Uchaguzi 2020 Watanzania wengi wa sasa hawatabiriki kama "Wajumbe"

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
275
801
Tarehe 28 hiyooo imefika,

Misimamo ya watanzania haitabiriki,

Hii inatokana na kukosa uhuru wa kuongea,

Watanzania wakikutana kwenye vijiwe wanamsifia Magufuli,

Ukimdadisi mmoja mmoja kwa wakati tofauti msimamo unapingana na wakiwa wengi,
.
Wanahofu ya kupata majanga ya kushtakiwa, kufungwa, au kutekwa,

Je, wampigia nani kwenye chumba cha kupigia kura?,

Nawakumbuka Wajumbe,

"Tupo pamoja, unakubalika, wewe ndiye mbunge",

Na maneno mengine mengi,

Mwisho wake mtia nia kapigwa spana,

Hajapigiwa kura hata na ndugu yake,

Kuna vilio vinasikika Lumumba,
.
Polepole akimlilia mshindwaji,

Bashiru akigalagala vumbini kwa uchungu,

Hawataki kufarijiwa kwa kuwa wameangukia pua,

Wajumbe wanewafundisha tabia nzuri watanzania,

Ni spana kwenda mbele,

Watu hawa hunisifia mdomoni tu,

Lakini moyoni wapo kwa Lissu,

Hunidhihaki nijaribiwapo,

Huniwekea vikao vya masimango,

Nao watasema umeanguka ewe Babeli umeanguka,

Ewe uliyewazamisha wafalme,

Ewe shujaa mwenye nguvu,

Umeanguka kama unyasi wa asubuhi,

Umeanguka ewe nyota ya alfajiri,

Ndugu zako watakudhihaki,

Yeye aliyewachukua mateka ndugu zake aneingia kwenye mtego wa mwindaji,

Watawala wa dunia watastaajabu,

Ni huyu ndiye aliyejiinua juu ya kiti cha enzi,

Ona sasa umeshuka mpaka mavumbini.

Wajumbe pigeni spana, watanganyika pigeni spana, wazanzibari pigeni spana.
 
Tarehe 28/10 watanzania watapigakura ambapo dunia itaona na kusikia.
Hapo asijitokeze mtu akataka kuwalazimisha watanzania watende kama anavyotaka
 
Hakuna lisilotabirika, Lissu anaungwa mkono na asilimia kubwa ya wapigakura nchini, hilo halina mjadala.
 
Lisu is a victor
 
Tarehe 28/10 watanzania watapigakura ambapo dunia itaona na kusikia.
Hapo asijitokeze mtu akataka kuwalazimisha watanzania watende kama anavyotaka
Simu zitazimwa tarehe 27/10 mpaka 12/11.
Tanesco nao watakuwa wamezima mitambo.
 
Shetani anajaribu kushindana na Mungu.

Hakuna Jiwe litakalosalia Juu ya Jiwe ambalo halitabomolewa.

Babeli imeanguka.

Danieli 5
25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.

26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Yaani wamedi na waajemi ni ACT ZANZIBAR NA CHADEMA TANZANIA BARA.
 
Safari hii Mungu hadhihakiwi.
Shetani anadondoka hadharani kweupee.
Kura zote kwa Lissu
 
Hakika Mungu ni mwema wakati wote na hakuna kisicho na mwisho,ccm wajue hilo lipo wazi mwaka huu.
 
Mgombea ana tabia za MANGE KIMANGI MANGE KIMANGE.

Yaani tayari ameshaweka TIKETI kiunoni ili akafanye uanaharakati NEW YORK BEIBIIIIIII.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom