Watanzania wapewa siku 3 kuondoka kwenye kijiji cha Msumbiji walipouliwa wenzao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Watanzani wapewa siku tatu kuhamisha mali zao mpakani mwa Msumbiji
Watanzani wapewa siku tatu kuhamisha mali zao mpakani mwa Msumbiji

Serikali ya Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kutoa siku tatu kwa wakazi wa kijiji cha Kitaya wilaya ya Mtwara kuhamisha mali zao zilizopo katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji baada ya kutokea kwa mauaji ya Watanzania 10.

Wiki iliyopita watanzania 10 waliuliwa katika kijiji hicho kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Wananchi hao wameanza kuhamisha mali zao chini ya ulinzi wa serikali zote mbili kutoka katika kijiji hicho nchini Msumbiji.
IMG-20190704-WA0011.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amesema kuwa wananchi hao wameanza kuhamisha mali zao kuanzia jana katika kijiji cha Mtole kilichopo pembezoni mwa Mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Mmanda amesema wananchi hao wanatakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku tatu kuanzia jana.

“Kuanzia jana tumewajulisha watu wenye mali zao upande wa pili wakazichukue tumewawekea ulinzi wapo waliovuka mto Ruvuma na wengine wametumia usafiri wa mitumbi kufuata mali zao” alisema Mmanda.
Wananchi hao wameshukuru serikali hizo mbili kwa kuwapa ulinzi wa kuvuka na kufuata mali zao bila kupata madhara yoyote.
IMG-20190704-WA0012.jpg

Aidha, walidai changamoto waliyokutana nayo ni baadhi ya mizigo yao kukosekana na pia hakuna amani nchini huko.
IMG-20190704-WA0013-300x111.jpg

Pia wamesema usiku wa kuamkia jana kuna milio ya mabomu kwa upande wa Msumbiji ambayo imewaongezea hofu na kuiomba serikali iwaongezee ulinzi.
 
Jeshi letu la policcm huu ndio muda muafaka wa kujipambanua kama kweli nyie mpo kamili.
Ile kazi yenu ya kuzuia mikutano ya wapinzani Kwa kisingizio cha intelijensia sasa nendeni huko msumbiji mkawazuie hawa magaidi
 
Msumbiji na Tanzania wamekubaliana kwamba magaidi wako right, Watanzania hawatakiwi kuwepo Msumbiji, kwa hiyo waondoke in three days.

Na ukiondoa tatizo la Watanzania kuishi Msumbiji ugaidi Msumbiji utaisha.

Vichwa vya viongozi wa serikali za third world.
 
Siasa wawachie akina polepole waimarishe intelijensia ya kubaini magaidi,wasishangilie ushindi wa kibiti Tu hawa watu wapo undercover wakilipuka itakuwa shida
 
Msumbiji na Tanzania wamekubaliana kwamba magaidi wako right, Watanzania hawatakiwi kuwepo Msumbiji, kwa hiyo waondoke in three days.

Na ukiondoa tatizo la Watanzania kuishi Msumbiji ugaidi Msumbiji utaisha.

Vichwa vya viongozi wa serikali za third world.
Nafikiri wamegundua kuwa suala si ugaidi bali xenophobia!
 
Msumbiji na Tanzania wamekubaliana kwamba magaidi wako right, Watanzania hawatakiwi kuwepo Msumbiji, kwa hiyo waondoke in three days.

Na ukiondoa tatizo la Watanzania kuishi Msumbiji ugaidi Msumbiji utaisha.

Vichwa vya viongozi wa serikali za third world.
Be positive to your country no matter what. Like: Serikali mbili hizi zinataka kuanza kuwashughulikia hao magaidi, lakini kusudi wasihatarishe usalama wa watanzania - wamaonelea kwanza waTanzania warudi kwao ili wadeal na hao magaidi barabara.
 
Hivi kweli magaidi? Kwanini tusiseme kikundi cha usalama unataka kuwaondoa watanzania nchini msumbiji lakini wanatumia ugaidi ili kutimiza azma yao. Kuwa positive na mzalendo na nchi nakubaliana nayo lakini tusikubali kulishwa matango pori. Na kufanywa mazwazwa wa kutupwa Mungu katupa akili ili kufikiria na kujua la kweli na uongo.

Nangatukaa 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Msumbiji na Tanzania wamekubaliana kwamba magaidi wako right, Watanzania hawatakiwi kuwepo Msumbiji, kwa hiyo waondoke in three days.
Na ukiondoa tatizo la Watanzania kuishi Msumbiji ugaidi Msumbiji utaisha.
Vichwa vya viongozi wa serikali za third world.
Mkuu mali na maisha ya raia wake ndio kipaumbele cha kwanza cha serikali yeyote duniani.

Tunasikia na kuona kwenye TV mara nyingi Marekani au nchi za Ulaya wakiwapa msaada raia wa nchi zake waondoke ndani ya nchi au eneo lenye hatari (machafuko).
Tuliona Ufaransa na Marekani zikiondoa raia wake Jamhuri ya Afrika ya kati na kule Libya.

Pia tuliona wakati wa maandamano ya Misri au Tunisia.

Wakati mwingine waafrika tuache kujidharau.
 
Sawa, tatizo la Ugaidi lipo lakini hapo naona limetumika kama kisingizio tu, hawawataki watanzania hapo kijijini basi
 
Be positive to your country no matter what. Like: Serikali mbili hizi zinataka kuanza kuwashughulikia hao magaidi, lakini kusudi wasihatarishe usalama wa watanzania - wamaonelea kwanza waTanzania warudi kwao ili wadeal na hao magaidi barabara.
Mkuu unadhani hao magaidi Wana ALAMA au Uniform basi?? Wanakula nao, wanaswali nao, wanacheza nao na wanahama nao
 
Be positive to your country no matter what. Like: Serikali mbili hizi zinataka kuanza kuwashughulikia hao magaidi, lakini kusudi wasihatarishe usalama wa watanzania - wamaonelea kwanza waTanzania warudi kwao ili wadeal na hao magaidi barabara.
kwa akili yako 'kubwa' unaamini magaidi watabaki kusubiri ulichosema? Siasa hiyo. Pindi uchaguzi ukiisha na mambo yatatulia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom