Watanzania wengi hawafahamu tofauti ya wajibu wa Mahakama na DPP

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,206
Tumeshuhudia watu wengi wasio na ufahamu wakisema eti kesi ya Mbowe tuiachie Mahakama iamue na kusiwekwe shinikizo la serikali kuiondoa kwa vile ni ya kubumba.

Tumeona pia Bunge la EU lililaumiwa eti liache kumshinikiza Rais Samia kuondoa kesi hii kwa vile tayari iko mahakamani. Tukumbuke Mahakama sio iliyo mpa kesi hii Mbowe, kesi hii ni ya serikali chini ya DPP hivyo kama ni ya kweli au kubumba mwenye kuielewa ni DPP ila hatimae Mahakama ndiyo itachuja.

Watanzania (ukiacha wenye ushabiki) wameona mwenendo wa kubumba wa kesi na uongo wake, mabalozi wameona na wame ripoti mwenendo mzima kwa mabosi wao ambao ndio wahisani wetu na hata vijana wetu wa ulinzi na usalama wamegundua mkakati wa kummaliza Mbowe. Lakini jee nchi itakuwa salama kwa mkakati huu?

Kesi hii bado iko kwa Rais kupitia DPP wake kama ilivyokuwa zile kesi za kina Rugelalila na wengine, sasa mnataka Mbowe akae jela miaka mingapi kisha mje mseme hana hatia?

NOLLE itumike nchi itulie
 
Mahakama za majaji wanaoipendelea CCM na serikali yake.
 
Kesi hii bado iko kwa Rais kupitia DPP wake kama ilivyokuwa zile kesi za kina Rugelalila na wengine, sasa mnataka Mbowe akae jela miaka mingapi kisha mje mseme hana hatia?
NOLLE itumike nchi itulie
Najaribu kuwaza kwa sauti. 🤔
 
Back
Top Bottom