Watanzania wekeni uzalendo mbele tarehe 11/03/2011 mkampokee Prof Lipumba

Mkuu mimi nitaenda kumpokea. Nadhani kwa sasa hana itikadi ya kichama. Kama watu hujitokeza kwenda kuwapokea washiriki wa Big Btother (akina Bhoke) kwa nini tusimpokee huyu ambaye ameonyesha kwamba TZ kuna vichwa?

mimi ningeenda kumpokea, ila aliwahi kuilaani Israel ilipokuwa inapigana na wahuni wa HAMAS. Hakutaka kulaani maroketi ya hamas ila alilaani Israel ilipokuwa inajihami. Huyu hafai hata kuongoza chama cha mpira wa vikapu.
 
Kama Prof alilaani mashambulizi ya Israel alikuwa sahihi sioni kosa hapo.kwakuwa Palestina haina jeshi wacha hamas isaidie. Ukumbuke kwamba Hamas ilishinda uchaguzi pale kwahiyo usiwaite wahuni.
 
Unaonyesha jinsi ulivyo na akili finyu. Ndalichako amewakataza ninyi kusoma? Unataka kutuaminisha kuwa serikali ya Tanzania inafundisha watu wake kuchukia baadhi ya dini? Kama unataka nchi inayoendeshwa kiislam hamia Libya, Saudia nk

Unabisha nini?siku tu Ndalichako atapofuta matokeo ya shule za Makanisa. hapo ndio mwisho wa mapnzi wa Ndalichako. maana wahahariri wote wakienda j2 kanisani. wataambiwa moja tu. Ndalichako aondoke, adui wa taifa. kila gazeti utaona linakuja na makala yake kuhusu mama.
Hukumbuki alipokingwa na wabunge wakiristo bungeni baada Mbunge mmoja kulituhumu baraza hili?
 
mimi ningeenda kumpokea, ila aliwahi kuilaani israel ilipokuwa inapigana na wahuni wa hamas. Hakutaka kulaani maroketi ya hamas ila alilaani israel ilipokuwa inajihami. Huyu hafai hata kuongoza chama cha mpira wa vikapu.
kama hamas ni wahuni basi hata chadema ni wahuni. Maana hamas ni ya waislam wa palestina, chadema ni ya wakiristo watz
 
Aaah! Hivi mara hii mmeshawasahau wa Tanzania? Walikuja ma miss walienda kuwapokea, wakaja wakaa uchi toka (BBA), wakaenda kuwapokea ndivyo walivyoumbwa jamani.
Lipumba kajipatia mkataba wake kwenye hiyo NGO wanaibuka tena kujipanga Airport.
Mtu asifanye kitu nje ya nchi, utakuta watu tayari wameshafika airpot.
Mwishowe mtaenda kupokea wale wanaorudi baada ya kuzaa na wazungu, waarabu wahindi na wachina.
 
Wewe nawe akili yako mbaya.Nampokea Lipumba kama nani.Jamaa kapata kula yake na watoto wake mimi nikajianike juani,sina utaahira huo.
watanzania mnahimizwa na kuombwa kwenda kumpokea profesa ibrahimu lipumba alieiwakilisha vyema tanzania.katika maswala ya uchumi wakidunia akiongoza zaidi ya maprofesa 100 nitunu ya watanzania
 
mimi ningeenda kumpokea, ila aliwahi kuilaani Israel ilipokuwa inapigana na wahuni wa HAMAS. Hakutaka kulaani maroketi ya hamas ila alilaani Israel ilipokuwa inajihami. Huyu hafai hata kuongoza chama cha mpira wa vikapu.
Mkuu nadhani unaunganisha haya mambo na imani. Mimi huwa sifungwi na mambo ya kiimani huwa napenda kuwa huru zaidi. Haya mambo ya Middle East yamejikita zaidi katika imani hivyo huwa sipendi kuyaongelea japo nayajua vizuri. Mbona Israel imekuwa ikilaaniwa na mataifa mengi tu? Nyerere alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kuwakaribisha PLO kufungua ubalozi hapa Tanzania. Kwa mataifa mengine, PLO wakishirikiana na PFLP (akina George Habash, Mohamed Hamshal, Ahmed Jibril, Waddie Hadadi na Carlos Ilitch Ramirez Sanchez - the Jackal), ilikuwa ni kikundi cha kigaidi lakini Nyerere kwa kutambua haki za Wapelestina akaitambua PLO. Mkuu haya mambo ni ya kihistoria na kiimani zaidi.
 
watanzania mnahimizwa na kuombwa kwenda kumpokea profesa ibrahimu lipumba alieiwakilisha vyema tanzania.katika maswala ya uchumi wakidunia akiongoza zaidi ya maprofesa 100 nitunu ya watanzania

Kama tuna mwana uchumi mzuri kama huyu alafu uchumi wetu unaporomoka kwa kasi hivi? jk inamaana humwoni?
 
Mkuu mimi nitaenda kumpokea. Nadhani kwa sasa hana itikadi ya kichama. Kama watu hujitokeza kwenda kuwapokea washiriki wa Big Btother (akina Bhoke) kwa nini tusimpokee huyu ambaye ameonyesha kwamba TZ kuna vichwa?

Even mkuu wa kaya ni kichwa?
 
Kama tuna mwana uchumi mzuri kama huyu alafu uchumi wetu unaporomoka kwa kasi hivi? jk inamaana humwoni?

Mkuu kwa Great Thinker hili ndilo lingekuwa suala la kujiuliza na siyo itikadi na imani. Huwa tunasema ati tunaongelea mustakabali wa Taifa kumbe siyo; tunaongelea itikadi na vyama vyetu!
 
mi napita tu hapa mwishowe mtasema na linah naye akiimba vizuri tumpokee anaporudi,kanumba the great akitoa movie nzuri ikasifiwa nje naye mtataka tukampokee kwa shangwe,baba mwanaasha akipewa tena u dr. feki twende tukampokee,tokeeenii hapo mi hamnipeleki huko yaaani mtu anakusifiwa umevaa nguo mpya wakati hujaaoga wiki nzima mwili unanuka ushafu
 
mi napita tu hapa mwishowe mtasema na linah naye akiimba vizuri tumpokee anaporudi,kanumba the great akitoa movie nzuri ikasifiwa nje naye mtataka tukampokee kwa shangwe,baba mwanaasha akipewa tena u dr. feki twende tukampokee,tokeeenii hapo mi hamnipeleki huko yaaani mtu anakusifiwa umevaa nguo mpya wakati hujaaoga wiki nzima mwili unanuka ushafu

Mkuu hujawahi kuona watu wamejikusanya na maua yao wakiwapokea celebrities wetu? Kama hiyo huitaki angalia Watanzania tunavyopenda kuwapokea watu kwa shngwe.

wanasukuma-gari-la-jairo.jpg
 
HAPO JEE VIPI BIBLIA HAIJAWAKASIRISHA WAKRISTO? Waislamu Hawali Nguruwe, Damu, Au Wanyama Wafu. Biblia Pia Inakataza Hilo “Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika
lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi.
Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga ya”(Biblia Walawi 11:7-8) Baadaye katika aya ya 21 ya sura hiyo tunasoma yafuatayo: “usile kitu kilichokufa
chenyewe. “... Na wale wenye kula nguruwe na uchafu mwingine, ndiyo, pia panya, watapotea wote, asema Bwana”. (Isaya 66:17 Biblia) “Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa najisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu; wajiepushe na uasherati; wasile mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe
damu.”(Biblia
Matendo 15:20) “Ni lazima tu subiri si kwa kula damu. Kwa sababu damu ni roho na roho usile na nyama. Unapaswa kumwaga kwenye ardhi kama maji “. (Kumbukumbu
12:23-24 Biblia) “Na kama mtu wa nyumba ya Israeli, au mmoja wa wageni ambao wanaishi kati yao, akinywa damu yoyote, nami nitaweka uso wangu dhidi yake ambae anakunywa damu na kumkatilia kwake mbali na watu wake” (Mambo ya Walawi 17:10 Biblia) “Na hakuna damu yoyote
mtayokunywa, ama kwa ndege au mifugo, bila kujali wapi mlipo. Kila mtu anaekunywa damu yoyote, huyo atakatiliwa mbali na watu wake “. (Walawi 7:26-27 Biblia) Ni Haramu Kwa Waislamu Kunywa Pombe. Biblia Inatueleza Wazi Yafutayo “Uasherati na pombe lazima uondoshe akilini” (Hosea 4:11 Biblia) Je, wamesahau kwamba watu wabaya
hawataurithi
Utawala wa Mungu? Msidanganyike!
Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu
sanamu, wazinzi, au walawiti. wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji,
wanyang'anyi, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu. (Biblia Kwanza Wakorintho 6:9-10) Katika Uislamu ni haramu Riba. Biblia pia inakataza Riba “Unaweza kukopa fedha kwa ajili ya maskini yeyote kati yenu, kati ya watu wangu, hivyo ni lazima si kitendo dhidi yake kama walaji riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote” (Biblia, Kutoka 22:25) “Usichukue faida yoyote ya ndugu yako, ama ya pesa au chakula au kitu kingine chochote ikawa umechukua riba” (Biblia, Kumbukumbu la Torati 23:19) “Na kama mnawakopesha
wale tu mnaotumaini
watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha
wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!”. Biblia (Luka 06:34) “... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe,
lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake “. (Biblia Ezekieli 18:13) Waislamu huchinja na kutoa Swadaqah ya kondoo mwanamke
akijifungua. Hii pia imetajwa katika Biblia. “Na siku yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja
kondoo mwenye umri kwa sadaka ya kuteketezwa ... (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia) Waislamu
Hutahiriwa. Yesu Na
Ibraahiym Na Manabii Wote Wa Israeli Walikuwa Wakitahiriwa? “Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa
mimba '(Biblia, Luka 2:21) “Na Mungu akamwambia
Abrahamu:”Utunze
agano langu, wewe na uzao wako baada yako, na vizazi vyote. Na hili ndilo agano kati ya mimi na wewe na uzao wako baada yenu, ambaye mtazishika kila uume kati yenu kutahiriwa katika govi zenu, na hii itakuwa ni ishara ya agano kati ya mimi na wewe. Vizazi, kila mtoto wa kiume kati yenu atatahiriwa, wakati ni umri wa siku nane, kama walivyofanya
mtumishi wa kuzaliwa katika nyumba yako na yeye ambaye kanunuliwa kwa fedha za kigeni kutoka kwa watu ambao si wa ukoo wako. Utahiriwa ni kwa mtumishi wenu na aliozaliwa katika nyumba yako na yule uliemnunua kwa fedha. Na ndiyo ahadi yangu katika mwili wako wazi kuwa agano la milele. Lakini mmoja wa watoto wa mataifa mengine mtu mmoja ambaye govi haijawahi kutahiriwa, naye atatengwa na watu wake. Yeye kavunjwa ahadi yangu. (Biblia, Mwanzo 9-14)
“Na Ibrahimu alichukua mtoto wake Ismail na watumishi wake wote, mzaliwa wa nyumba yake na watu waliokuwa wamenunuliwa kwa fedha, kila uume kati ya watu wa Ibrahimu, na kutahiriwa siku hiyo govi yao ambayo Mungu alimwambia. Na Abrahimu alikuwa na miaka tisini na tisa. Wakati govi yake ilitahiriwa na mtoto wake Ismail alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu wakati govi yake ilitahiriwa. Tarehe ya siku hiyo Ibrahimu katahiriwa,
na mtoto wake Ismail. Na ya watu wote katika nyumba yake, mzaliwa wa watumishi wake wa nyumbani na wale ambao walikuwa wamenunuliwa kwa fedha kutoka mataifa ya nje, walikuwa
wametahiriwa
pamoja naye “. (Mwanzo 17:23-27 Biblia) “Na Ibrahimu katahiriwa mtoto wake Isaka alipokuwa na umri wa siku nane, kama Mungu
alivyomwamuru”.
(Biblia, Mwanzo 21:04) Kuhusu kutahiri ipo katika biblia: “Agano la Kale liliteuliwa na Mungu kama ishara ya pekee kwa watu wa Israeli, na kama ukumbusho wa ahadi zao pamoja naye. (Kutoka 17:09 a, 3 Mwanzo 0:03, Yohana 7:22) Pamoja
na kwamba mistari yote ya Wayahudi inashuhudia hivyo ikawa ni “moto” na utata suala ambalo lilisaidia kugawa watu baada ya kipindi cha Yesu. Kuoa Wake Wengi Katika Uislamu. Hata Katika Biblia Kumetajwa Kuoa Wake Wengi “Akichukua mke mwingine, basi asifanya upungufu wowote katika mlo wa zamani, mavazi au sheria za ndoa”. (Biblia,
Kutoka 21:10) “Kama mtu ana wake wawili, mmoja
anayempenda na mwingine ambaye hamuoni ...” (Biblia, Kumbukumbu la Torati 21:15) “Yeye alikuwa na wake
wawili ...” (Biblia, Samuel 01:02) “Kwa hiyo, Daudi alifika huko pamoja na wake zake wawili ...” (Biblia ya Samuel 02:02) “Lakini wakati wa usiku aliamka na kuchukua wake wake wawili na watu wake wawili wahuduma na wanawe kumi na mmoja….” (Biblia, Mwanzo 32:22 Uislamu Unaamuru Wanaume Kufuga Ndevu: Tuangalie Biblia
Inatwambiaje
Kuhusu Suala Hili “Msikate pande yote ya nywele zenu ya vichwa, wala msikate pande ya ndevu zenu. (Biblia, Walawi 19:27) Katika Biblia imetajwa katika maeneo mengi, kwamba manabii na waumini walikuwa na ndevu. Tazama kwa mfano Ezra 9:03, Mambo ya Walawi 21:05, Nehemia 13:26


Safi sana kiongozi kilichobaki UBATIZWE tu na uchague kati ya maji mengi au machache, sababu wajua bibilia kuliko hata Qorani, mbaya zaidi unawazidi mpaka wakristu wenye bibilia yao.

Unasitahili nishani iliyotukuka.
 
Back
Top Bottom