kanuni ya adhabu.

  Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo ambapo mshitakiwa Bonda aliwekewa dhamana na wadhamini wawili na washitakiwa wawili Deus na Nestory walirudishwa mahabusu kutokana na kukosa wadhamini.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17, mwaka huu itakapotajwa tena.
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Na bado! ngoja 2015 isogee ndo tutasikia maasi ya ajabu. Hayo magamba nayo bado yanataka utawala wa nchi.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Magamba hayo yanauwana. Wacha waendelee kuuana tu wote hawana faida kwetu.
   
Loading...