Watanzania wengi hujiunga na CCM wakifikisha umri wa miaka 40 na kuendelea

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,923
8,314
Ukiondoa chipukizi na UVCCM ambalo huandaliwa toka wakiwa wadogo kuja kuwa viongozi.

Kuna kundi kubwa sana la Watanzania wakifikisha miaka 40 huamua kuwa Wanachama wa CCM kabla ya hapa hili kundi huwa halijishughulishi sana na siasa zaidi ya ushabiki wa mdogo mdogo tu.

Makatibu wengi wa CCM kwenye mashina wanakiri kuwa watu wengi wenye familia huwa wanaenda kujiandikisha kujiunga na CCM Kwasababu wanakuwa wameshakuwa na majukumu na wanaona CCM kuna uongozi bora.

Ndio maana vijana wengi wenye kupitia umri wa miaka 25 hadi 35 mpaka 39 ndio wanakuwa na mihemko ya kisiasa wakipita hapo basi hujiunga na CCM

Ni kupitia utafiti huu utakuta vijana wengi wanasema wazee ndio wanaibeba CCM ila sio kweli kuna kundi kubwa sana la watu wazima wanaojiunga na CCM hali inayopelekea CCM kuweza kuongoza kwa miaka mingine mia moja ijayo hapo ni nje ya lile kundi la chipkizi na UVCCM.

Asante CCM, bila wewe hatuwezi kuwa na amani. Vyama vya upinzani havifai kwani vinachezea amani yetu
 
Watanzania wengi wanafiki

Wanaikataa CCM kwenye vijiwe vya kahawa ila ni Ccm lia lia
Bia yetu,

Hao watu wanaofikia miaka 40 na kujiunga na CCM, fuatilia vizuri utakuta ni wale waliopoteza ramani za maisha. Niko na watu kibao wenye ramani za maisha walioko 40+, ukiwahusisha huo uchafu uitwao ccm wanakuambia kawaambie mafala wa vijijini.
 
Naunga mkono hoja

Bia yao ananichekeshaga sana yaani uzi anaanzisha yeye, maswali anauliza yeye, majibu anatoa yeye, changamoto anaziibua mwenyewe, mapendekezo anatoa yeye, ushauri na msisitizo vyote mwenyewe... nk, lakini si hivyo tu bali hata comments nyingi pia unakuta ni za kwake
 
Mkuu sio kweli Fuatilia vizuri utapata uhalisia wa jambo

Takwimu zinaonyesha hivyo, mimi nafikiri mtu akishakuwa na familia anatengeneza mazingira salama kwa familia yake ili iishi kwa amani
Kwasababu Ccm ndio kuna uhakika wa utulivu watu huchagua kujiunga na Ccm ili apambane na maisha mengine

Unaongea ujinga gani boss? Kuna watu kibao wana zaidi ya miaka 40 na hawana muda na hilo genge la wahuni. Wale waliopoteza ramani ndio kimbilio lao, maana wanaweza kushiriki kwenye siasa za mbeleko. Lakini mtu anayeweza kupambana kabisa hawezi kuungana na hilo genge hatari.
 
Na hawana mbwembwe mitandaoni Uchaguzi ukifika anaenda kupiga kura anarudi anatulia
Kujua idadi ya Chadema sio kazi,kwanza wapo mijini tu,pili wengi wao wapo kwenye mitandao tweeter,insta,fb.hata ukiamua kuwahesabu unapata idadi yao within 1 week.
 
Na hawana mbwembwe mitandaoni Uchaguzi ukifika anaenda kupiga kura anarudi anatulia

Nikikumbuka ule uchaguzi wa marudio hapo kwa Mtolea mabox ya kura kutolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm, tena kwa uratibu wa polisi na tume ya uchaguzi, nikiona hiki unachoandika hapa natamani kutapika.
 
Duuh,umesugua kichwa umewazaa na kuwaza mpaka ukapata uzi na ndio huu😁😁!

Wale wazee wa ambao walikuwa vijana enzi za Nyerere wanakaribia kuisha,hapo lile kundi la wajinga mnalolifanya mataji wa kura kwenu linateketea kwa kasi!Vijana wanatake over,na hapo ndio itakuwa ngumu sana kwa CCM!
 
Sio kweli watu wazima kibao kwenye huo umri, wengi sana hujiunga na Ccm na wengi wana circle nzuri tu ya uchumi

Nafikiria huwa wanapima Sehemu salama, sio salama kuwa zaidi upinzani Kwasababu vyama vingi havina sera ila mihemuko na matusi

Hao wenye uchumi mzuri ni wale wenye hofu ya kuhujumiwa shughuli zao za kujiingizia kipato, na wala hawajuingi kwa ridhaa yao. Haya mambo yanafanyika mbele ya macho yetu.
 
Mi Niko above 40, sijawahi kufikiria huo ujinga Wa kujiunga na CCM.

majority wanajiunga na CCM kwa kuwa ni kichaka cha watu waovu,mafisadi na kadhalika ili kuficha mambo yao.

Na pia hata wao wanjinasibu kuwa ukitaka mambo yao yaende vizuri jiunge ccm,kwa hyo wengi wankimbilia huko so kwa mapenzi waliyo nayo kwa chama.
 
Bia yetu,

Hao watu wanaofikia miaka 40 na kujiunga na CCM, fuatilia vizuri utakuta ni wale waliopoteza ramani za maisha. Niko na watu kibao wenye ramani za maisha walioko 40+, ukiwahusisha huo uchafu uitwao ccm wanakuambia kawaambie mafala wa vijijini.
Unataka kusema watu wa vijijini ni mafala.

Hao nyie humuwahitaji.
 
Bia yetu,

Hao watu wanaofikia miaka 40 na kujiunga na CCM, fuatilia vizuri utakuta ni wale waliopoteza ramani za maisha. Niko na watu kibao wenye ramani za maisha walioko 40+, ukiwahusisha huo uchafu uitwao ccm wanakuambia kawaambie mafala wa vijijini.
Kumbuka kuwa Ccm imekuwa tamu baada ya JPM kufanya kazi iliyotukuka. Kwa hiyo usijifarague kupinga kila kitu.
 
Nikikumbuka ule uchaguzi wa marudio hapo kwa Mtolea mabox ya kura kutolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm, tena kwa uratibu wa polisi na tume ya uchaguzi, nikiona hiki unachoandika hapa natamani kutapika.
Wakati mabox yanabebwa mawakala wa Chadema walikuwa wapi? Acha uwongo wewe.
 
Back
Top Bottom