Watapokosa fedha za Miradi mbalimbali kwa kunyimwa misaada na mikopo, wataanza kulaumu Wapinzani hata kama Bunge litakuwa lao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika,kuna kila dalili Wahisani na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa yatatutenga ukizingatia tumepuuza wito wa wahisani wa kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki.

Kwahiyo, kitachofuata ni serikali hii kuanza kukwama katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali na hivyo wataanza kutafuta mahali pa kuelekeza lawama na hapo ndio wapinzani watapoanza kubebeshwa lawama wakati chanzo ni wao wenyewe kushindwa kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki.

Huko Bungeni hata wakiwa ni wao watupu,wataanza kuwajadili wapinzani ambao watakuwa hawamo kwa kuwalaumu na kuwabebesha lawama ambazo haziwahusu kwa.hoja kwamba ndio wanaosababisha serikali ikose mikopo na misaada na kutaka Watanzania wawaone wapinzani kuwa ndio chanzo cha wao kushindwa ku-deliver.

Narudia,baada ya kuwahujumu wapinzani na Bunge lote wakalitawala wao, bado Mbowe, Lissu, Lema, Sugu, Zitto na wapinzani wengine wataendelea kujadiliwa humo Bungeni na kubebeshwa lawama zisizowahusu wakati serikali itakuwa ni yao na Bunge pia litakuwa ni lao.

Hivi sasa kiu yao ni kutaka kuona wapinzani, hasa CHADEMA na ACT , hawaingii Bungeni lakini hilo likitimia, bado wataendelea kuhangaika tu kwani hata nafsi zao zitakuwa zinawasuta huku matatizo ya wananchi yakibaki pale pale na si ajabu hali ikawa mbaya zaidi.

Wataanza kuwaza 2025 tutawaambia mini wananchi kama Bunge lote lilikuwa lao na serikali pia ilikuwa yao hivyo lazima watengeneza propaganda mradi tu waelekeza lawama kwa wapinzani.

Tukumbuke wamekuwa wakiwalaumu wapinzani kupinga kila kitu Bungeni na kukwamisha maendeleo majimboni, hivyo sasa watakuwa ni kibarua cha kuthibitisha kwa vitendo kuwa wapinzani ambao walikuwa hawakusanyi kodi, ndio kweli walikuwa kikwazo kuanzia Bungeni mpaka kwenye majimbo.

Wameshavuruga uchaguzi na kwahiyo Bunge liktakuwa lao ila mjue tu bado wataendelea kusakama wapinzani ambao si tu hawatakuwapo Bungeni, bali pia watakuwa hawaruhusiwi kufanya hata siasa.

Na baada ya kuwaondoa wapinzani wa kweli Bungeni, msishangae wakarudisha na Bunge live, Bunge litalokuwa na kazi ya kusifu na kutukuza kama ilivyo TBC.

Time will tell.
 
Lots of disappointment kweny huu uchaguzi imekuwa ni police against wananchi hakuna uchaguzi toka tumepata uhuru umekuwa hivi haki imeporwa waziwazi ni aibu aibu aibu

Wapinzan wajifunze Bila tume huru ya uchaguz hakuna uchaguzi
Siyo Watanzania tujifunze? Maana hatijui kesho yetu.
 
Lots of disappointment kweny huu uchaguzi imekuwa ni police against wananchi hakuna uchaguzi toka tumepata uhuru umekuwa hivi haki imeporwa waziwazi ni aibu aibu aibu

Wapinzan wajifunze Bila tume huru ya uchaguz hakuna uchaguzi
Wakibaki CCM peke yao, nadhani by 2025 Tanzania itakuwa kama US kimaendeleo maana wapinzani ndio walikuwa kikwazo.
 
Lots of disappointment kweny huu uchaguzi imekuwa ni police against wananchi hakuna uchaguzi toka tumepata uhuru umekuwa hivi haki imeporwa waziwazi ni aibu aibu aibu

Wapinzan wajifunze Bila tume huru ya uchaguz hakuna uchaguzi
Polisi kakufanyaje jomba?
 
Kama hata kibaraka wao amekiri kuwa zoezi zima la upigaji kura lilienda vizuri, hao watoa 'fedha za misaada' watapata wapi sababu ya kufunga fundo?
 
Aliyeplan huu uchakachuaji alichemsha kuzuia mawakala kuingia tangu mwanzoni kwenye vituo vya kupigia kura. Kile kitendo kimeondoa dhana ya uchaguzi huru na wa haki
 
Aliyeplan huu uchakachuaji alichemsha kuzuia mawakala kuingia tangu mwanzoni kwenye vituo vya kupigia kura. Kile kitendo kimeondoa dhana ya uchaguzi huru na wa haki
Unapomchagua wakala ni wajibu wako kuhakikisha;
1. Anao uwezo wa kiafya kimwili na kiakili kufanya kazi hiyo.

2. Anao uaminifu na utayari wa kuifanya kazi hiyo.

3. Amepata mafunzo ya kumuwezesha kutambua wajibu na haki zake katika kazi hiyo.

4. Umeweka utaratibu wa kumpa support anapopata changamoto.

5 Umeweka utaratibu wa kumsimamia.

6. Umelinda maslahi yake binafsi.

7. Amefika kazini na kuifanya kazi.

Kwahiyo, wakala akishindwa kufanya kazi maana yake mgombea na chama chake hawana mfumo wa kuwapata, kuwaandaa na kuwasimamia mawakala.
 
Tatizo lenu mnaanzishaga post za kijinga na kuanza kugongeana likes, mkiambiwa Magufuli watanzania wanamwelewa nyie mnashinda JF na Twitter huku mkikosoa miradi inayowagusa watu.

Situation kwa kweli sio nzuri kwa mpenda demokrasia yeyote unahitaji upinzani; on the positive side upinzani wenyewe ulikuwa weak mna miaka 5 ya kujipanga upya. Kufanya kosa sio kurudia kosa ndio kosa.

Viva Magufuli
 
Back
Top Bottom