Hata kama Rais Samia haumkubali, si sahihi kumpuuza na kumwandikia jumbe zisizo na staha

Maoni ya mtu binafsi yanakubaliwa kikatiba, hatuwezi kuwazuiwa wananchi wasitoe hisia zao huu ndio uwazi na faida za mitandao. Ila staha ni wajibu wa kila mtu hapo sasa mtu anatoka nje wa ruhusa ya kikatiba. Kwani katiba hairuhusu kuwaudhi wengine au mwingine. Ukiwa Rais unakuwa jalala na ndio Urais wenyewe. Mengi ni ya kupuuza na kuna machache yana maana au ujumbe ndani yake. Kuna kilio cha waliachwa mayatima na utawala uliopita hawa wataelewa taratibu nchi haipo kwao tena na ndio maana ya demokrasia hakuna mtu anaeweza kuhudhi madaraka yote kwa kipindi zaidi ya katiba ya sasa inavyosema. Hili kwao nawapa pole. Utawala wa sasa haujapoteza direction ila inabidi kuwaelewa kwa kupima matokeo, muda nimfupi mno kuwapima hata kupendekeza huyu aondolewe au huyi hivi kwani pia sio kazi ya wananchi ila kiongozi mkuu. Nampongeza sana Rais wa sasa kwa uvumilivu alio nao kwani kipindi kile wengi wangekuwa wameshazolewa na wasijulikana na hawajulikani walipo.
 
Kumstahi na kumpa heshima yake kunahusiana vipi na kueleza tatizo liko wapi? Au unaona ukieleza tatizo pasipo kumkosea heshima hatasikia?
Lengo la kuchagua Rais siyo tumpe heshima bali asimamie haki na ajenge nchi yetu na hivyo ndiyo vina sababisha kueshimiwa au kutokueshimiwa kwake
 
Umeibuka utamaduni wa wengi pale inapotokea mada imuhusuyo mheshimiwa Rais Samia walio wengi wamekuwa wakimbeza na kujibu yamhusuyo pasi na staha.

Hakika hiyo tabia si ya kiuungwana na sote kwa umoja wetu tuikemee.

Samia ni dada,mama,shangazi lakini pia ni mke.Shime tusiutweze utu wake.

Na hata kama hana uwezo wa kuongoza kama Viongozi wengine waliopata kuwa lakini bado ni kiongozi wetu.

Mungu ibariki Tanzania.

Nb: Gesi ya Mtwara wazungu walishafanyaga yao kitambo!
Ulichomalizia ni ukweli unaoumiza, usitutoneshe donda mkuu
 
Hata Hitler alikufa na cheo namba moja,unadhan mbele ya Mungu kuna cheo no.1 na ya mwisho????
︎ Ndiyo hivyo sasa aliwateua 11 na haukumfanya kitu, na hata sasa hauna cha kumfanya, utabaki kulialia tu mitandaoni.

︎ Hela aligawa kwa wananchi bila idhini ya Bunge and yet hauna chochote cha kumfanya, isipokuwa unaendelea kuteseka na chuki inayokutafuna kidogokidogo mpaka utakapokufa.

NB: Mwenzio amekufa akiwa na cheo namba moja kabisa nchini ambacho wewe hata ufanyaje utakaa ukisikie tu. Ni ushauri kwako ujikite kuitafutia familia yako mkate badala ya kuhangaika na marehemu.
 
Hahaha, Huyo Magufuli mwenyewe alikuwa na Masters and PhD fake, angeanza kujifukuza mwenyewe ingekuwa poa zaidi
Maskini Ben alithubutu kumkumbusha akaliwa kichwa hata maiti haikuonekana! Mchakato wa kumshitaki Makonda uanze mara moja>
 
Huna lolote eti unamtetea wakati we ndo una chuki nae acha unafiki,,eti hata kama wengi hawamkubali!!! Eti hata kama hana uwezo kama viongozi waliopita!! Jipange 2030 si karibu
Umemsoma vizuri Sana. Eti wengi! Ametaka kulikuza. Kumbe ni yeye
 
Na Mbowe ana watoto na família kiujumla inamhitaji yeye sio aonewe kwasababu ya mitazamo tofauti na watawala.

Huyo Samia atakachokipanda ndicho atakachovuna na atakejeliwa bila ya kuangalia sura yake.
Wachaga bhana
 
Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa Rais wa JMT kwa mujibu wa katiba, bila matayarisho. Haijalishi ni mwanamke ama nani, lakini Ccm ilipopata 84% ya kura zote kwenye uchaguzi mkuu, maana yakeni kwamba 84% zilikubaliana na Ccm na mambo yake yote akiwemo Rais Samia Hassan, kama Makamu wa Raisi na majukumu yake yote likiwemo la kura Rais wa nchi iwapo ingetokea ndivyo sivyo kwa Rais. 84% ya kura hazikuwa za Rais Hayati Magufuli peke yake bali zilikuwa pia za SSH, ilani ya Ccm na kila kitu cha Ccm kwa mujibu wa katiba.
Sasa yanaibuka malumbano mbali mbali, mara "-

Mama hakuchaguliwa, kitu kinachoonyesha namna gani watoa hoja, hawana uelewa wa mifumo inayoongoza nchi.
Kila mtu anasema anachoweza bila mipaka ili mradi anatumia uhuru wa kujieleza. Sasa, ombi langu ni hili:-

Watanzania tumsaidie Rais kutuongoza ili tusonge mbele. Kumdhoofisha kwa namna yoyote ni kudhoofisha nguvu yake ya kutuongoza na hivyo kudumaza maendeleo na mustakabari wa taifa.

Hulka ya kuwa kila mtu ni mjuzi wa mambo yote, ni dalili ya kushuka kwa thamani ama viwango vya elimu nchini. Lakini hii haiondoi kwamba katika Elimu kuna maarifa na maarifa ni nguvu hivyo, wananchi tunapashwa kuheshimu utaalam ufanye kazi badala ya porojo na kampeni za kisiasa kila mahali.

Ninaona baada ya nafasi za kisiasa, sasa watu wanaanza kupiga kampeni za wataalamu, mtoe huyu, mweke huyu bila kutolewa maelezo ya kitaalam. Hii inafanya wataalam waone hawanathamani na inaweza kuharibu viwango vyao vya utendaji kazi. Taratibu za kuchukuliana hatua pale mtaalamu anapoharibu, zifuatwe lakini si kelele za mtoe huyu, mweke huyu.

Mama ni kiongozi mkuu wa nchi lakini pia ni binadamu kama binadamu wengine. Anapoonekana kukosea, akosolewe kwa adabu na heshima. Hii itampa nafasi yeye na watu wake wa karibu kutafakari na kujipanga vyema namna ya kurekebisha kasoro, bila fedheha. Unapomfedhehesha kiongozi wa nchi, unalifedhehesha taifa na hakuna mtu mwenye akli timamu atakayeona fahari kuwa chini ya uongozi unaodharaulika na kufedheheshwa isipokuwa mtu yule asiyelitakia mema taifa, mwenye nia ya kuasisi machafuko ambayo mwisho wa siku hayamnufaishi mwananchi wa kawaida.

Ccm ndiko chimbuko kubwa la uharibifu dhidi ya taasis ya Urais. Watu wengi wanajigundisha na urais kwa kuamini kwamba kwa kuwa ccm inatawala basi kila kiongozi wa CCM ni mtawala wa wasio ccm katika ngazi yoyote aliyopo, na ni serikali na ananguvu na uhuru wa kufanya lolote. Wana ccm acheni kutuharibia nchi. Kaeni mbali na serikali, mmwache mama afanye kazi na serikali yake.

Tofautisheni Chama na Serikali kwa kuwa kama inavyoonekana, bila hiyo tofauti, migogoro yenu ya chama sasa mnaiunganisha serikalini. Tunafahamu kwamba Ccm mnajifanya mentors na mmejiglue na urais ili kufanya manipulations tu na si kwa sababu nyingine yoyote. Sasa mwacheni Rais kwa sababu Urais ni taaisis kubwa yenye mifumo mingi inayotakiwa kuimarishwa, kutumika na kusimamiwa ipasavyo ili kufanya kazi na Rais kwa maslahi ya taifa.

Kwa mutakabar wa taifa, tunaomba katikba mpya, isiyona ulali kwenye vyama vya siasa, za kisiasa bali kwa ustawi wa Taifa na vizazi vijavyo. Mfano katiba ikiweka bayana kwamba Rais, asiwe na uenyekiti kwa chama chake, bila shaka, machafuko ya kwenye vyama yatabakia huko na hayataliingiza taifa kwenye sintofaham.
 
Kwahiyo kwakua mama yako ni rais bila matayarisho unataka kila mtanzania aende naye? Dege moja litatosha wote mwende?
 
Kwahiyo kwakua mama yako ni rais bila matayarisho unataka kila mtanzania aende naye? Dege moja litatosha wote mwende?
Unataka kumwondoa kwa utaratibu gani? Kumdhoofisha ni kulidhoofishsa taifa na haina maslahi kwa yeyote. Anapopungukiwa, tumpe nguvu ili tusonge mbele. Kosa lake kubwa ni lipi kwa mjibu wa kwako?
 
Back
Top Bottom