Watanzania wazidi kukumbwa na ‘jinamizi’ la ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wazidi kukumbwa na ‘jinamizi’ la ajira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 20, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TATIZO la ajira nchini limeendelea kuongezeka na kusababisha maelfu ya Watanzania kugombea nafasi za kazi chache zinazotangazwa sasa hivi kwenye mashirika mbalimbali.

  Miongoni mwa eneo ambalo limeonekana kugombewa ni nafasi za kazi 17 zilizotangazwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), lakini waombaji ni 1,540.

  Katika nafasi hizo, 10 ni za Ofisa Mwendeshaji ambapo waombaji ni 1,484 na nafasi saba za wahasibu ambapo walioomba ni 56.

  Akizungumza na gazeti hili leo, Mkuu wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema ni kawaida kila kunapotangazwa nafasi za kazi waombaji wanakuwa wengi na kuongeza “mfano Septemba mwaka jana, tulitaka nafasi chache, lakini waombaji walifika 4,000 na hii si kwetu tu kwenye mashirika mengi hali ndiyo ilivyo sasa.”

  Chiume alisema shirika hilo limeamua kutangaza majina ya wote walioomba ili waende kufanyiwa usaili Alhamisi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo watafanyiwa mtihani wa kuandika unaotungwa na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

  “Sisi (NSSF) hatuujui mtihani wao, UDSM watawachuja kulingana na ufaulu wao na wanaweza kuwafanyia mtihani zaidi ya mara moja na mwisho kwa kila nafasi watatuletea majina kama manne ya waliofanya vizuri na ndipo tutawafanyia usaili wa ndani na hatimaye kupata idadi tunayoitaka,” alisema ofisa huyo.

  Akielezea sababu za kutochuja majina kabla ya kuwaita kwa ajili ya usaili, Chiume alisema “watu wengi wamekuwa wakilalamika wakiomba kazi NSSF hawapati, hivyo tumeona tutoe matangazo ya majina yote ya walioomba ili wajue wanaoomba ni wengi kuliko nafasi tunazokuwa nazo”.

  Akizungumzia juu ya tatizo la ajira na watu wengi kujitokeza kuomba kazi pindi kunapotangazwa nafasi, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alikiri tatizo la ajira nchini ni kubwa na kwenye mashirika na kampuni nyingi zinazotangaza kazi, waombaji wanakuwa wengi.

  Waziri huyo alisema “Serikali tunajitahidi kisera kuvutia wawekezaji ili kupunguza tatizo la ajira lakini wenzetu waandishi, Bunge na sisi hatuzungumzi lugha moja, mnapinga uwekezaji na kila mwekezaji mnamuona shetani sasa hivi Rwanda wametupita kwa uwekezaji”.

  “Ninachowaomba wote tuwe lugha moja tuheshimu sheria za kazi na kazi zenyewe zifuatwe na tukaribishe uwekezaji ili kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira nchini”
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hizo tarakimu haziwakilishi watu wenye tatizo la ajira bali lina mengi ndani yake........... kwa undani wake lina sehemu ndogo sana ya watu wanaotafuta ajira nikiwa na maana ya watu wasio na ajira wanaotafuta ajira............. wengi wao wanaajira tayari na baada ya kujiona wana uzoefu kiasi fulani wanataka kubadili mwajiri wakitafuta majani mabichi zaidi................ na kwa kweli watu kama hao ndio hatimaye wataajiriwa kwa sababu wakipambana na wasio na uzoefu wana nafasi kubwa ya kuwashinda na ajira za mtindo huu zinakuwa za kuajiri wenye ajira na kuwaacha wasio na ajira............. hiyo ndo tanzania na dunia ya sasa.......... wenye kazi wanabadili kazi wapendavyo na wasio na kazi wanalia na kusaga meno............ nafikiri tukio la mtu kupata ajira kwa mara ya kwanza linatakiwa kusherehekewa kwa shukrani kubwa sna a kwa Mungu kwani ndio ukombozi halisi..................
   
Loading...