Watanzania "wazagaa" nje ya nchi yao!!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,241
Watanzania wengi wapo Ulaya Magharibi, Marekani ya Kaskazini na Japan. Sababu za wao kwenda huko ni nyingi. Lakini wengi wao wameenda au walienda huko kwa malengo ya elimu, wengine kwa maswala ya kibiashara, wengine kwa lengo la kuhamia na wengine kwa ajili ya kutembea. Mbinu na nyenzo walizotumia kufika huko zinatofautiana...

-------------------- [url="https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=654"]waraka huu unaishia hapa!![/url] --------------------
 
Hivyo basi watanzania tusishangae kuona wachina wanazagaa katika mitaa ya Tanzania.
 
Hivyo basi watanzania tusishangae kuona wachina wanazagaa katika mitaa ya Tanzania.

....exactly! kama wapo hapa nchini kwa kufata sheria zote na yote wanayotenda hapa nchini yako ndani ya sheria... tuwaache wakae kwa amani.
Kama tu vile ambavyo Watanzania wanabughudhiwa na sheria za huko walikohamia zinavyozidi kutungwa kuwabana makazini na wasizidi kuongezeka; basi nasi tuzibe loopholes zilizopo kama presence yao hapa hivi sasa siyo- conducive. Na tusianze kuwabugudhi individuals..
 
kwa vitendo maana hivi hivi tu umaskini kamwe hautalaanika!

vitendo gani sasa, maana watu walima, wamefanya biashara lakini umaskini bado upo. Vitendo vipi vifanyike ili kuumaliza huu umaskini? unaumiza akili, mwili na roho.
 
vitendo gani sasa, maana watu walima, wamefanya biashara lakini umaskini bado upo. Vitendo vipi vifanyike ili kuumaliza huu umaskini? unaumiza akili, mwili na roho.

Mama!
Asilimia kubwa ya watanzania hawalimi,hawafanyi biashara,hawana elimu!in general hatufanyi kazi yaani ni wavivu!Hivyo basi kuuondoa umaskini lazima kuwe na self commitiment kuanzia kwenye kaya hadi kwenye taifa!
Thanks to God tuna kila kitu ila ndo hivyo hatujui kuvitumia najua masikio ya waafrica wengi yako kusikia G8 wameongeza dau gani la msaada!
katika Taifa pia ni lazima viongozi wawe waaminifu kwa taifa lao na si kushiriki katika Rushwa na kuiuza nchi yao!Unajua umaskini unapimwa pia kwa kuwepo na wawekezaji wengi kutoka mataifa ya nje hii inamaanisha serikali imeshindwa kujiendesha na ndo khali tuliyonayo kwa sasa!
In short kazi ipo ila tunahitaji kujitoa ki ukweli kuanzia katika kaya hadi taifa kuumaliza umaskini!kwa kutumika katika uzalishaji naamini tumake POVERTY A HISTORY!
 
hivi kulima kwa jembe la mkono kunaweza kumtoa mtu kwenye umaskini? nahisi kuna kitu zaidi ya kuwa wavivu. Mkoa wa Iringa ulikuwa unaongoza kwa kilimo cha mazao ya chakula miaka fulani, Hivi hali yao ya maisha iliboreka?

Je wale wanaolima matunda na kukosa soko nao nani alaumiwe?

Je hudhani kuwa wakulima hawajawezeshwa vya kutosha ili kuweza kuwa wakulima wazalishaji na sio wakulima wakulima chakula chao ambacho wengine hakikidhi hata mahitaji ya kaya zao kwa mwaka?

Mkoa kama Singida, Dodoma, Shinyanga na Tabora, unadhani wakulima hata walime usiku na mchana wanaweza kujikwamua hali zao za maisha?

Nadhni kuna kitu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.
 
kwa mfano walimaji wa matunda wangewekewa kiwanda cha kutengeneza juice!kwa mfano korogwe kama sikosei kunakiwanda ambacho kilikuwa kiwe cha kutengeneza juice sijui iliishia wapi!
Ni kwamba mama suala la uvivu lipo pale pale pamoja na suala la kutokuwa na strategies na Rushwa pamoja na ubadhilifu ukichanganya vyote hivi inakuwa ni mwiko kuulaani umaskini!
kwa mfano Shinyanga na Mwanza kulikuwa na vyama vya ushirika sasa huvi vipo kwenye magogo yaani vianasuasua ile mbaya hapa namaanisha SHIRECU na NYANZA!ukiangalia source ni ubadhilifu hivi vyama viliwasaidia wakulima wa pamba enzi zile kwa kununua mazao yao!
ki ukweli kuna cycle hapo hivyo basi kila mtu lazima ajikomit kuondoa umaskini!
Any way tusije tukahama kwenye maudhui ya thread!Maana thread inaongelea kuzagaa kwa wtz nje!
 
usijali kwani bado hatuko nje ya mda, tunazojadili hapa ni sababu zinazowafanya watanzania wazagae nje ya nchi.

