Watanzania wengi ni wamebobea uchumi lala (sleeping economics) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wengi ni wamebobea uchumi lala (sleeping economics)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RICHEST, Jul 26, 2011.

 1. RICHEST

  RICHEST Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanapenda sana kulala.Ukigombana naye tu atakuambia usinibabaishe nina kwangu (kwa kulala).
  Kuna wimbo wa zamani niliimba shule unasema "Wazee wa zamani walilala mapangoni katika nchi Tanzania" Walipenda sana kulala.Baadaye inasemekana wazee walikuwa wanalalia pesa.

  Leo hii miaka mingi baadaye kuna watanzania wako tayari kujenga majumba ya milioni mia tano mbezi beach au mikocheni za kulala lakini hawawezi kununua kiwanda au godown la milioni mia mbili pugu road mtaa wa viwanda.Kwa ufupi badala ya kulalia PESA nafikiri wanaogopa majambazi watawaua wanaamua kujengea pango la kisasa la kulala.

  Mswahili akikukaribisha mgeni kama umetoka nje ya nchi atakuambia tuende ukaone kwangu (Ukaone pango anakolala huyo lofa asiyekuwa na kitega uchumi chochote).

  Kazi kucheka wahindi oh! hawana kwao.Mhindi kitu cha kwanza apate kitega uchumi kwanza.Hivyo wako tayari kupanga hadi kieleweke.Waswahili akipata pesa haanzii kitega uchumi anaanzia kajumba na tumarumaru mtumba twa china atengeneze pa kulala kwanza atambie walalaji wenzie kuwa ana pa kulala bora penye usingizi mnono kuliko mwenzie.(Wanashindana kuonyeshana pa kulala badala ya vitega uchumi) Akienda mbele sana atamwonyesha kagari kenye A/C na viti vizuri vya kukunjua kujilaza ukichoka uulimbe usingizi ndani ya kagari.Hapo mswahili kafika.

  Kama pesa za ujenzi wa Majumba ya Mikocheni,Mbezi beach na Masaki zingeelekezwa kwenye uwekezaji hata wazungu wangekimbia nchi hii kuogopa wawekezaji wazawa wenye uwezo wa kutisha.Raisi Kikwete asingehangaika kwenda kutafuta wawekezaji nje angekuwa anazunguka humu humu nchini kuongea na wawekezaji wazawa.

  Kwa ufupi Tanzania haiendelei sababu wananchi wengi wamebobea katika uchumi lala au kwa kimombo Sleeping Economics.Ni vizuri waswahili wakaanza kujifunza kwa wahindi.Mhindi vitega uchumi vikikaa sawa ndipo anahama kupanga na siku akihama haendi kujenga masaki wala mbezi beach ujue anaenda zake kununua jumba london au canada huko ndiko atafia akila kuku kwa mrija maisha yake yote.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wabunge wa ccm kwa kulala bungeni wanaaminia
   
 3. S

  Shamu JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good point. Sema kitu kinachoiangusha TZ ni elimu. TZ ina wasomi wengi lakini hawajui njia innovations. Idea kubwa ya kila MTZ ni kwenda shule na kuajiriwa, especially serikalini. Wenzetu wakipata BA, MBA, au PhD wanaanza kujiajiri wenyewe ktk biashara ndogondogo mpaka zinakuwa kubwa. Sasa hivi WTZ wasomi wanailaumu serikali kwamba haiwasaidii, huu ni ujinga.

  Mtu ana elimu bado anasubiri serikali? tuna ardhi kubwa, lakini bado anataka kazi za ofisini, huu ni ujinga wa kielimu. Matajiri wakubwa duniani ktk nchi zilizoendelea ni wakulima. TZ tuna ardhi yenye rutba, lakini watu bado wanataka kuajiriwa na serikali. Tatizo ni kuelimika. WTZ wanayo elimu, lakini bado kuelimika.
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu kitu kinachotufanya tujenge kwanza ni maisha yasiyo na tumaini(confidence)ni kwamba hata waziri mwenyewe anatamani awe na kwake kabla uwaziri haujaisha,hayo mambo tumerithishwa na serikali mbovu ya ccm,sio kosa la watanzania
  mkuu nimetembea sana nchi nyingi hapa duniani,nathubutu kukueleza watanzania ni watu wenye akili sana na kamwe huwezi kuwalinganisha na mataifa mengine hasa ya kiafrica
   
 5. A

  Ame JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya tu hizo akili hawazileti nyumbani kwao wanazipeleka kwa wengine; kama zingeletwa kwao basi ndugu zao wangekuwa better off for that case kuliko hizo nchi nyingi za Africa! Watanzania iko maneno mengi sana kuliko matendo; kiswahili kimetufanya wote tukawa waswahili nikiwa kiongozi wa nchi nitakipiga marufuku nakufanya luga yangu ya kihaya luga ya taifa! Bora nchi igeuke ya ma deal kama Nigeria kuliko kuwa na maneno mengi ya umbea kama ilivyo lol!
   
 6. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu wewe ni muhindi?
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nafikiri umepotoka tu, kama wahindi unaowasifia ndio level yako ya kufikiria inabidi urudi darasani tena. Unapokuwa na nyumba kwa wenzetu wa nchi za magharibi hicho ni kitega uchumi chako, unaweza kukitumia kununua viwanda nk. Tatizo kubwa ambalo linawafanya Watanzania wasiendelee ni hawa wahindi ambao unasema ni werevu ie wasiolipa kodi, majambazi nk. Je, Tanzania tunahitaji society kama hiyo? No thank you. Watanzania wengi wameamua kujenga vibanda vyao baada ya shirika la NHC kushindwa kukidhi haja ya nyumba kwa wengi, na wasingependelea kulala kwenye mapango.

  Ukweli unabaki bila kufichika hawa ndio wanaoididimiza Tanzania kwa kuwarubuni viongozi wengi wa Tanzania, watoa rushwa wakubwa kabisa Tanzania ni hawa wahindi pitia kashfa ya radar, kashfa ya BOT nk. Watanzania wengi wenye nyadhifa wameghiribiwa na hawa g a b a c h o l i hata ukienda madukani mwao wameweka picha walizopiga na hawa viongozi uchwara.

  Sio sahihi kabisa kusema ati wana nyumba UK na Canada etc. Hao ni wachache sana angalia fact zako kabla hujaja kutema upupu hapa jamvini. Hao wahindi wenye pesa kwa nini wasijenge nyumba zao na kuendelea kukalia nyumba za NHC.

  Serikali inachotakiwa kufanya ni kuwabana hasa financial institutions kuwakopesha Watanzania wenye assets wanapotaka kufungua viwanda nk. (kama inavyotokea UK, Canada, USA, Germany, Sweden, Japan etc.) kwani wengi wanakatishwa tamaaa na hii system ambayo inawapendelea wageni .

  Wahindi wengi ambao wamezaliwa Tanzania hawana uzalendo, wao ni kujiona bora zaidi kuliko wazawa na iko siku tena yaja watakiona cha mtema kuni. Huko Canada na UK hawakubaliki ndio sababu wanang'ang'ania kuchuma mali bure Tanzania kwa njia zao chafu. I can assure you they will pay taxes in those countries without fail let alone work for their money.
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu umeongea point,wahindi sio wenzetu hata kidogo nashangaa wanawakabidhi ubunge,mungu apishie mbali hawa tunawasagia meno lakini hawajui
   
 9. RICHEST

  RICHEST Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani hizo nyumba za NHC Wanazokaa nani alijenga? kama hujui ni wahindi walijenga serikali ikataifisha na sasa wamerudi kukaa tatitzo liko wapi?
  Ungeuliza waswahili wanaokaa NHC ndio wakajenge zao.Wahindi hayo maghorofa ya NHC kariakoo,upanga, katikati ya mji kalitafute lilojengwa na Mswahili ni lipi? walijenga wao vikiwa vitega uchumi vyao serikali ikawapokonya ikabidi waanze upya.
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Walijenga kwa pesa za nani? Rejea kwa nini zilitaifishwa. Usirukeruke tu kama chura.
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wali-take chance ya baba zetu kutokujua sana wakati ule,wakaiba hela zetu wakajenga canada
  ni watu ambao hatuwezi kuwaita wenzetu kwa sababu huwezi kumwona muhindi anaishi manzese
  nafikiri wakati utafika tutajua cha kufanya na hii jamii
   
 12. RICHEST

  RICHEST Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walijenga kwa pesa zao halali.Kama waliiba serikali ilipotaifisha mbona iliamua kuwalipa fidia ya kuzichukua? Au wewe kutaifisha unafikiri serikali ilichukua bure na kuwatimua?
  Au wewe una ushahidi kuwa kuna wamiliki wa hizo nyumba waliwahi pelekwa mahakamani kwa wizi wa pesa walizojengea hizo nyumba?

  You are arguments naona ziko below the sea level.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,461
  Trophy Points: 280
  unajua kuwa Mengi alibaniwa kuwekeza kwenye hoteli moja kubwa nchini?? kwa nini?
   
 14. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  hata mimi nimeona kwa watz mtu akiwa na kijumba na kigari basi anajiona kafika mwisho wa reli hafikirii akiretire itakuwaje no wonder tunakufa mapema after retirement.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nimekwambia Wacha kuruka ruka kama chura unaweza kuona jinsi unavyojichanganya. Kama walifidiwa kwa nini tena waendelee kukaa baada ya kurudi? Kama unataka tuamini maneno yako? Unasema walianza upya, wapi hapo walipojenga upya kama sio wizi wa mchana kweupe? Hoja zako hazina mshiko ni porojo za mitaani.
   
 16. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu sio wote,nafikiri unawaona wale wa class yako
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,461
  Trophy Points: 280
  stori za kwenye kahawa
   
 18. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Unafahamu hawa wezi siku zao zinahesabika. Si umeona RA kakimbia mwenyewe tutawashughulikia tu, we have the time and power to deliver.
   
 19. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wakuu tunamshambulia huyo bwana Richest lakini ana kapoint kazuri anakosimamia, hebu badala ya kumshambulia tufuatilie maoni yake kwa makini ingawa kishahili chake ndio hivyo tena. Binafsi nakubaliana naye kuwa kama kasi ya kuziweka pesa katika mambo yasiyozalisha ingeenda sambasamba na kuwekeza kwenye uzalishaji kungekuwa na mabadiliko. Ila swali hawa wote wanaofanya maajabu haya huko mbezi beach na wapi wamezipate hizi pesa, hapo ndipo unapoanza huo mtihani. Mara nyingi pesa inayoingia bila ya kuihangaikia ni aghalabu sana kuingiza kwenye uzalishaji kwa nini mnaweza kunisaidia.
  Kwa mfano vile vijisenti jamaa angekuja kufungulia navyo kiwanda au hata mashamba, angesaidia kwa kiasi gani nchi yake?. Je wako wangapi wa jinsi hiyo?, ni majuzi tu tumesikia mgao wa bahasha unafikiri ni kiasi gani kingekwenda kwenye kuwekeza baada ya hapo?. Sanasana wangejenga majumba na kununua magari, bila ya kusahau kufunga bar. Kwa sababu hawana uchungu nazo, fikiria wewe ungepata kiasi hicho kinachozungumzwa ingekuwa hivyo, si ajabu breki ya kwanza kununua hiace kwa ajili ya daladala. Hivyo jamaa anasema kweli, tuiangalie kwa utulivu mada yake.
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja kwanza nina aleji na avatar yako kama unaweza kuibali tafadhali sana niombi tu!

  Pili ebu muulize Kikwete maana alisomea Uchumi chuo kikuu cha Dar es Salaam labda alifundishwa hayo unayojaribu kusema hapa ila yeye atakuwa anajuwa zaidi yetu, jibu atakalo kupa tuletee hapa ili tuendelee na mjadala sawia.
   
Loading...