Watanzania wengi hutegea kazi Ijumaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wengi hutegea kazi Ijumaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Huduma, Oct 30, 2009.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utafiti usio rasmi unaonesha kuwa Watanzania wengi huwa hawaendi kazini siku za Ijumaa isipokuwa kwa wale walioajiriwa katika sekta binafsi. Wale wanaokwenda kazini husemekana huenda kujionesha tu.

  Wakati huo huo kilio cha Waislamu cha kutaka siku ya Ijumaa iwe ya mapumziko kimewafikia viziwi na vipofu na hakuna yeyote anayeona umuhimu wake. Hata hivyo, Waislamu sasa wameanza tabia ya kususa vikao vyote vinavyofanyika siku ya Ijumaa wakisema huku ni kuidharau siku hiyo adhimu kwa wanaimani hao.

  Wao wanaamini kwamba Ijumaa ingelikuwa siku ya mapumziko kila baada ya wiki moja wakipokezana na siku ya Jumapili. Hii ina maana wiki hii Ijumaa ikiwa mapumziko basi wiki Ijayo ni Jumapili ndiyo itakyokuwa mapumziko.
  Naona hili mlizungumze wanajamii ili tuweze kuwa watenda haki kwa dini zote mbili kubwa nchini.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Sasa wewe HUDUMA, hiyo Huduma unayoanzisha iweke vizuri, maana hapa kuna hoja mbili, sa sijui unataka ipi ijadiliwe.

  -Hoja ya watu kutegea Ijumaa na
  -kUTAKA iJUMAA IWE SIKU ya mapumziko...
  Ungerahisisha mambo kwa kuposti threads mbili tofauti!

  Lakini pia utafiti huo usio rasmi uliufanyia wapi?
  Mi naona mambo hayo yakianza itakuwa ni fujo sana, na tutarudi enzi za Mwinyi za kuhamisha sikukuu!
  Mimi katika taasisi ninayofanyia kazi Waislamu wanaruhusiwa kwenda Msikitini Ijumaa, lakini kama ni ishu ya kupumzika, wanapumzika Jumapili pamoja na Wakristo!
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kweli bongo tambalale,yaani pamoja na hali ngumu tuliyo nayo bado kuna watu wanataka kupumzika/kutegea. Wenzetu huko tunakoiga kila kitu muda ni mali kwelikweli.

  Vipi kama na sisi tukiiga kufanya kazi non stop kama wenzetu itakuwaje. Nina hakika Mungu hapendi wavivu/wategaji. Sijui kama kuna kifungu kinachotaja adhabu kwa watu wanaofanya kazi bila kupumzika ktk vitabu vya dini.
   
 4. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Leta uthibitisho kuwa Waislamu wa Tanzania wanadai mapumziko ya siku ya Ijumaa; sio unatuletea habari za juu juu.

  Ninachofahamu Waislamu wengi wanadai muda wa kwenda kuswali unapowadia wapewe fursa ya kwenda kutekeleza hiyo ibada muhimu kwa mujibu wa Imani yetu.

  Kuna katabia kapo ofisi nyingi sana hapa nchini; vikao vingi huwa vinapangwa siku ya Ijumaa tena ktk zero hour za muda wa swala ya Ijumaa, au mitihani inapangwa zile saa ambazo watu wanahitaji kwenda kutekeleza hiyo ibada muhimu.

  Hayo ndio kwa uchache nayafahamu yanayopigiwa sn kelele yaangaliwe na yarekebishwe.

  Hebu malizia na maneno haya yafuatayo hapa chini:-

  [​IMG]

  10. Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa. ***

  (Qur'an 62:10)
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  maneno sawia kabisa.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Acha ujinga wewe..waislamu hawana haja kutaka ijumaa iwe mapumziko...hiyo ni wewe na uchochezi wako..kwa utafiti uchwara..lakubali kwamba time ya kwenda kusali ijumaa between 12.30-2.00pm watu wanaomba waruhusiwe kwenda kufanya ibada..kama ofisi (bosi analeta UDINI wake) huyo ndio wakumshughulikia.. unafikiri waislamu wanapenda kupendelewa kama wakristo shame.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wewe na huyo huduma si mhamie iran??
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Utafiti usio rasmi huleta takwimu zisizo rasmi, ambazo husababisha malumbano yaliyo rasmi lakini hayana faida.
   
 9. October

  October JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu asante kwa quotation yako, imesaidia ku clarify hii issue once and for all.

  kuhusu swala la kutega kazi siku za ijumaa, nafikiri taasisi za umma zinaongoza kwa tatizo hili sugu la utegaji wa kazi, tatizo hili haliko tu kwa wafanyakazi wa chini bali hata watendaji wakuu wa serikali wana kasumba hii. nadani mikataba mibovu na hasara nyingi zinazotokea serikalini ni ushahidi tosha kabisa kuwa hawa jamaa hawajali chochote na hawana uchungu wowote na rasilimali za taifa.
  Tatizo la utegaji hufanyika siku zote za wiki, labda tu kwa vile weekend spirit huanza mapema ndo maana hali hii inaonekana zaidi ijumaa kuliko siku nyingine za wiki.

  mwishi ingekua vyema kama ungetuambia utafiti huo ulifanyika lini na nani aliufanya.
   
 10. W

  Wasegesege Senior Member

  #10
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa Proff. Dr. Mankiw ambaye amebobea katika masuala ya Uchumi anasema katika kanuni ya 8 kati ya Kanuni 10 za Uchumi kwamba. Nanukuu:

  A COUNTRY'S STANDARD OF LIVING AND ITS ABILITY TO PRODUCE GOODS AND SERVICES
  Almost all variation in living standard is attributed to differences in country PRODUCTIVITY.

  PRODUCTIVITY refers to the amount of goods and services produced from each hours of a worker's time. In Nations where workers can produce a large quality of goods and Services per unit of time, most people enjoy a high standard of living, in Nations where works are less productive, most people must endure a more meagre existence. Similarly, the growth rate of a nation's productivity determines the growth rate of its average income.

  The relationship between productivity and living standard has profound implications for public policy. When thinking about how any policy will affect living standard, the key question is how it will affect our ability to produce goods and Services.

  Mwisho wa Kunukuu.

  Sasa suala la swala ya Ijumaa kwamba, Waislam wanakwenda au wanataka iwe mapumziko lisiingie hapa kwenye Mjadala.

  Haina haja ya kutafuta Mtafiti wa kujua kama Watanzania wanafanya kazi siku tano zote za wiki (J3, J4, J5, Alh, Ij). Kwa kifupi suala siyo kufika kazini suala ni muda gani au masaa mangapi Watanzania tunatumia kuzalisha mali (kwa maana ya kuwepo kazini na kufanya kazi).

  Utakuta Mtu yupo kazini lakini mara kaja Shangazi yake ataongea nae saa 2, mara kaja mwenyekiti wa Kamati ya harusi ya Jirani yake wataenda nae kukusanya michango. anaporudi ni saa 7 amechoka anashika gazeti la Ijumaa anasoma jinsi wasanii wetu wanavyotongozana. Saa 9 na nusu inafika anakwenda Nyumba.

  Unapotaka kujua Watanzania wanakwenda kazini unatakiwa ujuwe hata wale wanaokwenda kazini je muda wa kuanzia saa 1:30 hadi 9:30 wanautumia inavyotakiwa? au ndo porojo.

  Suala la kuwahi Ofisini, nenda kwenye Ofisi za Wakuu wa Mikoa kaone wanafika kazini saa ngapi, nenda kwenye Mawizara kaone Makatibu Wakuu wa Wakurugenzi au Makamishani wanafika saa ngapi kazini, nenda kwenye Ofisi za Halmashauri kaoni Wakurugenzi na Watendaji wengine wanafika saa ngapi kazini. usiuangalie Mji wa DSM nenda hata kwenye Wilaya kama Pangapi ambapo ukiamka saa moja kamili unaweza kufika kazini saa 1:30 lakini kaone watumishi wanafika kazini saa ngapi.

  Na je wakifika wanaweza kukuonyesha jana walifanya nini? leo watafanya nini? na kesho wamepanga kufanya nini? ni Maafisa Mafaili kama hayapo wanacheza karata na kuangalia PICHA ZA NGONO kwenye KOMPYUTA matokeo yake wakitoka wanapitia sehemu sehemu maana mwili umechemka.
  kuna haja ya kuanzisha "Balanced Score Card" kwenye Taasisi zote za Umma na za Binafsi. Somo la Balanced Score Card ni pana linahitaji muda kulieleza.

  kwa herini

   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  St. nyerere alishindwa wewe utaweza..jaribu basi
   
 12. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swadaka Allahu l'azimu
   
Loading...