Watanzania wenzangu kumbe inawezekana!!!(yobu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wenzangu kumbe inawezekana!!!(yobu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ramson34, May 6, 2010.

 1. r

  ramson34 Senior Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hallow Wandugu,
  Habari za LEO?
  Naomba niwashirikishe jambo moja ambalo kwa kweli ni kitu cha ubunifu tu.
  Swala la foleni za magari barabarani katika jiji letu la DSM limekuwa sasa ni KERO kubwa yenye kuhitaji watu ambao ni CREATIVE and ACTIVE and more than tha wenye HEKIMA na kuongozwa na MUNGU katika kutatua tatizo hili moja katika mengi ambayo yanatukabili wananchi wa DAR ES SALAAM. Kutokana na UGENI na habari kwamba barabara zitafungwa basi juzi, jana na leo kuna WATANZANIA waaminifu kweli kweli wanaamka mapema sana na kuwahi makazini kwao na wengine wamepanga kuingia kazini kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri na kutoka saa nane kwa kweli hii nimeipenda na yaweza kuwa ni moja ya DAWA ya foleni badala ya watu wote kuingia ofisini (muda mmoja) yaani saa mbili. Hii naiona ni nzuri kwa hiyo kwa wale wote au zile ofisi na makampuni yenye uwezo wa kuendeleza hili/ hii ratiba tafadhali endeleeni.
  Siku hizi foleni ziko kila mahali na ni kila wakati huwezi ukatoka Mwenge ukaenda mjini ukatumia dk 10 ambazo ndio muda wa wastani wa kwenda mjini from Mwenge. Sasa inashangaza tutafikiaje hayo maendeleo while we are wasting a lot of time mabarabarani pamoja na gharama kubwa ya mafuta.
  Hii yote ni kutokana na MIUNDO MBINU hafifu ambazo ni chache na hakuna uboreshaji wala kuongezwa kutokana na kupanuka kwa jiji la Dar es Salaam na vilevile ni kutokana na kuwa na viongozi ambao hawana UPEO wala aibu ya kujua matakwa na mahitaji ya wananchi ambao ndio WAAJIRI wao katika nafasi walizo nazo kuanzia POLITICAL LEADERS na hata TECHNOCRATS nao wanashindwa kufanya maamuzi ya msingi katika nchi hii mabayo yanaweza kuongeza TIJA na kuinua hali ya uchumi wa nchi yetu yenye UTAJIRI lukuki.
  Mara nyingi huwa ninaogopa sana nikihusishanisha mambo yalivyo na haswa nikiangalia we have everything MUNGU ametupa rasilimali nyingi ambazo nyingi tunashindwa kuzitumia yaani inafika mahali ninaoanisha na ile habari katika BIBLIA ya wale waliopewa TALANTA wengine wakazifanyia kazi na kuzalisha mwingine akaweka pengine alikuwa mvivu wa kufanya kazi na hata kufikiri na ndicho tunachokiona hata leo hapa Dar es Salaam na Tanzania yote kwa ujumla.
  Kuna methali au msemo wa kiswahili usemao MGENI AJE MWENYEJI.............
  nimeshangaa sana pale ambapo wageni wanapofika au wanapokuja nchini kwetu yaani usafi unafanyika barabara kabisa lakini hii ni DESTURI gani na ya wapi? Usafi unafanyika tu pale mgeni ajapo? Au ndio FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU..............? Hakika Watanzania tunapaswa kubadilika. Hata Usafi wa kufagi barabara unafanywa vizuri pale wageni wajapo nchini hii kwa kweli ni AIBU. Nimeshangaa kuona miti (Palm Trees) ZIKIPANDWA sam Nujoma Road zikiwa kubwa na tena zikipandwa kwa WINCH hakika inabidi niwaulize ndugu zangu wa SUA kama zitaota. Lakini nikajiuliza ya nini yote haya? Ni kwa ajili ya hawa wageni tu watakaokuja kwa ajili ya mkutano wa WEF tu? Je Watanzania hawapendi USAFI wala kuwa na MITI mizuri kwenye barabara zetu? Cha kushangaza zaidi barabara zetu nyingi hazina TRAFIC LIGHTS au TAA za barabarani AMBAZO NI MUHIMU sana kuwepo kwenye kila barabara kwa ajili ya usalama wa watumia barabara.
  Palm Trees zilizopandwa SAM Nujoma Road zikiwa kubwa kwa ajili ya wageni, Si zingepandwa kwa utaalamu tu zikiwa ndogo na zikatunzwa vizuri pamoja na miti mingine kwa ajili ya afya zetu na kwa kusaidia kunyonya HEWA CHAFU kutoka kwenye magari na urembo na na sio kwa ajili ya wageni? Je sisi wenyewe hatuhitaji vitu na mazingira mazuri?
  Imenishangaza kweli pale ambapo hata kiongozi kama Waziri Mkuu na hata Mkuu wa Mkoa wanapofanya ziara za kukagua usafi kwa ajili ya wageni mimi ninajiuliza je haya hayawezekani kufanyika ni hadi pale Viongozi na wageni wa nje wanapokuja nchini kwetu Tanzania?
  Ninaona ni vema usafi ukafanyika kila siku na ikajengwa tabia na desturi ya kupenda USAFI wa mazingira na makazi yetu ili tuishi kwa furaha na amani and FREE from Diseases. Hat malaria na kipindupindu magonjwa haya yangeweza kupungua kwa kiasi kikubwa sana ikiwa tutaweza kuzingatia USAFI.
  Barabara za DSM hata City Centre imagine Azikiwe Street mbele ya CRDB Bank kuna mashimo kama mahandaki mbele ya Jengo la Haidery Plaza hadi maji machafu ya Vyooni yanatiririka barabarani mjini kabisa sehemu ambayo ni very busy na inatumiwa na watu wengi INACHUKUA MORE THAN 6 MONTHS KUTENGENEZWA unaweza kujiuliza je kuna VIONGOZI kweli? na je hakuna viongozi au wamiliki wa majengo hayo wanaweza kurekebisha mapungufu hayo?
  Inatia HASIRA kweli kweli ingelikuwa ni nchi nyingine au jamii nyingine hata watu wasingeingia kwenye Bank hii wala jengo hilo na ikaitokea hivyo basi wahusika watawajibika mara moja kutokana na SHINIKIZO la wenye MAJENGO, Biashara na WANANCHI kwa ujumla.
  Nisizungumze mengi kwa sababu hayataisha maana kwa kweli ufumbuzi wa haya yote ni sisi WANANCHI tukiamua INAWEZEKANA kufanya mabadiliko makubwa sana na kuweka mambo sawa na wananchi wa NCHI hii wakayaona hayo maisha BORA ambayo wanayasikia tu na wengi hawajui yatakuja lini. Viongozi kama mmoja wao alioulizwa siku za hivi karibuni juu ya shida na kero za mitaro kuziba na miundo mbinu hafifu katika jiji la DSM je kuna mikakati/mipango gani iliyoko kutatua matatizo haya ambayo mara nyingi yanatokea DSM kutokana na Mvua ambapo maji hukusa mwelekeo kutokana na miundo mbinu hafifu na chakavu na huyu mheshimiwa wa JIJI kujibu kuwa matatizo kama haya yako katika MIJI yote DUNIANI kwa hiyo kwake yeye ni kama jambo la kawaida na kutufanya as if WATANZANIA WENGINE WOTE NI wajinga na washamba kiasi kwamba hawajawahi kufika au kutembelea miji mingine hivyo yeye ni bingwa wa kutembelea miji mbalimbali Duniani na wao wana shida kama hizi kwa hiyo wananchi waendelee kupata shida ya mafuriko pasipo kujua hatima yake labda mpaka hapo NEEMA ya MUNGU itakapowashukia.
  Tuendelee kufanya ASSESSMENT ya hawa tuliowapa kazi 2005 ya kutuongoza na tusisahau Mwaka huu ni ule mwaka wa ku-renew zile CONTRACT zao. Hivyo ni jukumu letu sisi wenyewe kufanya TATHMINI na kuleta MABADILIKO ya kweli.
  MAENDELEO ya nchi yetu yataletwa na sisi WANANCHI wenyewe.
  Kazi njema na MUNGU atubariki sote.
  Regards,
  Yobu
   
