Uchaguzi 2020 Watanzania wengi sasa wanamiliki smartphone ili kupashana habari za uchaguzi hasa zinazohusu wapinzani

Kwa wake wanaodhani kuwa kudhibiti vyombo vya habari kuripoti habari za wapinzani kutawasaidia, wajue tu wanajidanganya kwani hivi sasa watanzania wengi wanamiliki smartphone hasa maeneo ya mijini, hivyo watazitumia kupashana habari za uchaguzi zikiwemo habari za wapinzani.

Lissu kasema wametishwa kuripoti habari zake na kwamba wanamuogopa mtu mmoja ila akaongeza kuwa ,watu sasa watutimia WhatsApp kupashana habari za uchaguzi.

Ukweli ni kwamba,Lissu kataja WhatsApp kama mfano tu, ila watu watatumia Facebook,Instagram, Twitter na mitandao mingine kama huu wa JamiiForums kusambaza na kupashana habari za nini kitakachokuwa kinajiri kwenye mkutano ya kampeni ya wapinzani hata kama watu wa TV na magazeti hawataripoti.

Uzuri wa haya mambo ni kuwa,watu wakipuuza hizi media,hata like kitakachokuwa kinaripotiwa na hizi media pia nacho kitapuuzwa, hivyo wataopata hasara ni hao watakaokuwa wanategeme hizi media ziwabebe.

Wao waendelee tu kujidanganya wakati watu Siku hizi wameanza kutegemea social media zaidi kama chanzo cha kupata habari huku mainstream media zikibaki kutumika kwakuwa tu ziko majumbani mwetu.

Siku hizi watu wanasikiliza habari kwenye tv huku teyari wana taarifa za matukio karibu yote ya siku husika tena taarifa hizo wakizipata pasipo kuchujwa ili kumsitiri mtu au kuficha baadhi ya mambo.

Mfano mzuri ni ujio wa Lissu ambao ulitangazwa zaidi kupitia social media lakini karibu kila mtu alikuwa na taarifa na alipokelewa na watu wengi utadhani tukio husika liliitangazwa na vyombo vikubwa vya habari mwezi mmoja kabla.

Labda yule Malaika wa kuzima mitandao ashuke ndio itakuwa ponepone yao ingawa nae anaonekana kukwama huko mawinguni.

Imekula kwao mwaka huu.
Smartphone kuanzia laki moja unapata vijana wote wanazo. So media outlet kwa sasa is subsituted from magazine to social media outlet
 
Hakuna anayesikiliza radio tena wala kuangalia TV za bongo.Tumerudi nyuma mika 50 kidemokeasia.Hatuna tena uwezo wa kujenga hoja.Debate za upande mmoja tu bila kualika upande wa pili ni mbaya.
Binafsi nina miaka 5 sijawahi kuangalia tv yoyote hapa nchini.
 
Serikali ya CCM HAIJAFANYA KITU. Sasa hao wananchi hizo smartphones, WhatsApp na Twitter wanazitoa wapi hapa Tanzania?
Duh! Hadi huruma, hawa ndio great thinkers ambao Jamiiforums inajivunia kuwa nao?
Maxence Mello kama ndio hivi ndoto zako zimebuma, GT's wamechanganyika na milupo!
 
Lumumba mlisema upinzani umekufa sasa leo mnatapata tuwaeleweje au tatizo ni uwezo mdogo mlionao ndio unawagharimu?

Hiyo miradi sio issue ya kufanya watanzania wajinga tutaona miradi hiyo ihalalishe utekaji, utesaji, mauaji, kunyima watu haki zao, kutesa watumishi wa umma, kusimanga wananchi majukwaani mfano wahanga wa tetemo Kule Bukoba, n.k
Kusema chama cha siasa kufa si kama unavyodhania kufa kwa chama ni kutokuwa active ktk majukwaa ya kisiasa hasa shuguli zote zinazofanya chama kuitwa cha siasa lakini ukisema chadema haijafa kwa kuangalia wafwasi au watu wanaojaa kwenye misafara yenu utakuwa unachekesha coz hata CUF au TLP leo bado wanawafwasi kibao je CUF hii ndo CUF ya mwaka 2000? Jibu unalo mwenyewe


Ukizungumzia watu kujaa au kuwafata kwenye misafara yenu ndo useme sasa Chadema haijafa kisiasa nitakushangaa coz hata Diamond akitembea kkoo watu wanaomfata ni wengi sana tena wanaweza kusimamisha shuguli kabisa na kunaitajika police tena wengi sasa leo ukisema Diamond tena ni mtu mmoja si chama cha siasa akigombea hata ubunge Ilala atapata eti kigezo cha watu wengi kumfata au kumjua?

Leo Diamond anawafwasi 10.4 IG ninaimani wengi wapo Tanzania na 70% wanaumri wa kupiga kura so leo Diamond akigombea uraisi unaweza kusema atashinda? Jibu ni hapana tena inawezekana hata kula 1milion hatofikisha kufa kisiasa ni tofauti sana unavyoweza kidhani .
 
Watu wako kwenye Social Media hivyo vyombo vya habari ni wachache sana ambao bado wana shauku navyo hadi magazeti yanaelekea kufirisika.
 
Back
Top Bottom