Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Watanzani wapewa siku tatu kuhamisha mali zao mpakani mwa Msumbiji
Serikali ya Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kutoa siku tatu kwa wakazi wa kijiji cha Kitaya wilaya ya Mtwara kuhamisha mali zao zilizopo katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji baada ya kutokea kwa mauaji ya Watanzania 10.
Wiki iliyopita watanzania 10 waliuliwa katika kijiji hicho kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Wananchi hao wameanza kuhamisha mali zao chini ya ulinzi wa serikali zote mbili kutoka katika kijiji hicho nchini Msumbiji.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amesema kuwa wananchi hao wameanza kuhamisha mali zao kuanzia jana katika kijiji cha Mtole kilichopo pembezoni mwa Mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Mmanda amesema wananchi hao wanatakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku tatu kuanzia jana.
“Kuanzia jana tumewajulisha watu wenye mali zao upande wa pili wakazichukue tumewawekea ulinzi wapo waliovuka mto Ruvuma na wengine wametumia usafiri wa mitumbi kufuata mali zao” alisema Mmanda.
Wananchi hao wameshukuru serikali hizo mbili kwa kuwapa ulinzi wa kuvuka na kufuata mali zao bila kupata madhara yoyote.
Aidha, walidai changamoto waliyokutana nayo ni baadhi ya mizigo yao kukosekana na pia hakuna amani nchini huko.
Pia wamesema usiku wa kuamkia jana kuna milio ya mabomu kwa upande wa Msumbiji ambayo imewaongezea hofu na kuiomba serikali iwaongezee ulinzi.