Watanzania wengi hawawezi kuimba wimbo wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wengi hawawezi kuimba wimbo wa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by consigliori, Mar 28, 2011.

 1. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jumamosi nilikuwa mmoja wa watanzania wachache waliokwenda kuishangilia timu yetu ya taifa. Kama kawaida ya mechi za kimataifa, nyimbo za taifa hupigwa. Kilichonihuzunisha ni jinsi watanzania tulivyoonekana kutoujua vizuri wimbo wetu wa taifa, kwani kabla wimbo haujaisha, watu walishangilia kwa kupiga makofi na kukaa chini!

  Jamani watanzania, hata wimbo wa taifa hatuujui kweli? Ni aibu kwani wenzetu wa CAR walishindwa kutuelewa kabisa.
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inatia aibu sana....!
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  kwani wimbo wenyewe unaimbwaje? Naomba mashairi yake
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  hawa ndio Watanzania zaidi ya uwajuavyo.
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi niliwahi kuuliza swali humu lakini sikujibiwa, na nadhani sitajibiwa hata nikirudia. Swali langu ni hili: Ni wakati/matukio gani ambapo wimbo wa taifa unaimbwa ubeti mmoja na wakati gani zinaimbwa beti zote mbili? Naombeni majibu.
   
 6. enhe

  enhe JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 933
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 80
  wa nini bwana! tifa lenyewe la kuliimbia liko wapi?? lete mada muhimu sio upuuzi..
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Uzalendo uliisha nchi hii, na ni hawahawa viongozi njaa wanaumalizia!
  Mbona zamani watu wote tuliujua, lakini pia kulikuwa na ule mwingine wa "Tanazania Tanzania, Nakupenda kwa Moyo wote...", ambapo kwa sasa unaimbwa kukiwa na msiba wa kigogo!
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hauna tn haja ya kuujfunza. Kwny lile kongamano la waislam Ar juz walnshangaza walposema et wmbo wa Taifa ni wa kikris2, mpk leo bdo nashangaa!
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  hakuna wakati wimbo wa taifa unaimbwa nusu, package ni wimno kam aulivyo beti mbili zote hakuna kuchakachua.
   
 10. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uweze kuuimba alafu ukusaidie nini?
   
 11. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni kweli hata mm niko nje ya nchi kuna siku tulikuwa tuna hafla ya kupewa medali na ni lazima 2imbe wimbo wa taifa cha ajabu mwanzisha wimbo na baadhi ye2 hawaujui wakaanza kuimba tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wangu....! then ndo walipomaliza nikaanzisha Mungu ibariki,cjui ni kukata tamaa ya maisha au la!!
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Wimbo wa taifa unaojulikana ni Mungu ibariki DOWANS!
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu wimbo utaimbika katika hali kama hii njaa tupu hadi midomo imekuwa mizito.
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hivi Uzalendo unaanzia wapi?

  Kama hatuwezi kuimba wimbo wa taifa letu au hata kuujua tu, tutafika? Jumamosi nilishuhudia tukio ambalo lilinisikitisha na kunitisha sana, kabla ya mechi ya mpira wa miguu kuanza kati ya timu ya taifa na ile ya Jamhuri ya Africa ya kati, nyimbo za taifa zilipigwa live na brassBand.

  Watanzania tulisimama kwa heshima zote, lakini cha ajabu watu walikua hawaimbi ule wimbo na ulipofika nusu, baada ya Mungu ibariki Afrika, Uwanja ulilipuka kwa kushangilia kuashilia wimbo umekwisha, baadae watu waka stuka kuona wimbo unaendelea sehemu ya pili, yaani Mungu ibariki Tanzania…. Kabla haujakwisha watu wakashangilia tena. Kwa kweli watu hawajui wimbo wa taifa. Nadhani Serikali inatakiwa kufanyakitu Viongozi wetu waache malumbano yasiyo na tija.

  Infact nikamkumbuka Kaijage na CD zake
   
 15. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nimefanya uchunguzi kidogo nikaona, Watanzania wengi wanachanganya wimbo wa 'Tanzania Tanzania' na ule wa 'Mungu ibariki'
   
 16. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kaijage alilitambua hilo ndo maana akona hawa jamaa dawa yao ni staili ya bongo fleva CD mfuko wa nyuma ikifika zamu yake ni playback wakati mwenyewe anatafuna maneno. BIG UP Kaijage we miss yuuuuuuu
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  SHule zimekufa wakuu...
  Kwani hili ni jipya!!!
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Uzalendo wa nini wakati watu wanaibiwa. Viongozi wamesahau wajibu wao na hayo niyo matokeo. Sidhani kama wimbo wa Taifa unachanganywa na ule wa Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wot....... Kwanza vijana wengi wa siku hizi hata hawaufahamu. It's tru uzalendo wananchi umewaishia.
   
 19. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Uko sahihin mkuu, as time goes on, Tutaweza kuimba taarabu tu..
   
 20. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Na hawa ndio watanzania Viongozi nchi inaelekea kubaya! Wenzetu wanabuni hata National day ya kuwaunganisha wananchi wao sisi hata wimbo wa taifa tunashindwa!
   
Loading...