Watanzania wengi ni wamebobea uchumi lala (sleeping economics)

Naunga mkono hoja ila natoa angalizo kwa wachangiaji kwamba tusimshambulie mleta mada ebu tujaribu kuweka jazba pembeni halafu hiyo mada yake tuiasili ktk mazingira yetu ya kitanzania.
#.Je fursa za kuwekeza Tanzania tumezitumia vizuri?
Mimi nimeamua kuwekeza kwenye kilimo cha kuku wa kienyeji pamoja na kuandaa juice ya matunda(fruit pulp) kwa ajili ya kuiuza viwandani UAE.
#.Kwa nini viongozi wetu mbona wanawapapatikia wageni?
Mzawa hawezi mudu 10%,nikikupa 10% utanimalizia mtaji wangu.
#.Je,elimu tunayoipata ni jibu la umaskini wetu au inatakiwa iwe chaji ktk bongo zetu ili tuzidi kupambanua mambo kwa kina?
Mmh hapa ni tatizo maana walimu wangu wa Chuo kikuu wapo tu kutimiza siku na kujidai wao ndio wanashikilia kesho yako.Nyoko mbona wananifelisha kila kukicha kisa ninawapa changamoto kuanzia za kijamii,kisiasa na kiuchumi.
#.Je unaweza tengeneza ajira ktk soko la ajira Tanzania?
Nina baiskeli 100 ambazo wanaendesha vijana waliomaliza sekondari huku wakingokea kuendelea na masomo baadaye,kazi yao ni kusambaza bidhaa za bakery yangu(chapati,vitumbua,karanga,sambusa,popcorn nk) kwa wateja wangu wapatao 2500 kila siku hapa mjini .Ujira ni Tshs 5000/= per day per each bicyle kid.
Labda haya machache yatatusaidia sote wapenda maendeleo.
 
Wakuu tunamshambulia huyo bwana Richest lakini ana kapoint kazuri anakosimamia, hebu badala ya kumshambulia tufuatilie maoni yake kwa makini ingawa kishahili chake ndio hivyo tena. ...............................



Naunga mkono hoja ila natoa angalizo kwa wachangiaji kwamba tusimshambulie mleta mada ebu tujaribu kuweka jazba pembeni halafu hiyo mada yake tuiasili ktk mazingira yetu ya kitanzania.
.

Ameshambuliwa wapi au ameshindwa kujibu hoja?
 
mkuu kitu kinachotufanya tujenge kwanza ni maisha yasiyo na tumaini(confidence)ni kwamba hata waziri mwenyewe anatamani awe na kwake kabla uwaziri haujaisha,hayo mambo tumerithishwa na serikali mbovu ya ccm,sio kosa la watanzania
mkuu nimetembea sana nchi nyingi hapa duniani,nathubutu kukueleza watanzania ni watu wenye akili sana na kamwe huwezi kuwalinganisha na mataifa mengine hasa ya kiafrica

Hivi hiyo serikali tunayoilaumu inatokana na nani? au tumekodi management toka ulaya? ............siyo sisi wenyewe watanzania?


Duuh, watanzania kila tatizo wao ni serikali tu,
 
Hivi hiyo serikali tunayoilaumu inatokana na nani? au tumekodi management toka ulaya? ............siyo sisi wenyewe watanzania?


Duuh, watanzania kila tatizo wao ni serikali tu,


Wacha ku-generalize soma hapo nyuma hoja ya serikali kuwabana bankers etc. UK, USA na nchi tajiri zote wanafanya ndio sababu wanaendelea sisi tumekaliwa na hawa m a g a b a c h o l i kujifanya wao ndio vinara wa kuto rushwa.
 
Hapa marekani bepari mkubwa duniani mwenye kumiliki maduka ya reja reja : Watson Wal-malt. Yeye alianzia kuwa mtoto wa mkulima na alianza na kulima na kufungua duka dogo la leja leja mpaka akwa Tajiri wa dunia wa maduka ya wal-mart. alisoma mpaka alipata degree ya kwanza ya uchumi ila yeye aliitumia kujijengea biashara. Ndiye aliyevumbua kuweka bidhaa katika mashelves na watu wanachukua kwa kujaza katika macurts na kucash out kwa cashier. Jana CEO wake kagundua ndia ya kulipa vitu mia moja katika cuts bila kuonesha kwa cashier na unalipa moja kwa moja. au unanunua bidhaa katika duka lake kupitia On line , halafu wahudumu dunkani mwake wnakujazia katika box. Unalpa kwa credit cards na halafu wanakuletea nyumbani. Hii yote ni elimu na kuwatumia vizuri wasomi.
 
Mswahili akikukaribisha mgeni kama umetoka nje ya nchi atakuambia tuende ukaone kwangu (Ukaone pango anakolala huyo lofa asiyekuwa na kitega uchumi chochote).

Nadhani kuna umuhimu vijana wetu kufunzwa uwekezaji kabla ya kuanza kazi.Wafundishwe kuwa waanze kuwa wawekezaji badala ya kukimbilia kununua magari ya kifahari na kujenga nyumba za kulala.
 
Wajinga sana hununua takataka, wajinga kidogo hununua bidhaa mizigo(liabilities), majanja na wenye akili hununua assets aka mali zinazozalisha. Jitafakari upo kwenye kundi gani. Watanzania wengi tupo kwenye kundi la kwanza na la pili
 
Ni kweli kabisa

a. Nyumba za waswahili zilizo mikoheni, mbezi Beach na Kwingineko haziendani na viwanda walivyonavyo waswahili..assuming kiwanda kidogo cha M.700. (hesabu nyumba za zaidi ya hiyo pesa?

b. Kuna tatizo la over emphasize on building houses kuliko kufanya investments
 
Ni kweli kabisa
Kuna tatizo la over emphasize on building houses kuliko kufanya investments
Yaani hii overemphasis ya kupenda kujenga nyumba za kulala kuliko vitega uchumi sijui watanzania tumeitoa wapi? Wataalamu wa historia na falsafa watusaidie na ikiwezekana watoe ufumbuzi nini kifanyike hali ibadilike.Maana vinginevyo tukiendelea na huu mfumo ambapo hata watoto wadogo wanaoanza kazi wanaota kwanza wapate nyumba na gari ya kutembelea chap chap kabla ya investments nadhani kama nchi tutakwama mbeleni.Hii lifestyle sio nzuri.

Mtu unasikia eti nilichukua milioni kumi za mboga nini hicho? Angesema alichukua akawekeza pengine miguno ingekuwa midogo

Nikiri mtoa mada kanifumbua macho asante jamii forums.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom