Watanzania wenzangu amkeni; adui yetu mkubwa ni Bunge letu na Uongozi wake

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
4,199
Ndugu zangu naomba tujue mahala pa kuanzia kuelekeza malalamiko yetu. Kwa muda mrefu sasa wale tunaowatuma bungeni kutuwakilisha wameshindwa kabisa kutekeleza wajibu wao badala yake ndio wamekuwa wanatuchongea kwa mamlaka za nchi kuwa tukandamizwe kwa kukatwa makodi kibao.

Mfano mdogo ni huyu Zungu ambaye amekomaa na hoja yake ya kukatwa kodi ya uzalendo hadi ameitikiwa. Lakini hajawahi simama bungeni kuomba mishahara ipande au bei za mafuta zishushwe.

Wabunge wengine vivyo hivyo wakiongozwa na spika. Kazi yao ni kutetea serikali badala ya wananchi, tuamke jamani. Tuna pakuanzia. Sasa suala la makato kwenye miamala wamekinukisha halafu sasa akina shigongo wanaanza kujikosha eti anaongea na Rais tozo zishushwe. Arrrrrhhh! Nasikia hasira nasikia hasiraaaaaa.

Hatupaswi kabisa kuwaacha watulie, tuungane kuwang'ong'a mpaka wajitambue au angalau wajue kuwa tunajua kuwa hawatimizi wajibu wao. They are not in touch with the representees.
 
Zungu katika hali ya uzalendo angeomba bunge lifute sheria ya wabunge kutolipa kodi ili uzalendo usiwe kwa raia tu uwe na kwa wabunge pia, mishara mikubwa na miposho kedekede ingetunisha sana hazina lkn huu uzalendo wa kutungia wengine tu lbd wenzetu wanajihesabu hawaishi TZ ndiyo maana wanadai walipwe dolali.
 
Back
Top Bottom