Elections 2010 Watanzania wenzangu tusifanye mzaha huu ni mwaka wa kufanya maamuzi makini

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu zangu watanzania,

Tuache ushabiki usio na mantiki. Tusibadili siasa kuwa kama ushabiki wa Simba na Yanga. Wenzetu waghana ilifika wakati wakaacha ushabiki wa kijinga wakaunga mkono chama cha upinzani na ukawa mwanzo wa maendeleo tunayoshuhudia leo. Hivi sasa, Ghana ni miongoni mwa nchi zenye demokrasia makini na faida zake za kiuchumi zimeanza kujitokeza. Ndiyo maana hata Rais Obama wa Marekani aliamua kuitembelea Ghana ikiwa ni nchi ya kwanza kuitembelea tangu ashike madaraka ya kuongoza taifa kubwa la Marekani. Maneno yaliyokuwa yakitamkwa na chama tawala kwamba mkiwachagua wapinzani wataleta vita na mifarakano nchini. Hivi sasa, wananchi wameng'amua kuwa huo ulikuwa ni ujanja tu wa chama tawala.

Hivi sasa, ni miaka takriban 50 tangu tupate uhuru lakini wananchi wanazidi kuwa maskini siku hadi siku. Pamoja na utajiri mkubwa wa rasilimali za madini, wanyama, ardhi yenye rutuba, n.k. wananchi bado ni maskini wa kutupwa. Ni jambo lisilofichika kuwa Mhe. Mkapa alijitahidi sana kujenga uchumi na hata wakati anaondoka wataalam wa uchumi wanatuambia aliacha akiba nzuri ya fedha za kigeni. Kilichotarajiwa na wananchi wengi ni kuwa kikwete angeendeleza jitihada zilizofanywa na Mhe. Mkapa lakini aliyofanya kikwete ni madudu matupu. Wananchi wote ni mashahidi wa haya ninayosema. Maisha yameendelea kuwa magumu siku hadi siku. Kinachotakiwa sasa ni ukombozi wa nchi.

Tarehe 31 Oktoba 2010 tufanye uamuzi mgumu tulioshindwa kuufanywa miaka ya nyuma kwa uwoga uliosababishwa na propaganda za ccm. Tumeona wenzetu waghana, wakenya, wamalawi, wazambia, n.k. kwa nini sisi tushindwe ndugu zangu. Mwaka huu lazima tufanye maamuzi kwa kumchagua Dr. Slaa ambaye rekodi yake kiutendaji inafahamika kila kona ya nchi hii. Utendaji wa Dr. Slaa umeitikisa ccm kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea. Kilichobaki sasa ni kumpatia Dr. Slaa madaraka kamili ili asafishe uchafu wote uliozagaa nchini na kuwakomboa wananchi walio kwenye lindi la umaskini.

Shime wananchi tuachane na propaganda za ccm zinazomchafua Dr. Slaa na Chadema za udini, ukabila na n.k. Tanzania bila ccm inawezekana.
 
Ghana walikuwa na chama makini mbadala. Hapa Tza bado hakuna chama makini cha kuachiwa nchi.
Bora CCM waendelee, wamejipang vizuri.
Unadhani uongozi wa nchi ni wa kujaribu na kumpa mtu wa hivihivi? Halafu waanze kuzozana katika kugombea nafasi za uongozi wa nchi?
No way, hatutakubali. Watanzania tulio wengi tunataka nchi yetu iendelee kuwa na amani na maendeleo endelevu.
Mungu Ibariki Tz. Kitakapojitokeza chama kilicho komaa, kiwe Chadema, CUF, NCCR or TLP, na tukihakikisha kuwa kuna VIONGOZI wanaoweza kuaminiwa kukabidhiwa nchi, tutawapisha kwa kuwapigia kura nyiingi.
NOT NOW.
 
Nimekusamehe bure!!!
 
Back
Top Bottom