Watanzania waridhishwa na Utendaji kazi wa Serikali ya Rais Samia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,220
9,648
Ndugu zangu watanzania,

Watanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa, Dini zao, makabila Yao, Kanda zao, jinsia zao,Rika zao, Elimu zao Na vipato vyaao Wameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia.

Watanzania Wameonyesha kuridhishwa na hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali yao,wanafurahishwa na kuguswa mioyo Yao na kumpa pongezi Rais Samia na serikali yake ya ccm kwa hatua zake na uamuzi wake wa kuendesha na kuongoza maridhiano ya kisiasa hapa nchini ambayo yamepelekea kuimarika kwa umoja wa kitaifa na mshikamano wa watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa.

Hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya Rais Samia katika kukuza na kujenga uchumi jumuishi umewafurahisha Sana watanzania kwa kuwa wanapenda uchumi unaokua katika mifuko yao na siyo katika makaratasi tu, miradi mbalimbali ya kimkakati iliyo chochea ongezeko la ajira kwa vijana imeleta Tabasamu kwa watanzania wengi, utulivu amani na usalama ulio Tamalaki hapa inchini umewapa furaha watanzania na kuwafanya kuishi kwa amani bila hofu Wala wasiwasi na kuendesha shughuli zao kwa utulivu mkubwa.

Wafanyabiashara nao Wameonyesha kuridhishwa na hatua za serikali katika kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kibiashara yaliyopelekea kushamiri na kuchipua kwa biashara mbalimbali hapa nchini zilizopelekea kuongezeka kwa makusanyo ya mapato mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo kukimbizana Wala kufungiana biashara mitaani bila kujali hasara anayoipata mtu ambaye alikuwa hajapewa hata Elimu juu ya jambo fulani,kwa Sasa TRA inatoa Elimu kwa wafanyabiashara na kuwatembelea Mara kwa Mara katika maeneo yao na kuwapa semina ambayo imejenga mazingira na Hali ya kuaminiana na kuondoa ule uhasama na kuviziana au kukomoana.

Vijana wameridhishwa na hatua mbalimbali za serikali ya Rais Samia katika suala la ajira na kutengeneza fursa za ajira ikiwepo kuipa nafasi secta binafsi ili iweze kukua na kutoa ajira kwa vijana, vijana wanaridhishwa na utendaji kazi wa Serikali Yao kwa kutambua kuwa ajira imekuwa ni tatizo linaloisumbua Dunia kwa kuwa vijana wanadhidi kuhitimu katika vyuo mbalimbali kila mwaka kwa Kasi kubwa Sana ukilinganisha na kasi ya ukuaji wa secta zinazotoa ajira, Ndio maana wanaridhishwa na Hatua za serikali yao kwa namna ilivyotengeneza maelfu ya ajira.

Kwa hakika uongozi wa serikali ya Rais Samia Umebarikiwa na kupewa kibali na Mwenyezi MUNGU, watanzania wamempa baraka zote Rais Samia na serikali yake, watanzania wapo bega kwa bega na serikali yao,kwa Sasa Hakuna adui yeyote kutoka nje ya nchi anayeweza kutushinda maana umoja tulionao kwa Sasa Ni imara na madhubuti Sana,Hakuna upenyo wa kupenyeza adui kwa kutumia mtanzania maana kwa Sasa mbegu ya Uzalendo iliyopandwa katika mioyo ya watanzania imewafanya watanzania kutanguliza mbele Taifa letu.

Hakika uongozi Ni hekima busara na maarifa, vitu ambavyo Rais Samia amejaliwa kuwa navyo katika ulimi wake na akili yake.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Kaka sisi wote ni watanzania na tunaishi hapa hapa tz, huenda unalipambania tumbo lako na familia yako.

Ila ukweli maisha yamepanda Sana Hari ya uchumi,mahitaji dukani na zahanati sio rafiki toka Samia akubari kuwa chini ya wafanya biashara.

Inamaana mkuu ujui kuwa watanzania hatukubaliani. Na hii Hari mbaya ya maisha?
 
Kaka sisi wote ni watanzania na tunaishi hapa hapa tz,huenda unalipambania tumbo lako na familia yako.
Ila ukweli maisha yamepanda Sana Hari ya uchumi,mahitaji dukani na zahanati sio rafiki toka Samia akubari kuwa chini ya wafanya biashara.
Inamaana mkuu ujui kuwa watanzania hatukubaliani. Na hii Hari mbaya ya maisha?
Rais Samia amefanya juhudi na kazi kubwa Sana katika kuujenga uchumi wetu ,Amefanya jitihada kubwa Sana zilizochochea mzunguko mzuri wa fedha mitaani ikiwepo ujenzi wa miradi mbalimbali,ulipaji wa mdeni kwa watumishi wa umma,upandishaji wa mishahara kwa watumishi wa umma,kutoa Mikopo kwa vijana kupitia halmashauri Hali iliyochochea hali nzuri ya biashara mitaani,

Suala la mfumuko wa Bei pia amefanya kazi kubwa Sana Rais Samia na serikali Yake ikiwepo kutoa mabillioni ya pesa Kama Ruzuku mfano katika Nishati ya mafuta serikali ilikuwa inatoa shilingi billioni Mia moja kila mwezi,wakati katika mbolea serikali ilitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini Hali iliyo pelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu.

Hatua hizo na zingine nyingi zilipunguza ugumu na makali ya maisha kwa watanzania kwa serikali kuamua kujitwisha mzigo na kumtua mtanzania
 
Kaka ngoja nikwambie tu ukweli,huwezi kupata teuzi na Wala huwezi kupigiwa simu na kitengo yeyote yule Mana unajitia uchawa wakijinga mno.
 
Back
Top Bottom