Watanzania watakiwa kusoma vitabu ili kujielimisha

Apr 9, 2022
66
32
Watanzania wametakiwa kutumia maktaba ili kuweza kujielimisha na kujitafakarisha Masuala Mbalimbali yahusuyo jamii.
Phoenix20221028_044940.png


Wito huo umetolewa na Waziri ofisi ya Rais uratibu na Bunge Jenista Muhagama jijini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu Cha my life my purpose Cha Rais wa awamu yatatu Hayati Benjamin Mkapa ambapo amesema Pindi msomaji anaposoma vitabu Anapata kujielimisha zaidi kupitia vitabu.

"Maktaba ni chombo Muhimu katika kujenga taifa letu,Kama viongozi nilazima tutumie maktaba ilikuweza kufikikia Maendeleo Endelevu". Alisema Jenista Muhagama.
Waziri Jenista Muhagama Alisema kuwa kwa kutumia njia ya usomaji wa vitabu viongozi waweze kupata Miongozo itakayowasaidia kuliongoza taifa.

Alisema kwa kusoma vitabu viongozi wataweza kuwa wabunifu nakuongeza uwezo wakujiamini.

"Tuongeze Kasi ya kusoma vitabu ili tuweze kujielimisha kwakusoma vitabu kunaleta files bora". Aliongeza Jenista Muhagama.

Waziri Muhagama aliwataka waandishi wa vitabu nchini kutumia lugha ya kiswahili katika machapisho ilikuweza kukuza lugha hiyo.

Naye Katibu Mkuu ikulu Dk Moses kusiluka aliwataka viongozi kuweza kuandika vitabu nakujenga Utamaduni wa kusoma vitabu.
 
Vijana gani hao,au hiki kizaz cha bongofleva cha kuwafatilia wasanii

Ova
 
Watu wanasoma vitabu ila shida Sasa wame elimishwa na kuaminishwa walichokisoma Hadi kusahau kukidadisi...... •Tunaona Hadi vitabu vyenye Maarifa batili vikinadiwa wazi wazi.
•kuharibika kwa baadhi ya watu ni kutokana na Maandiko wanayokutana nayo.
#Attention_Economy
 
Uzi sahihi kabisa kwa mahitaji ya vitabu ndani na nje ya jiji la dar es salam ntakupatia hard copy ya kitabu chochote cha mwandishi wako pendwa kwa gharama ya elfu kumi na tano tu( afu 15 tu )
20220923_203142.jpg
 

Attachments

  • 20220923_203116.jpg
    20220923_203116.jpg
    965.3 KB · Views: 12
  • 20220912_210011.jpg
    20220912_210011.jpg
    1.2 MB · Views: 12
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom