Watanzania wasahaulifi sana-waliorejesha fedha za epa wanatakiwa kuwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wasahaulifi sana-waliorejesha fedha za epa wanatakiwa kuwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Nov 24, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Moja ya sifa kuu tuliyo nayo watanzania ni WEPESI KUSHAU NA KUSAMEHE. CCM na viongozi wake wanaoujua udahifu wetu huo. Mwaka Desemab 2005 wa hotuba yake ya kuzindua bunge Raisi Jakya Kiwete alisema "Katika Serikali yake mar tu Wakaguzi wa hesbu (auditor) watakapogundua wizi suala hilo litafikishwa Polisi kwa hatua zaidi badlla ya kungoja vikao kukaa kupitisha maamuzi"

  Mwaka 2006 ripoti ya wakaguzi wa ndani na nje ikaonyesha kuwa katika Benki Kuu zimeibiwa kiasi kikubwa cha fedha na kuwataja wahusika wakiwemo wamiliki wa Kampuni ya KaAGODA na kupendekeza kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiha masuala ya kugushi ambayo ni makosa ya jinai
  , wahusika wafikishwe Polisi mara moja.

  Alichokifanya Raisi Jakya Kikwete ni kuunda Tume tofauti na kauli yake wakati wa uzinduzi wa Bunge la 9 Desema 2005 na baadaye kuwapatia wezi hao fursa ya kurejesha fedha walizoiba Serikalini. Mpaka leo baadhi ya wezi hao ni wajube wa Kamati Kuu ya CCM.

  Tarehe 18 Novemba 2010 wakati Rais Jakya Kikwete anazindua Bunge la 10 alirudia kauli yake ya kuwataka Wizi utakaogunduliwa na wakaguazi wa mahesabu wahusika kufikishwa Polisi badala ya kungoja vikao.

  kwa kuwa Sheria iko wazi kabisa katika makosa ya Jinai, kuwa kurejesha ulichoiba sio kinga ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria wala kupatiwa adhabu stahiki kwa amujibu wa sheria.

  Na kwa kuwa wapo watu mbali mbali ambao waliwahi kurejesha walivyoiba lakini sheria ikachukua mkondo wake. Mfano hai m iaka ya nyuma kidogo Mhasibu mmoja wa Wizara moja aliyewahi kujipatia mishahara miwili isivyo halali; alipogundulika ndugu zake wakaomba kurejesha kiasi alichoiba ndugu yao (Mhasibu), wakarhusiwa na wakarejesha na kukatiwa stakabadhi ya serikali ya kuirejeshea serikali kilichokuwa kimeibiwa.

  Lakini kwa kuwa kurejesha kilichoibiwa sio kinga ya mtuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria, Serikali ilitumia stakabdhi za urejeshaiji wa fedha hizo kama ushahidi kuthibitisha kosa mahakamani; na mtuhumiwa akapatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela. Na kwa bahati mbaya alipoteza maisha wakati akitumikia kifungo hicho.

  Nini mtazamo wako kuhusu kauli za Rais Jakaya Kikwete kuhusu wanaoiba fedha Serikali wakigundulika kufikishwa Polisi alizotoa wakati akizindua Bunge Desema 2005 na baadaye wezi walipogundulika akawataka kurejesha fedha walizoiba; na Serikali yake ikashindwa kuwachukulia hatua zaidi za kisheria baada ya ushahidi kupatikana kirahisi kama ambavyo Serikali zilizomtanguia zilivyofanya kulingana mdfano uliotajwa hapo juu?

  Au ndio yale yale ya Watanzania wepesi kusahau na kusamehe?
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Akili zetu inabidi zikapimwe kweli tena! Kuna kaugonjwa kwenye vichwa vyetu na tusipokadhibiti tunaelekea kubaya zaidi!
  Huwezi amini lowasa atagombea uraisi na kupita kwa ccm na watu wakashangilia, sitasubili litokee hili ntakuwa nimehama hii nchi!
   
 3. b

  bojuka Senior Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowasa akichaguliwa rais naingia msituni.
   
Loading...