My take, hakuna nchi inayokosa wavivu duniani, hii ndio moja ya diversity Mungu alizotupatia. Kwa hiyo uvivu hapa Tanzania hatuwezi kuuepuka!

Kwa kusema wakulima wote ni wavivu hapo nakataa kata kata. Wakulima wanalima ekari tano kwa mkono, na wakati wa mavuno anaishia kupata laki tatu kwa wenye bahati! Wakati huo huo, hakuna hospitali nzuri kijijini hapo ili hata atakapougu basi apate matibabu! hakuna maji safi hapo kijijini na analizimika mwanakijiji huyu asafiri umbali wa hadi kilomita 5 na zaidi kuyafata. Akirudi nyumbani bado hajatafuta kuni, na msitu aliozoea kutafutia kuni, uko conserved na wanamazingira hivyo haruhusiwi kukata kuni. Hapo bado anadaiwa kodi ya kuku, ng'ombe, mbuzi, baiskeli, na hajanunua nguo za shule za watoto, madaftari na michango mingine ya kijamii. Hivi atakuwa na nguvu hata ya kufikiri kweli?

Ndio maana baadhi ya watanzania wanaona bora wakawe mbwa ulaya na marekani kuliko kuwa mtu na kubaki hapo Tanzania.
 
Ndio maana baadhi ya watanzania wanaona bora wakawe mbwa ulaya na marekani kuliko kuwa mtu na kubaki hapo Tanzania.

Huko ulaya na marekani wtz wanakokimbilia hawakulala na kesho yake wakaamka
wameupunguza umaskini!na kukimbia matatizo huo ni ubanafsi kwa mfano wanaoenda huko kwa masomo then wanalowea badala ya kuja kufanya mapinduzi kwenye nchi zao ili kuondoa matatizo!hata hao huko tunakokimbilia walikuwa maskini walianzia kwenye ziro point ila wakajicomit kufanya walichokifanya hadi leo wtz wanakimbilia huko kwenda kufaidika na maendeleo kwenye hizo nchi huku nchi zao zikiwa kwenye magogo!
umaskini utafutwa na maskini wenyewe na sio G8!
 
watanzania wanaozagaa nje na wachina wanaozagaa hapa tz roles zao ni tofauti!wachina wapo hapa na wanafanya biashara ya vitu kutoka kwao hapo wanafaidisha nchi yao!sisi huko nje tunafaidishaje nchi yetu?vitu wanavyouza wachina hata sisi tungeweza kutengeneza na tukauza ila ndo hivyo tena uvivu wa kubuni mambo ambayo yatatuwezesha kutatua matatizo yetu ya umaskini na kadhalika
 
Mama!
Asilimia kubwa ya watanzania hawalimi,hawafanyi biashara,hawana elimu!in general hatufanyi kazi yaani ni wavivu!Hivyo basi kuuondoa umaskini lazima kuwe na self commitiment kuanzia kwenye kaya hadi kwenye taifa!

First Lady, Kula 5

Maneno yako Kuntum! yaani hamna ulichokosea ndio maana MAFISADI wanajua kabisa Tutasema sana na mwisho tutalala kwa upeo wetu mdogo wa kutofikiri na kukosa self committiment. Wana JF sisi ni wachache sana kati ya walioweza kupata upeo wa kuelimika kimawazo ila na mbaya wengi ni wale waishio nje ya nchi, Je sasa asilimia nyingine ya nchi wanatambua na kuwa na mawazo kama ya humu ndani JF ikiwa Wana JF wanachukua kama 0.14% ya Watanzania wote?
 
Huko ulaya na marekani wtz wanakokimbilia hawakulala na kesho yake wakaamka
wameupunguza umaskini!na kukimbia matatizo huo ni ubanafsi kwa mfano wanaoenda huko kwa masomo then wanalowea badala ya kuja kufanya mapinduzi kwenye nchi zao ili kuondoa matatizo!hata hao huko tunakokimbilia walikuwa maskini walianzia kwenye ziro point ila wakajicomit kufanya walichokifanya hadi leo wtz wanakimbilia huko kwenda kufaidika na maendeleo kwenye hizo nchi huku nchi zao zikiwa kwenye magogo!
umaskini utafutwa na maskini wenyewe na sio G8!

Hivyo suala linakuja ni kwa nini hapa tanzania ni vigumu sana kutoka kwenye ziro point? Kwa nini vijana wetu kama wanaweza kufanya kazi kwa bidii wakiwa nje hapa nyumbani washindwe? Naamini kuna kitu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii. Na kitu hicho hasa mimi kwa upande wangu nadhani ni miundombinu duni. Tanzania hakuna umeme reliable, upatikanaji wa sio maji reliable,b barabara ndio usiseme, utasafirishaje hayo mazao kutoka ruvuma vijijini kuja kwenye soko lenye bei za kueleweka ruvuma mjini aun hata morogoro na dar es salaam? usafiri wa reli ndio usafiri wa nchi kavu unaoweza kubeba mzigo mkubwa kwa gharama nafuu, je tuna railway network ambayo ni reliable?

Bado G8 itakuwa ina mchango mkubwa kisera, kwani tupende tusipende bado uchumi wetu unakuwa control na siasa za kimagahribi. Mfano, parachichi utalokula Tanzania sio sawa na utakalokuwa ulaya. La Tanzania lina ubora wa hali ya juu na liko tasty hadi mzungu mwenyewe anabana ngenge akilila. Parachichi hilo kulisafirisha kwenda kuliuza huko maulaya ambako bei ni nzuri ni kitu kisichowezekana kabisa. Utawekewa vikwazo ooh, lina doa jeusi, oo mara vile, mara kiwango na kadhalika. Je kwa nini kama globalisation inafungua milango ya free markets, kwa nini basi na sisi tusiexport free kwenda nchi yeyote duniani bila vikwazo?
 
Mama!
Asilimia kubwa ya watanzania hawalimi,hawafanyi biashara,hawana elimu!in general hatufanyi kazi yaani ni wavivu!Hivyo basi kuuondoa umaskini lazima kuwe na self commitiment kuanzia kwenye kaya hadi kwenye taifa!
Thanks to God tuna kila kitu ila ndo hivyo hatujui kuvitumia najua masikio ya waafrica wengi yako kusikia G8 wameongeza dau gani la msaada!
katika Taifa pia ni lazima viongozi wawe waaminifu kwa taifa lao na si kushiriki katika Rushwa na kuiuza nchi yao!Unajua umaskini unapimwa pia kwa kuwepo na wawekezaji wengi kutoka mataifa ya nje hii inamaanisha serikali imeshindwa kujiendesha na ndo khali tuliyonayo kwa sasa!
In short kazi ipo ila tunahitaji kujitoa ki ukweli kuanzia katika kaya hadi taifa kuumaliza umaskini!kwa kutumika katika uzalishaji naamini tumake POVERTY A HISTORY!

Wakuu,

"Ili kujipatia maendeleo, tunahitaji vitu vinne, 1. Watu 2. Ardhi 3. Siasa safi na 4. Viongozi bora." JKN.

Tanzania kama nchi si masikini hata kidogo, nchi hii ina utajiri wa hali ya juu kabisa kuliko nchi nyingi nyingine duniani.

Kama ni hivyo kwa nini sisi watanzania wenyewe tu masikini wa kutupwa. Ndio, sisi ni masikini sana pampja hata na wale wenye vijisenti. Nao pia ni masikini wa kutupwa. Tuna umasikini wa mali, wa ujinga na wa uwoga.

Iweje baada ya miaka 50 ya uhuru tuwe tumo katika hali hii. Maradhi hayatubanduki, umasikini umetuzonga, ujinga umetutapakaa, rushwa imetuzagaa na ufisadi umetuvaa na sisi tumekaa tunakodoa macho tu.

Msingi wa umasikini wetu ni "inaction." Hakuna kitu kibaya kama kutokufanya kitu. Watu tunao na ardhi tunayo, lakini je, siasa yetu ni safi? Viongozi wetu je? Ni bora?

Madini yetu tu, yangetosha kutupunguzia umasikini kama siyo kutuondolea kabisa. Tungechimba na kuyasafisha, kuyakata, kuyatengeneza na kuyauza wenyewe. Na kama tunashindwa, tungeweka masharti ambayo yangetunufaisha kwa wawekezaji.

Kwa mfano, tungemwambia mwekezaji sisi ndio wenye mali yetu hapa ni 51% na wewe ni 49%. Unapokuwa hapa 5% ya wafanya kazi wataalamu ni wako na wafanya kazi 95% ni wetu na baada ya miaka 10 hao wataalamu 5% wawe watu wetu uliowafundisha. Unataka chukua, hutaki tusalimie. Huyo ndio masikni jeuri. Miaka 50 hii tungekuwa tumeshafikia mahali panapoonekana.

Kama hujala, utakosa wapi kuwa mvivu? Njaa inatuzagaza nje ya nchi. Iwe njaa ya mali au elimu.
 
vitendo gani sasa, maana watu walima, wamefanya biashara lakini umaskini bado upo. Vitendo vipi vifanyike ili kuumaliza huu umaskini? unaumiza akili, mwili na roho.

Kwa kuondoa viongozi wabovu katika uongozi na hili litawezekana kwa kubadilika sisi wenyewe - pale ambapo tutajiamini na kuondoa woga wa kusema sasa basi kwa njia yeyote au gharama yeyote ile.
 
Kwa kuondoa viongozi wabovu katika uongozi na hili litawezekana kwa kubadilika sisi wenyewe - pale ambapo tutajiamini na kuondoa woga wa kusema sasa basi kwa njia yeyote au gharama yeyote ile.

huo woga utaondokaje wakati mtu ana njaa na mate yanamdondoka akisikia harufu ya chakula? kuwaondoka viongozi wabovu inakuwa ngumu kwa sababu hao viongozi wanachukulia udhaifu wa njaa za wananchi na hivyo kurudi madarakani miaka nenda rudi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom