Watanzania wenzangu tupewe nini ili tuache kulalamika?

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Miaka kadhaa watu walimchukia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kumsema vibaya kila kona, lakini leo hii yupo Rais Magufuli bado tu watu wanalalamika kila kona.

Sasa sijui aje Rais gani tena au ndiyo unafiki wa Watanzania na kulalamika kila kukicha.

Mimi kama Mtanzania mwenzenu nataka kufahamu ni kipi hasa hitaji lenu nyie watu wa humu mtandaoni mnachokitaka hasa na mwishoe mtaacha kupiga kelele na kuisema vibaya serikali.

Nawasilisha.
 
Uhuru wa kuongea, kuandamana, mikutano ya kisiasa na vitu kama hivyo bila kusisitiza kufanya kazi.

Mwisho serikali iache kujenga vitu badala yake ituletee hela mkononi baada ya maandamano.

Kwa ujumla bata kwa sana in ZZK voice!
 
Miaka kadhaa watu walimchukia JK na kumsema vibaya kila kona,lakini leo hii yupo JPM bado tu watu wanalalamika kila kona .Sasa sijui aje Rais gani tena au ndiyo unafiki Wa Watanzania na kulalamika kila kukicha.Mimi kama mtanzania mwenzenu nataka kufahamu ni kipi hasa hitaji lenu nyie watu wa humu mtandaoni mnachokitaka hasa na mwishoe mtaacha kupiga kelele na kuisema vibaya serikali.Nawasilisha.
Mazaga,

Mimi na wengi hapa lalamiko ni uonevu na demokrasia yetu.
 
mazaga one,
Wapewe wapiga polishi na wachoma mishikaki uongozi, maana toka ujambazi uthibitiwe na magamushi mengine hali zao zimekuwa za kuwashwa washwa
 
Miaka kadhaa watu walimchukia JK na kumsema vibaya kila kona,lakini leo hii yupo JPM bado tu watu wanalalamika kila kona .Sasa sijui aje Rais gani tena au ndiyo unafiki Wa Watanzania na kulalamika kila kukicha.Mimi kama mtanzania mwenzenu nataka kufahamu ni kipi hasa hitaji lenu nyie watu wa humu mtandaoni mnachokitaka hasa na mwishoe mtaacha kupiga kelele na kuisema vibaya serikali.Nawasilisha.

Kwanza tunashukuru kwa kujua kwamba tunalalamika, ni kweli katika malalamiko yetu hujaona ni kipi tunalalamikia? Tunataka haki yetu na uhuru wetu wa kuhoji na kumchagua tumtakaye. Hatuko tayari kwa katiba inayompa rais umungu mtu, kuna maoni yetu yalikusanywa na tume ya jaji Warioba japo yalichakachuliwa, lakini kuna katiba iliyo pending, ije hiyo.

Kwa ujumla hatuko tayari tena kuongozwa na chama kuitwacho ccm, lakini hatutaki kuitoa kwa machafuko, ndio maana tunataka box la kura liheshimiwe tuwatoe kwa amani. Lakini inaonekana ccm haiko tayari kutoka na hata kutoka kwa amani ndio maana wanaendelesha chaguzi za kikatili na kihayawani, na kuishia kunajisi chaguzi za nchi hii mfano uchaguzi wa SM. Hivyo msishangae watu kuendelea kulalamika na kutoridhika, ni kwakuwa mmeshindwa kutambua kanuni ya wakati kwamba wakati ni ukuta, huku mkilazimisha kutawala bila ridhaa ya wananchi.
 
UNAFIKI:...Unafiki ni utovu wa ukweli katika mwenendo wa binadamu hasa kwa lengo la kujipatia sifa, k. mf. kama mwanadini mwadilifu. Tofauti na mkosefu, mnafiki anatenda vema kwa nje, lakini nia yake si kufuata dhamiri yake na maadili anayojua ni mazuri, bali ni kupendeza watu wengine ili kupata faida fulani kutoka kwao. Wikipedia
unapoona jambo fulani halipo sawa na kusema sasa wewe unakuwa mnafiki? mkuu wewe ndo unakuwa mnafiki wa kwanza katika taifa hili
 
..dhana kwamba tunatakiwa " KUPEWA " kitu / vitu fulani inadhihirisha kwamba hatuko sawasawa ktk fikra zetu. Ni dhana ya KINYONGE na KITUMWA.

.
 
Uhuru wa kuongea, kuandamana, mikutano ya kisiasa na vitu kama hivyo bila kusisitiza kufanya kazi.

Mwisho serikali iache kujenga vitu badala yake ituletee hela mkononi baada ya maandamano.

Kwa ujumla bata kwa sana in ZZK voice!

Acha upotoshaji, Kwanza uhuru wa kuongea, kuandamana, mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba na sio kosa kisheria wala hisani ya mtu au kiongozi yoyote yule. Hakuna yoyote asiyefanya kazi, maana hakuna mtu amewahi kuwapelekea viongozi familia zako ili wawape chakula kisa hawafanyi kazi. Na hakuna popote serikali imezuiwa kujenga chochote zaidi ya watu kutumia haki yao kuhoji utekelezaji wa vipaumbele, na namna ya utekelezaji. Onyesha mtu aliyekwenda na sururu kubomoa barabara, au kubeba nyundo kwenda kubomoa darasa.

Ni hivi hatuko tayari kuongozwa na chama chochote bila ridhaa yetu. Mnanajisi box la kura na kuleta viongozi ambao hawana ridhaa ya watu, matokeo yake zinatumika nguvu nyingi kulazimisha kutawala watu wasiowakubali. Ukiona malalamiko hayaishi, jiulize hao viongozi walio madarakani wamechaguliwa kihalali na watu, au ni zao la uchakachuaji na chaguzi za kikatili na unyama?
 
Miaka kadhaa watu walimchukia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kumsema vibaya kila kona, lakini leo hii yupo Rais Magufuli bado tu watu wanalalamika kila kona.

Sasa sijui aje Rais gani tena au ndiyo unafiki wa Watanzania na kulalamika kila kukicha.

Mimi kama Mtanzania mwenzenu nataka kufahamu ni kipi hasa hitaji lenu nyie watu wa humu mtandaoni mnachokitaka hasa na mwishoe mtaacha kupiga kelele na kuisema vibaya serikali.

Nawasilisha.
Uhuru!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ya tano ikimaliza muda wake mtaendelea na huo upuuzi,kwa sasa "BIG NO"

Sent using Jamii Forums mobile app

Haki ni upuuzi ndani ya awamu hii ya tano!? Sasa kama unaamini haki ni upuuzi, unatarajia nini watu wanapoamua kuihoji haki yao? Kama awamu hii ya tano inaona haki ni upuuzi, basi ivumilie kelele zisizoisha wala isitegemee kusikia sifa yoyote zaidi ya kero.
 
Nakumbuka waziri wa michezo Dr. Mwakyembe ambaye historia haitamuacha kumkumbuka kama ni mmoja wa wasomi waliokuja kupingana na maandiko yake kwa kujali maslahi ya chama, kuhusu muungano.

akiwa bungeni alilalamika sana watu kumnyonya marehemu Mzee Majuto.

maendeleo hayana vyama.

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Miaka kadhaa watu walimchukia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kumsema vibaya kila kona, lakini leo hii yupo Rais Magufuli bado tu watu wanalalamika kila kona.

Sasa sijui aje Rais gani tena au ndiyo unafiki wa Watanzania na kulalamika kila kukicha.

Mimi kama Mtanzania mwenzenu nataka kufahamu ni kipi hasa hitaji lenu nyie watu wa humu mtandaoni mnachokitaka hasa na mwishoe mtaacha kupiga kelele na kuisema vibaya serikali.

Nawasilisha.
Hivi kweli Roma mkatoriki akisoma huu uzi atakuelewa? Hivi ndugu za Tundu Lissu wakisoma huu uzi watakuelewa? Hivi unajua kuwa Ben Saa nane alikuwa ameowa na alikuwa na wazazi? Viongozi wa Chadema ndo walifyatua risasi ya smg ikamuuwa Akwilina? Hujui kuwa Bashite Hana cheti Cha form four? Je waliotumia vyeti vya sekondari vya ndugu na jamaa wakajiendeleza wakawa madakitari,manesi na walimu Leo wako wapi?
 
Maitaji ya wananchi kwa sasa hivi ni kurudisha mfumo wa demokrasia maendeleo yanayoletwa kwa sasa hivi yataboreshwa na mfumo wa demokrasia maana katika mfumo huu unashirikisha raia wote wa Tanzania ya bila ubaguzi
 
Wafuasi wengi wa ccm ni viumbe wa ajabu sana! Eti hawafahamu ni kwa nini Watanzania wanalalamika! Mlitaka tucheke, tulie au tuwe mabubu kwa haya madudu yenu mengi mnayo yafanya hasa awamu hii?

Siku mtakapo tuachia nchi yetu, ndiyo itakua mwisho wetu wa kulalamika.
 
Sio kweli.Nimekaa nakuwaza kwanini humu mnalalamika lakini mkiambiwa mseme hamsemi sasa tuelewaje?
 
Acha uongo Wakat wa JK
Malalamiko Hayakua Mengi kama Sasa

Pia Malalamiko yenyewe hayakua na Hoja
Nyinyi humu hamkulalamika kuhusu safari za nje?? Humu ndani hamkulalamika tuwe na ndege???? Humu hamkulalamika upigaji bandarini?? Humu ndani hamkulalamika kuhusu usafiri Wa Reli???? Humu ndani hamkulalamikia baraza LA mawaziri kuwa kubwa??? Sasa hayo yote JPM kafanya na karekebisha nini tena tunataka Watanzania wenzangu??
 
Back
Top Bottom