Watanzania wawili wadakwa Kenya kwa tuhuma za ugaidi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
Watanzania wawili wamekamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi katika eneo la isiolo nchini Kenya, wakienda Somalia ambako wanahisiwa wakienda kujiunga na Al- Shabaab

Mkuu wa polisi kituo cha Isiolo Charles Ontita amesema Watanzania hao walikamatwa na maaskari katika bara bara ya Isiolo – Moyale karibu na njia panda inayoelekea Garba, na baada ya kuwapekua ndipo walibaini walikuwa Watanzania na hawakuwa na vibali vya kusafiria.

“Maaskari waliokuwa doria walisimamisha basi na kuanza kukagua, ndipo walipowakuta wageni wawili ambao hawakuwa na vibali, waliwaambia askari kuwa walikuwa wanaenda Moyale kufanya kazi ambayo wameitiwa, na baada ya kupekua simu zao walikuta baadhi ya namba za Somalia ambazo walikuwa wakiwasiliana nazo, na kusema ndio watu waliowaitia kazi”, amesema Kamanda Ontita.

Watanzania hao wametajwa kuwa ni Juma Abbas Zuberi mwenye miaka 28 na Ali Juma Kaondo wa miaka 17, wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Isiolo, huku wakiendelea kuchunguzwa na Akskari hao wa kupambana na ugaidi kutoka Nairobi

Chanzo:
KTN Kenya
 
Washaanza kulipiza kwa njia nyingine
Hapana hiyo ni sawa kabisa wacha wavune walichopanda! Wakikiri kwamba walikuwa wanaenda kuungana na Al-shabaab, wanyongwe mpaka kufa ili liwe fundisho kwa wengine wenye mawazo kama hayo!!
 
Watanzania wengi tu wako na alshababy na kuna wengine hata walisha uwawa na alshababy kwa sababu ya kutaka kutoroka.
 
247e1bd8f51491d4e2d08a568194bd08.jpg
 
Yote hayo wakenya wanaasira na magu na watamkomesha tu.

Swissme
 
Tunahitaji amani na utulivu wa dunia.

Kama ni kweli basi, wapewe ile kitu watu wanaogopa sana.
 
mimi nimeona hapo DENI LA TAIFA LAPANDA. sasa sijui lapanda ndege kwenda Canada kucheki uwezekano wa kukomboa ndege yetu?

kujiunga na vikundi kama hivyo ni imani na imani hata ukimfunga mtu au kumzuia ataendelea kuwa na imani yake hiyo hiyo.
 
Yote hayo wakenya wanaasira na magu na watamkomesha tu.

Swissme

swissme ,

Hata Tanzania tunao uwezo wa kuwakomesha wakenya tena sana na huyo Uhuru Kenyatta, usidhanie kuwa Kenya ni baba wa Tanzania.

Na kama hujui Tanzania ni baba wa figisu tukiamua Kenya anapumulia mtungi wa oxygen gasi ndani ya wiki moja tu.

Don't ever underestimate the power of a silent country like Tanzania.
 
Mkuu una vichekesho. Unamaanisha sisi tunaoongizwa na kina bashite?
 
Naamini wakenya wakitulia watalianzisha. Figisu......kubwa sana awamu hii naona haziendaniii kabisa !!! Urafiki uzalendo utaifa ujirani......undugu kipi zaidi??
 
Watanzania wawili wamekamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi katika eneo la isiolo nchini Kenya, wakienda Somalia ambako wanahisiwa wakienda kujiunga na Al- Shabaab

Mkuu wa polisi kituo cha Isiolo Charles Ontita amesema Watanzania hao walikamatwa na maaskari katika bara bara ya Isiolo – Moyale karibu na njia panda inayoelekea Garba, na baada ya kuwapekua ndipo walibaini walikuwa Watanzania na hawakuwa na vibali vya kusafiria.

“Maaskari waliokuwa doria walisimamisha basi na kuanza kukagua, ndipo walipowakuta wageni wawili ambao hawakuwa na vibali, waliwaambia askari kuwa walikuwa wanaenda Moyale kufanya kazi ambayo wameitiwa, na baada ya kupekua simu zao walikuta baadhi ya namba za Somalia ambazo walikuwa wakiwasiliana nazo, na kusema ndio watu waliowaitia kazi”, amesema Kamanda Ontita.

Watanzania hao wametajwa kuwa ni Juma Abbas Zuberi mwenye miaka 28 na Ali Juma Kaondo wa miaka 17, wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Isiolo, huku wakiendelea kuchunguzwa na Akskari hao wa kupambana na ugaidi kutoka Nairobi

Chanzo:
KTN Kenya

Endapo wangefanikiwa kwenda Somalia bila kukamatwa na baadae kurudi Tanzania hao ndio wangekuwa Magaidi ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti, Rufiji), UAMSHO na nk.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom