Watanzania watakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,315
2,000
Waumini mbalimbali na wakristo nchini wameaswa kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kupiga vita ubinafsi ili kujenga nchi yenye upendo, amani na maendeleo.

Mwito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Moravian, Jimbo la Mashariki na Pwani Tanzania, Emmaus Bandekile Mwamakula jana katika salamu zake kwa wakristo za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

“Tunaposherehekea sikukuu ya Krismasi hatuna budi kukumbuka maana halisi ya Krismasi. Biblia inafundisha kuwa Yesu Kristo aliamua kuacha utukufu wote aliokuwa nao mbinguni pale alipozaliwa sehemu ya kulishia ng’ombe ili awatumikie na kuwakomboa wanadamu,” alisema Askofu Mwamakula, Aidha, alisema tukio la kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Yesu Kristo inawakumbusha waumini na wakristo kuacha ubinafsi na kwani hakuna jamii yoyote iliyofanikiwa popote duniani kama inaendeleza ubinafsi.

Askofu Mwamakula alisema vita dhidi ya ubinafsi inayopigwa kwa nguvu zote na Rais Magufuli, inapaswa kuungwa mkono kwani ubinafsi ni adui wa haki, upendo, umoja, amani na maendeleo.

“Ubinafsi unafanya hospitali zinakosa dawa na huduma muhimu na kusababisha watu ambao wangekuwa wazalishaji mali kupoteza maisha kwasababu tu watu wachache wametumia pesa zilizotakiwa kutumika kuwatibia,” alisema askofu huyo.

Alisema Rais Magufuli ametambua madhara ya ubinafsi ndio maana ameanzisha vita alivyovipa jina la “Kutumbua Majipu” hivyo anapaswa kuungwa mkono na kupongezwa.

Aliwasihi Watanzania wote kuungana kwa kuwa vita hivyo havina dini, kabila, itikadi, jinsia, umri wala rangi na kuongeza kuwa kama jamii inahitaji demokrasia ya kweli, ni lazima kupiga vita ubinafsi.
 

G 4real

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
449
250
Anapiga vita nini???? Ubinafsi?

Kama ni maono,sawa tusubiri..kama anaongelea uhalisia basi huyu msemaji ni jipu.
 
May 3, 2014
66
95
Acheni chuki za ovyo nyie, TUMUOMBEE Rais wetu mpendwa azidi kuitendea haki nchi yetu kwa kuleta viwanda, kufufua shirika la ndege, kuondoa wafanyakazi hewa, kuboresha huduma za jamii kama afya, maji, umeme, mindombinu, elimu nakadhalika, hata kama mlidhani watu wenu wapiga deal wange lindwa, huu ni utawala wenye intergrity, kwahiyo wapiga deal hamwezi kusifia, sie tulio zoea kula kwa jasho letu, tuta muombea na naamini MUNGU atatusimamia na kiongozi wetu JPM. God bless u JPM and yr family
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
What..!!!! Maybe over his dead body...maana marehemu siku zote ni wema hata kama waliuwawa kipindi wanaiba au wameshikwa ugoni...
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,063
2,000
Sina muda wa kupoteza kumuombea mtu asie na huruma kwa raia wake....

Kila siku akiwa jukwaani anasema kuwa ye ni rafiki wa wanyonge....uongo mtupu

Watu wanaendelea kuzama kwenye dimbwi la umaskini afu anatuletea ngonjera za hovyo hovyo tu...

akajiombee mwenyewe huko....
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,094
2,000
Abebe msalaba wake mwenyewe! alijua ikulu ni makalvati na madaraja .
wacha roho mbaya. ingekua oktoba 2015 mumepata malisho baada ya unyumbu kilometa mamia uambiwe kumuombea edo badala ya magoti ungesujudu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom