Watanzania wapo tayari-CCM yazidi kukataliwa.

Amani iwe nanyi:

Tabia ya kusema huyu ni mwenzetu kwa hiyo asisemwe hadharani inazidi kuota mizizi ndani ya chadema. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba mtu akiwa mwanachadema hata akitenda maovu chama kitamlinda kwa nguvu zote na kumtetea.

Hii tabia ilikomaa kipindi kile mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda akitaja wauza madawa ya kulevya. Walitajwa wa vyama vyote lakini alipotajwa Mbowe chama badala ya kumwajibisha kikaanza kumlinda na kumtetea!!!

Ikaja kwenye mashamba pori , wengi wamenyang'anywa na kurejeshwa serikakini lakini waliponyang'anywa viongozi wa chadema(Sumaye) chama badala ya kumwajibisha sasa kinamtetea eti ameonewa!!

Jana tena Freeman Mbowe ameitisha maandamano yasiyo na kibali tena yanayoanza saa 12 jioni kuelekea ofisi ya mkurugenzi , matokeo yake vurugu zikatokea barabarani na kupelekea mabasi kupigwa mawe na hatimaye mwanafunzi asiye na hatia kupoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Ukweli ni kwamba bila Mbowe kuitisha maandamano haya mauaji yasingetokea, lakini pamoja na ukweli wote huu kuwa wazi bado wafuasi wa chadema wanamkingia kifua na kumtetea Mbowe badala ya kumtaka awajibike kutokana na uovu alioufanya!!

Mara nyingi pia tumekuwa tukiona mtu anaitwa mwizi na fisadi akiwa chama kingine lakini fisadi huyo akihamia chadema ghafla anasafishwa na kuanza kulindwa kwa nguvu zote na wanachadema!!

Kama sasa hivi hamjashika dola mnalindana namna hii mkishika uongozi wa nchi itakuwaje??

Si watu wataiba hadharani na kukimbilia kuchukua kadi ya chadema ili watetewe?

Tabia hii haikubaliki na ni mwendawazimu tu wa kushabikia tabia ya kusitiriana maovu namna hii.
 
I see wabongo wamebadirika pamoja na Magu kuonyesha kwamba anawajali wanyonge bado upinzani upo!
 
tupo wengi sana kwa mtaa sisiem tutawaonyesha pamoja na kuwa na uchwara hapo magogono.


Risasi za nini ww si unakubalika?
 
LOL PUMBA KATIKA UBORA WAKE
Pole sana nadhani na wewe ni mojawapo, lakini ujue tu chaguzi hizi za Siha na kinondoni zimetuma ujumbe mzito kuwa pamoja na propaganda zote za JPM na serikali yake lakini watanzania wamewakataa
 
Ukiona hivyo ujue wewe ni "kiti moto" maana ndio wanaotumia hizo pumba.

Mabavu na uonevu yenyewe yameshaanza kuchoka, Watanzania wanavyozidi kukaza anguko la huyu mtu halifiki 2025
 
Back
Top Bottom