Watanzania wenzangu, biashara ya usafiri wa anga (ndege) sio kama Uber jamani

Nilikuwa nimepanga kutokujihusisha na mijadala ya kisiasa, imebidi nijitokeze katika huu mjadala.

Mjadala huu umechukua sura ya kisiasa hasa baada ya ripoti ya CAG kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara.

Mleta mada kaliweka suala la ATCL kiuchumi zaidi ila wewe Eyce unatafuta majibu ya hoja zako kisiasa.

Tanzania katika awamu mbalimbali za Serikali zimekuwa na mikakati ya msingi ya kiuchumi. Sera ya Kilimo kwanza ilikuwa na inakusudia kujitosheleza kwa kilimo. Sera ya viwanda inakusudia kujitosheleza kwa bidhaa muhimu kwa mahitaji ya kila siku na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Ili kufanikisha hayo imelazimika kuimarisha miundo mbinu dhabiti ya usafirishaji (ardhini, majini na angani) kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wengi wetu humu JF hatujui vichocheo vya kiuchumi na hata kama tunajua, kwa sababu tunazozijua, tunajitokeza kubeza ununuzi wa ndege. Nina uhakika miaka ijayo faida ya kununua ndege zetu wenyewe leo itakuwa dhahiri.

Kwa mfano, baada ya kujitosheleza chakula na bidhaa, Sera ijayo ni ya uuzaji bidhaa nje ya nchi. Hili haliwezi kufanikiwa kwa faida bila kuwa na usafiri wa anga ulio imara. Kama utakumbuka hadi leo mazao yetu na madini husafirishwa kupitia Kenya, je, tuendelee hivyo hivyo kwa bidhaa za viwanda vyetu vinavyojengwa?
Maroli yanayotakiwa kupakia mazao kijijini Kodi ipo juu hayo magari yanayotumika kubeba watalii Kodi ipo juu unawezaje kuchochea uchumi wakati watu wako hawana kipato na hawawezeshwi kufanya hivyo...Nchi imegubikwa na upigaji wa kiwango cha juu mno mwezi January watu walijiongezea Kodi ya magari bila bunge kuhidhinisha leo Mama anataka ukaguzi wa hizo fedha ni kweli ndege zinaweza kuchochea uchumi kukua ila ukinunua kwa mkupuo hivyo hasara utaiona na sijui kama zina route za kueleweka zaidi ya kuambiwa abiria wa chato wamejaa...
 
Tunapoambiwa ATCL imepata hasara tusibeze sana. Kuna American Express na Delta Lines wanachungulia kaburi! Na Amar hapo UK British Airways imegubikwa madeni nusura izame! Tatizo lenu ni uzungu pori? Ni mashirika ya wenye mafuta kina EMIRATES, QATAR na wenzao Serikali zao zimenunua madeni. Baadhi ya matukio yaliyotikisa biashara ya usafiri wa anga duniani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita:

1. Global Economic and financial crisis (mtikisiko wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia).
2. Marubani, wahudumu na watumishi viwanjani kugoma Mara kwa mara nchini Marekani, UK, France na Italy.
3. Kodi mpya (carbon tax) kugharamia uchafuzi wa anga.
4. Covid 19 restrictions on travel (masharti ya covid 19)
5. Gharama za utengenezaji ndege kuongezeka mno kutokana na ushindani Kati ya Airbus na Boeing kufuatia mahitaji ya usalama wa abiria.
6. Nchi kunyimana route (protectionism policies).
7. Uendeshwaji mbaya wa airline
8. Kubadilika kwa sura ya utalii. Mfano watalii wengi kuanza kujikita kutembelea nchi au eneo lao, kushuka ari ya kuona wanyama au milima n.k.

Hizi ndio sababu ya mashirika mengi duniani kuendeshwa kwa hasara. Sio lazima éti hasara pawepo na wizi

Licha ya mashirika kufanya vibaya hakuna nchi imefunga shirika lake. KLM ilitaka ijiuze kwa AIR FRANCE wananchi wakaandamana! Serikali ikalazimika kubeba madeni.

Alitalia ya Italy ilitangazwa imefilisika Papa akamwandikia barua Prime Minister kwamba Vatican hairidhii uamuzi! Serikali ikabeba Madeni. Mpaka leo Alitalia ipoipo tu. Ukipatiwa ticket ya Alitalia jiandae for cancellation wakati wowote. Mara nyingi watakuhalishia Easy Jet au Ryan Air.

Sasa kuna mijitu inadhani biashara ya ndege sawa na biashara ya kuuza mashokishoki Darajani!
" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fstatic.xx.fbcdn.net%2Fimages%2Femoji.php%2Fv9%2Ft7f%2F1%2F16%2F1f60a.png&hash=efe739e1e11105d2cb04b5162bb1658d" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> <img src=" title="" width="" height="" />
ATCL yatoa gawio kwa Serekali.
ATCL yapata faida ya Bilioni 28

Hizi kauli ndio tunahoji zilikuwa na maana gani???
 
Back
Top Bottom