Watanzania wenzangu shime tufanye mapinduzi ya kizalendo ,dola ni sisi wananchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wenzangu shime tufanye mapinduzi ya kizalendo ,dola ni sisi wananchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saggy, Feb 11, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwakweli imedhihirika wazi kwamba Tanzania inahitaji Mapinduzi ya Kizalendo kwa haraka kuliko katiba Mpya,Katiba is just a peace of paper,kama kuna anayebisha aniambie ni kifungu gani katika katiba ya Egypt kimewaruhusu wananchi wa Misri kumweondoa Mubarak madarakani?Hoja si katiba,pamoja na katiba mpya ni lazima wanachi tujue kwamba sisi ndio dola yenyewe na tukiamua jambo wakati wowote tunafanya bila kungoja tukae na kubadilisha vifungu vya maandishi.

  Jamani mimi natoa wito kwa Watanzania wote kuamka na kufanya Mapinduzi ya Kizalendo kuikomboa nchi yetu mikononi mwa wanyang'anyi wa mali yetu.

  Napenda kuwakumbusha wanachi kwamba DOLA ni Wananchi na "Katiba",Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Majeshi likiwemo la Polisi lililouwa watu Arusha na Zanzibar ni Vyombo vya DOLA na DOLA ni WANANCHI kwanini tunaogopa vyombo vyetu?wewe unaweza kuogopa bakuli na sahani,kisu,jembe ambayo ni vyombo vyako mwenyewe?Shime wananchi tufanye Mapinduzi ya Kizalendo na tuwafukuze madarakani Watawala dharimu bila kujali Vyama vyao wala itikadi zao ikiwa hawatekelezi matakwa yetu sisi ambo ni DOLA

  Tuna haja gani ya kukaa majukwaani kujadili mabadiliko ya Katiba wakati tunaendelea kuangamia,tuamke tuseme sisi ndio Dola na hakuna haja ya kuomba kibali kwa vyombo vyetu wenyewe,kila mtanzania leo ajue sisi ndio DOLA yenyewe napenda kurudia tena sisi WANANCHI ndio Dola,sisi ndio DOLA Watanzania wenzangu,kwanini tunaogopa vyombo vya DOLA? Wakati Dola ni sisi Wananchi? Shime tufanye maandamano makubwa nchi nzima


  Tuamke sasa tuwaambie wanasiasa wote bila kujali ni Chedema au CCM au CUF tumechoka na maneno yenu.

  Saa imefika ya Mapinduzi ya Kizalendo ambapo hautangoja Miaka Mi 5 au 10 Kumwondoa mtu madarakani wakati tumemwona anafanya mengine ambayo hatukumtuma sisi,ATAONDOKA hata kama Katiba haisemi hivyo kwakuwa WANACHI ndio Dola yenyeweeeeeeeeee

  Shime wana jamii wenzangu,tuwaambie wanachi wote kwamba sisi ndio DOLA na kamwe tusiogope Vyombo vyetu kama Polisi,Jeshi na etc

  Natangaza kufanyika kwa maandamano makubwa nchi nzima siku ya tarehe 19 Jumosi ya Wiki ijayo,2011 kuishinikiza serikali iliyopo iondoke madarakani kama haitafanya yafuatayo

  1.Kukomesha mgawo wa Umeme haraka iwezekanavyo ndani ya siku 7

  2.Kushughulikia haraka matatizo ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu ikiwa ni pamoja Kuwaongezea Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya JUU posho ya Kujikimu kutoka TZS.5000 hadi TZS.15,000 kwa siku.

  3.Kutoa tamko kuhusu namna watavyoshughulikia tatizo la AJIRA kwa maelfu ya Vijana waliohitimu katika Vyuo mbalimbali

  4.Kuwakamata na kuwaweka ndani watuhumiwa wote wa Ufisadi kuanzia IPTL,Richmond,Dowans,Meremeta na wengine

  5.Kuwafukuza wawekezaji wote wanotuibia madini yetu kwenye Migodi yote nchi nzima ama lasivyo wanachi watavamia migodi yote kuanzia tarehe 19/02/2011

  6.Kushugulikia matatizo ya Walimu,kama ukosefu wa Nyumba,kutolipwa Posho na madai yao mbalimbali.

  7.Kuwakamata wezi wa Ruzuku za Pembejeo za Kilimo

  8.Kufufua usafiri wa Reli na Kurudisha vichwa na Mitambo ya shirika vilivyoibiwa na Wawekezaji wa TRL kutoka India

  9.Bunge livunjwe na kuitishwa uchaguzi mpya kwakuwa kulikuwa na dosari kubwa

  10.Kuundwa kwa Taifa Jipya la Tanganyika baada ya mabadiliko ya katiba yaliyozaa Zanzibar huru.

  11.Kujiuzuru kwa waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa jeshi la Polisi kwa kosa la kuhamasisha mauaji ya wananchi wasio na hatia Arusha.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka uko sahihi kabsaa hiyo ndo solution ya kuwatoa hawa wezi wa kura na historia ya muungano feki.
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mkuu wazo zuri iiiila???
   
 4. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kwa Bongo tu, yatatakiwa maji ya kunywa lita milioni 100 kwa siku 10, hapo bado mchele na maharagwe, ... upo hapo?
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ilaaaa nashindwa kumuelewa anataka maandamano hataki katiba wakati hata hayo maandamano yanatakiwa yafate utaratibu kutokana na katiba inavyosema.
  Yaani huyu anapewa bakuli zima la nyama halafu yeye anachagua kipande kimoja tu vingine vyote anaacha na mchuzi anamwaga. Lol!
   
 6. s

  saggy Senior Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nataka katiba Mpya,but nadhani hujanielewa mkazo wangu ni upi,nataka kukazia swala la mapinduzi ya Kizalendo ambayo hayahitaji Katiba,wakati wazee wetu akina mkwawa,Mangi na wengineo wanapigania uhuru walitumia kifungu gani cha katiba?jenga hoja hapo nikuelewe Bwana,umehoji swala la Msingi sana lakini..!!!

  Hapa ni hivi,Dola ni wanachi na Haki yao haiwezi kungoja mabadiliko ya Katiba,hata kama Kiongozi anatakiwa kutawala miaka mingapi kwa mujibu wa katiba,kama wanachi wamemchoko hata kama ni within a week wanapaswa kuwa na nguvu ya kumtoa bila kujali mabadiliko ya katiba yamefanyika au bado,hayo ni badaye,so ki msingi naunga mkono mabadiliko ya Katiba but nadhani Mapinduzi ya Kizalendo ni muhimu kwanza kabla ya mabadiliko hayo.

  Wanasiasa wajue kwamba any time wakituchezea wananchi tutawaondosha madarakani hata kama katiba inawalinda,DOLA ni wananchi na si Katiba,hii inadhihirika wazi kwa tukio la Misri na Tunisia,Haki ya wananchi kuandamana au kumtoa kiongozi madarakani haitokani na maandishi yaliyomo ndani ya katiba yanayompatia haki ya kuandamana bali ni Haki inayotokana na kwamba yeye mwanchi ndiye DOLA yenyewe na ndiye mwenye kumiliki nchi na ndiye aliyeweka madarakani serikali so it is "ownership right" so wanasiasa wakijua kwamba wananchi wanajua kwamba wao ni DOLA hawatatuchezea tena!!!
   
 7. escober

  escober JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  good idea
   
 8. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wazo safi sana na murua kabisa
   
Loading...