Watanzania Wenzangu, Wabunge Wetu na Serikali; Hivi Mzee Kawawa Ndiyo Tumemsahau Haraka Hivi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Wenzangu, Wabunge Wetu na Serikali; Hivi Mzee Kawawa Ndiyo Tumemsahau Haraka Hivi???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Apr 12, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba tumpe heshima anayostahili Mzee Wetu Rashid Mfaume Kawawa mmoja wa Waasisi mahiri kabisa wa Taifa letu. Natumaini wote tunakumbuka kuwa Simba wa Vita aliaga dunia katika Hospitali ya Viongozi pale Kijitonyama (kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Rais kwa umma) siku ya tarehe 31/12/2009.

  Pamoja na mema yote aliyoifanyia nchi yetu na uadilifu wake usiokuwa na mashaka yoyote, lakini amesahaulika haraka sana na inaonekana kuwa kama taifa tumeamua kutomuenzi kabisa. Nayasema haya kwa uchungu kwani wakati akitimiza mwaka mmoja toka kufariki hakuna tulichofanya kama taifa kumkumbuka shujaa na Mzee wetu huyu.

  Binafsi nilipendekeza siku aliyokufa kuwa tuwe na KAWAWA DAY KILA TAREHE 31/12 YA KILA MWAKA.

  Natumaini hatutayarudia tena makosa haya mwaka huu.
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Duh itakuwa poa sana tukitoka break ya Christmas, Boxing Day tunamalizia na mwisho wa mwaka yaani Kawawa Day tarehe 31/12 then kesho yake New Year tarehe 01/01. Wazo lako limepitishwa mkuu!
   
 3. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maana na nia yangu si kupata siku ya ziada ya kupumzika bali ni kuhakikisha kuwa taifa letu linaendelea kumkumbuka shujaa wetu na kuhakikisha kuwa vizazi na vizazi vinaelimishwa na kuufahamu kwa ukamilifu wake mchango wa Simba wa Vita kwa taifa letu.
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Tunamuenzi sana Simba wa vita na ndio maana tumewapeleka wanawe wawili kwenye BUNGE letu kule Dodoma; kama vile tulivyompeleka binti Sokoine pia!!!!
   
 5. b

  binti ashura Senior Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndugu una mawazo mazuri lakini kumbuka tutakuwa nao wengi sana badae tutakuwa hatufanyi kazi!.
   
 6. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Si sahihi kusema hivyo kwani mchango wa Mzee Kawawa kwa taifa hili ni wa kipekee. Anastahili kukumbukwa kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali katika kumuenzi. Kwa Upande wa viongozi mpaka sasa ni viongozi wawili ambao siku walizofariki ndiyo siku za mapumziko (Nyerere na Karume). Kwangu mimi Mzee Kawawa anastahili kuwa katika kundi hili.
   
Loading...