Watanzania waonywa dhidi ya tabia ya uwindaji na ulaji wa panya

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,733
48,294
RUKWA:

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amezua balaa kutokana na wananchi mkoani kwake kufanya panya kuwa kitoweo hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuwaua wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu unaofanywa na watu wanaowatafuta wanyama hao.

Agizo hilo alilitoa hivi karibuni katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, Kata ya Mpwapwa, wilayani Sumbawanga baada ya kuwauliza wananchi wa kijiji hicho juu ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya na wananchi kukataa.

Alisema kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwa sababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza misitu mkoani humo

panya-2.jpg

RUKWA: KITOWEO CHA PANYA CHAZUA BALAA - Global Publishers

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.

Amesema kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza misitu.

“DC tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma huko kuwatafuta hawa panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,” Alisisitiza.

Agizo hilo amelitoa katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya, japo wananchi walikataa.

Pia katika kuongezea hilo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha anasimamia sheria ya hifadhi ya mazingira na kuwawajibisha wote wanaohusika na uharibifu wa mazingira.

Nae akisoma taarifa Mkurugenzi wa H/W ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto ni muitikio mdogo wa uhifadhi wa mazingira pamoja na mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya hali inayosababisha uchomaji wa misitu wakati wa kiangazi.

“Changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa serikali ya Kijiji kujihusisha na uuzajia wa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya hifadhi ya Kijiji na usimamizi mdogo wa sheria ndogo za vijiji katika utunzaji wa misitu,” Alimalizia.

Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na upandaji kiti wa kibiashara Julius Magaga alimweleza Mh. Wangabo kuwa chnagmoto inayowakatisha tamaa vijana wengi ni kutokana na uwindaji wa panya uliokithiri na kusababisha hasara katika misitu.

Kwa msimu wa 2017/2018 hadi 30/1/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga imepanda miti 830,527 ambayo ni sawa na 55.4% na ina misitu 92 yenye ukubwa wa jumla ya Hekta 49,179.6. Huku Mh. Wangabo akigawa miche 850 kwa kaya 850 za Kijiji cha Mpwapwa, Wilayani Sumbawanga.

Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa - Full Shangwe Blog
 
huko wanawawinda ili wawaue na si kwa ajili ya kitoweo bali kuwaangamiza. MAANA kule panya ni shida SANA.

kichwa cha habari na habari yenyewe ni Kusini na kaskazini.

maana suala siyo kuwawinda panya na kula, bali ni njia yao ya kuwinda kwa kuchoma misitu. hivyo rai iliyotolewa na kiongozi ni kubadirisha njia ya kuwinda ya kutumia sumu ili misitu isitoweke kwa kuchoma moto.
 
DC tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto

Kumbe swala ni kuua panya kwa sumu wafie huko huko porini ili kuokoa misitu dhidi ya moto,nilidhani kwa uwindaji kwa ajili ya kula,Wakenya bhana.
 
huko wanawawinda ili wawaue na si kwa ajili ya kitoweo bali kuwaangamiza. MAANA kule panya ni shida SANA.

kichwa cha habari na habari yenyewe ni Kusini na kaskazini.

maana suala siyo kuwawinda panya na kila, bali ni njia yao ya kuwinda kwa kuchoma misitu. hivyo rai iliyotolewa na kiongozi ni kubadirisha njia ya kuwinda ya kutumia sumu ili misitu isitoweke kwa kuchoma moto.

Hehehe!! Mnatumia nguvu nyingi kubwabwaja kama mlioshiba minofu ya panya, DC ameamua kuwaua ili msiwapate huko porini.
RUKWA: KITOWEO CHA PANYA CHAZUA BALAA - Global Publishers

panya-2.jpg
 
MK254
huku suala si kuwinda na kula panya. bali ni namna gani wanavyowinda. wanachoma misitu.
 
HALAFU wewe MK254 sijui bichwa lako likoje. nani kasema panya hawaliwi. suala alilokuwa ukiongea D.C. ni namna ya kuwinda.
na kwa taarifa yako. kuna jamii nyingi hapa Tanzania wanakula panya na mbwa since time immemorial. ni desturi yao. wanakula kama chakula kingine tu. haijalishi ukame au mvua. ni jadi yao. sema kwa sasa hizo desturi zinaanza kupungua.
 