 2. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bravo!! Nakupa senks kwa kuueleza ukweli!
  Ni kweli, sisi wenyewe tukiamua TUTAWEZA!!
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu inatumia mfumo wa mzungu four. Yaani familia ikiongezeka badala ya kuongeza vitanda tunalala kwa kupishana. Na serikali ikikosa mapato kwa sababu ya uzembe wa baba mwenye nyumba basi tunalazimishwa kufunga mikanda tumbo lirudi ndani ili tusile kingi kukabliana na hali halisi. Huu ndio ukomo wa kufikiri wa serikali ya mtu mweusi ndg. Vyombo vizuri kabatini ndani ya nyumba ya mpumbavu ni kwa ajili ya mgeni lakini kwa mwelevu ni kwa ajili ya watoto wa nyumbani. Shame on us we africans!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Habari ndi hiyo!
  Tanzania ni sawa na nchi ya koloni inayotawaliwa, hatujui uchumi wake unapelekwa wapi maanake ndivyo tulivyofundishwa kuhusu umaskini wetu wakati wa mkoloni. Tuliwaondoa wakoloni kwa imani kwamba walikuwa wakituibia mali zetu na kupeleka makwao, leo hii tunaibiwa sijui hizo mali zinapelekwa wapi.
  Hii tabia ya kuamka saa kumi kwenda makazini ni asili yetu toka wakati wa Ukoloni. Wazee wetu walikuwa wakiamka saa kumi usiku na kujiandaa kwenda shamba kulima na hurudi mida ya saa tisa mchana jua linapochanganya. Moja ya sababu kubwa ilikuwa kukosekana kwa Usafiri hivyo ubunifu wa matumizi ya muda ilifuatana na ukosekanaji wa usafiri..

  Sasa leo tunapoambiwa kwamba nchi imeendelea hali muda wa kufanya kazi unazidi kupungua, uzalishaji unazidi kupungua na tunachojivunia ni uagizaji mkubwa wa mali toka nje tukilipa kwa fedha za mikopo, sijui haya maendeleo yanayozungumziwa yana faida gani kwa mwananchi mwisho wa siku kama sii kulimbikiza madeni ambayo hatuna uwezo wa kuyalipa isipokuwa kujiingiza tena ktk mikataba inayotufunga zaidi kiuchumi ili tupate misamaha.

  Mkuu wangu hakuna Ubunifu usiofuatana na Miundombinu. Hata ardhi na viwanja hupata thamani tu pale ardhi hiyo imepimwa kwa matumizi ikafuatia uboreshaji wa barabara yenye mifereji ya maji taka, mabomba ya maji na umeme. Walimcheka sana mwalimu alipoanzisha vijiji vya Ujamaa na hata wakathubutu kusema yalikuwa mawazo ya Kikomunist hali Urbanisation imetumika ktk miundomiji duniani kwa kuzingatia kuepuka matatizo kama haya tulokuwa nayo. Sisi hatukuona huko pamoja na umaskini wetu wa akili.

  Sasa nenda vijijini ukajionee mwenyewe demographic. Watu wameondoka rural area kuhamia mijini. Less than 10% ya vijana wa kati ya umri wa miaka 15 hadi 20 wanaishi vijijini. Kifupi hakuna vijana wanaoishi vijijini isipokuwa wale wadogo ambao bado wanategemea malezi ya wazazi wao. Hata miji midogo ya wilaya imeathirika kwa kupoteza vijana wao wakikimbilia miji mikubwa ya mkoa. Na kwa sababu mijini hakuna kazi, uhamiaji huu umezua tatizo jingine kubwa la - Ujambazi mijini. Hii sii bahati mbaya wala sii swala la tabia ya vijana waliotoka vijijini kuwa ni majambazi isipokuwa ni matokeo ya hali halisi ya mipango mibovu ya kimaendeleo kitaifa na mawazo mgando ya viongozi na wananchi ambao wanaamini kabisa kwamba maisha yapo mjini.

  Ebu tazama sababu zinazotolewa kutohamishia Makao makuu ya Taifa Dodoma. Ni upumbavu mtupu uliojaa Ulimbukeni..Kama makao makuu ya taifa yatahamia Dodoma nusu ya mji wa Dar es Salaam utapumua. huu ni mji mkuu wa biashara, mji usiohitaji milolongo ya misafara ya rais na mawaziri wake kila kukicha..Ardhi kubwa kuhodhiwa na ofisi za wizara, Jeshi, mabalozi ili mradi mji mzima ni makao makuu ya ofisi ambazo zinapunguza nguvu ya mzunguko wa fedha na biashara ya mji huu. Jeshi pekee limekamata karibu 1/8 ya eneo la mji wa Dar nzima hali hakuna sababu kabisa ya mji mkuu wa biahsra kuwa na kambi za jeshi kiasi hicho kama makao makuu yatahamia Dodoma. Na kifupi hakuna nchi yeyote iliyoendelea Duniani yenye makoa makuu ktk mji mkuu - HAKUNA isipokuwa Tanzania na tunajenga sababu za kijinga kabisa kuhalalisha Ulimbukeni wetu..Ati mji wa Dodoma hauna MAJI ndio sababu ya kufuta kabisa mpango mzima wa kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma. Siwezi hata kufikiria ingekuwa vipi kama makao makuu ya Marekani yangekuwa New York ama LA, Uingereza pale London sijui.

  Hivyo mkuu wangu, wanaposema wenzetu kwamba necessity is the mother of invention hawana maana ya ubunifu unaokwepa shida bali ubunifu unaotafuta suluhisho la shida iliyopo. Kuamka saa kumi usiku KUEPA traffic sii ubunifu bali ni mbinu za mkato kukwepa shida iliyopo na ndio mfumo unaotumika sana nchi maskini wa kufikiri. Hatutaki kuzichosha akili zetu kutafuta suluhisho la matatizo yetu kwa sababu ya Ubinafsi na siku zote makosa sii yetu bali ya umaskini wetu. Ndio kisingizio kikubwa, utasikia hatuna uwezo hali wao viongozi wakijenga mahekalu yenye thamani kupita kipato cha wizara wanayoiongoza. Uzalishaji unapopungua, tunafunga na kuuza viwanda hata kama soko lipo hatutaki taabu makosa ni ya kiwanda kutozalisha.
  Hili ndilo taifa la Wadanganyika - Karibu tena Ramson.
   
 5. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mi ishakuwa story ndefu naachilia kati .... summary jamani.
   
Loading...