Watatu (3) wafutiwa mashtaka ya kutorosha wanyama uwanja wa kia


commited

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,617
Points
1,195
Age
28
commited

commited

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,617 1,195
Watatu wafutiwa mashtaka kesi ya kutorosha wanyamahai

SOURCE MWANANCHI Posted Alhamisi,Novemba22 2012 saa 10:10 AM

Na Daniel Mjema, Moshi (email the author)

Posted Alhamisi,Novemba22 2012 saa 10:10 AM

KWA UFUPI
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.


SHARE THIS STORY
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), amewafutia mashtaka watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutorosha isivyo halali wanyamapori hai kwenda Doha, nchini Qatar.

Wanyama hao wakiwamo twiga wanne, wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani walisafirishwa Novemba 26 mwaka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo.

Liliwasilishwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Araffa Msafiri, Evetha Mushi na Pius Hilla.
Waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Jane Mbogo, raia wa Kenya ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Equity Aviation Services na maofisa usalama wawili wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Authority (Kadco).
Maofisa hao ni Veronica Benno na Locken Kimaro ambao jopo la mawakili wa Serikali walisema DPP ameamua kuwafutia mashtaka na kuiomba mahakama iwaachie huru, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, upande wa mashtaka umebadilisha hati ya mashtaka, kusoma hati mpya na kumwongeza mshitakiwa.

Mshtakiwa huyo ni Michael Mrutu ambaye ni Ofisa Usalama wa Kadco na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa waliobakia katika kesi hiyo kuwa wanne.

Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande hadi Desemba 4 mwaka huu na kutakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang'unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi likiwamo la kusafirisha wanyama kwenda Doha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh170.5 milioni.
Mshtakiwa Ahmed na Hawa wanakabiliwa na mashtaka mengine yakiwamo ya kula njama na kufadhili utoroshwaji wa wanyama hao, kufanya biashara ya wanyamapori bila leseni na kumiliki nyara za Serikali isivyo halali.

Kwa upande wao, Kimath na Mrutu wanakabiliwa na mashtaka ya kuwezesha kufanikisha mpango wa kuwatorosha wanyama hao, kushindwa kuzuia kosa na pia kushindwa kutoa taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao.

Jopo la mawakili wanaoendesha kesi hiyo waliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kwamba jana walikuwa tayari kuanza usikilizaji wa awali.
Hata hivyo washtakiwa waliiomba mahakama iahirishe kuendelea na usikilizaji huo wa awali, kwa maelezo kuwa wanatarajia kukodi mawakili wa kuwatetea na hasa ikizingatiwa kuwa wao hawajui sheria zinazohusu kosa linalowakabili.

Hakimu Kobelo alilikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 4 mwaka huu na kuwataka washtakiwa wahakikishe siku hiyo wanakwenda na mawakili wao, ili mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa awali.

 
Ngalangala

Ngalangala

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Messages
315
Points
195
Ngalangala

Ngalangala

JF-Expert Member
Joined May 4, 2012
315 195
Daga tupu walioshakiwa. Papa wako wapi kwenye kesi ya kuhujumu uchumi kama hii unakatama makarani na walinzi tu
 
D

DOMA

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Messages
946
Points
225
D

DOMA

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2011
946 225
Serikali ya ccm ya kisanii kuanzia rais mpaka mtendaji wa kijiji
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,402
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,402 0
Lazima kuna wakubwa behind this scam. Mshukiwa wangu wa kwanza ni yule aliyechaguliwa kushika nafasi ya Mukama katika chama twawala. Mnakumbuka huyu aliwahi kujihusisha na kashfa ya uwindaji Loliondo miaka ya 1990 wakati akiwa Mbunge wa Ars -- kuhusu ile kampuni ya Mwanamfalme wa nchi ja ya ghuba, nadhani Qatar.
 

Forum statistics

Threads 1,296,628
Members 498,713
Posts 31,254,170
Top