Hehehe!! Asante kwa kuingia penyewe na kunasa, haya kwaheri...
 
HALAFU wewe MK254 sijui bichwa lako likoje. nani kasema panya hawaliwi. suala alilokuwa ukiongea D.C. ni namna ya kuwinda.
na kwa taarifa yako. kuna jamii nyingi hapa Tanzania wanakula panya na mbwa since time immemorial. ni desturi yao. wanakula kama chakula kingine tu. haijalishi ukame au mvua. ni jadi yao. sema kwa sasa hizo desturi zinaanza kupungua.
Hii ndo inaitagwa kubadilisha gia arthini Cc. Jina kubwa, Deogratius Kisandu.
 
Japo Rukwa sio walaji wa Panya, ila panya wanatumiwa na jamii nyingi sana hapa duniani, hapa Afrika nchi ya Malawi, Zambia na Msumbiji wanatumia sana nyama ya Panya, Tanzania wamakonde ambao ni jamii ya watu wa Msumbiji wanatumia Panya, mimi ni mlaji mzuri wa jamii ya Panya wale wakubwa, jamii ya mijikenda huko Kenya, wadigo, waduruma, wagiriama, wanakula sana ndezi, ambayo na jamii ya panya buku, sasa mleta mada ninahisi ameishiwa mada za maana anajaribu kutapatapa
 
HALAFU wewe MK254 sijui bichwa lako likoje. nani kasema panya hawaliwi. suala alilokuwa ukiongea D.C. ni namna ya kuwinda.
na kwa taarifa yako. kuna jamii nyingi hapa Tanzania wanakula panya na mbwa since time immemorial. ni desturi yao. wanakula kama chakula kingine tu. haijalishi ukame au mvua. ni jadi yao. sema kwa sasa hizo desturi zinaanza kupungua.
Ana matatizo huyu jamaa, endeleeni kumpuuza.
 
Japo Rukwa sio walaji wa Panya, ila panya wanatumiwa na jamii nyingi sana hapa duniani, hapa Afrika nchi ya Malawi, Zambia na Msumbiji wanatumia sana nyama ya Panya, Tanzania wamakonde ambao ni jamii ya watu wa Msumbiji wanatumia Panya, mimi ni mlaji mzuri wa jamii ya Panya wale wakubwa, jamii ya mijikenda huko Kenya, wadigo, waduruma, wagiriama, wanakula sana ndezi, ambayo na jamii ya panya buku, sasa mleta mada ninahisi ameishiwa mada za maana anajari
Yaani we jamaa kumbe huwa unakula nyama ya panya na mbwa? Achana nao bana. Zime'affect' sana uwezo wako wa kutumia ubongo wako ifaavyo. Nenda katubu bana! Yote yaliisha msalabani. :D:D:D
 
Yaani we jamaa kumbe huwa unakula nyama ya panya na mbwa? Achana nao bana. Zime'affect' sana uwezo wako wa kutumia ubongo wako ifaavyo. Nenda katubu bana! Yote yaliisha msalabani. :D:D:D
South Korea na China ndiyo wanakula mbwa zaidi duniani na nyoka na Panya, kule hawaachi mnyama yoyote hapa duniani, na Japan nao ni hivyo hivyo, lakini ndiyo vinara wa technolojia hapa duniani
 
South Korea na China ndiyo wanakula mbwa zaidi duniani na nyoka na Panya, kule hawaachi mnyama yoyote hapa duniani, na Japan nao ni hivyo hivyo, lakini ndiyo vinara wa technolojia hapa duniani
Sasa mmeiga ulaji wao wa mbwa afu mambo ya teknolojia mkayatupilia kulee! Si nilidhani watz huwa mnakuza vyakula vya kujitosheleza. Hivi niulize, ukimaliza shughuli yenyewe huwa unatumia vichokonoa meno kutoa manyoya ya panya kwenye meno? Acha hizo bana, ni lunch time! :)
 
Maskini, yaani walimgeukia 'Simba' laivu, tena kabla ya kumfanyia kweli najua walipiga bonge la muluzi, akajileta yeye mwenyewe. Dah, inahuzunisha sana.

Hehehe! Jamaa wanapenda sana huo msosi haswa kipindi kama hiki vyuma vimekaza, siku hizi kila Mtanzania anapambana na hali yake maana pamekua pagumu pale.
 
Back
Top Bottom