Watanzania wangechambua siasa na uchumi kama wanavyochambua mpira tungefika mbali

David Goliath

JF-Expert Member
May 16, 2018
926
1,790
Habari zenu wakuu,

Bila kupoteza mda niende kwenye hoja yangu, miaka ya hivi karibuni kumekua na utitiri wa radio nyingi za masafa ya FM, kama tunavyojua dhima kubwa ya vyombo vya habari ni kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha jamii.

Kwa upande wa Redio zetu za Tanzania vipindi vya michezo vimepewa kipaumbele kuliko jambo lolote wanajadili michezo kuanzia asubuhi, mchana, jioni, usiku tuseme Taifa nikama halina jambo lingine linalofaa kupewa kipaumbele kujadiliwa zaidi ya michezo.

Wananchi nao muda wote wapo bize kujadili mpira iwe kwenye vyombo vya usafiri, sehemu za biashara, makazini, majumbani Hadi mashuleni, wakati nchi ina matatizo chungu nzima wanafunzi vyuo vikuu wanakosa mikopo.

Hali ya elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuoni zinatia huruma, masoko ya wakulima hali ni mbaya, huduma za kijamii kama maji, afya, umeme ni tabu tupu kwenye upande wa mambo ya upatikanaji wa haki masuala ya sheria Bado ni Giza, lakini yote hayo tumeyapa kisogo tumejikita kujadili na kuchambua mpira kana kwamba Taifa halina mahitaji mengine, Kwa upande wangu naona kama hii siyo sawa, kwenu wadau.
 
Huko kwenye mpira hakuna ugali wa CCM, watu wako free kuongea.
Ni tofauti na kwenye Siasa penye ugali wa CCM
 
Ukisikika unachambua siasa kwa nia njema kabisa unakabidhiwa kwa Usalama/Polisi unakuwa muangaliwa wao. Kila unavhofanya umekamatwa, umehojiwa, umewekwa ndani kidogo ili usisikike tena.
 
Hata kwenye mpira hawajui kuchambua.Madai na falsafa za kijinga tu na sifa za kijinga kuhusu timu wanazoshabikia.
Kama hujaziona zikicheza unaweza ukapata picha ni world class teams.
Kumbe tia maji tia maji.
 
Mambo mengi ya msingi tumeyapuuza na hatuyapi kipaumbele ..
 
Kama hapa Dar es salaam wanajadili mpira mpaka kero kuna eneo pale karume yaani kuna wauza kahawa kabisa kama kilinge wanajidili mpira masaa yote
 
Moja ya sababu mpira umekuwa gumzo kubwa ni watu kutotaka kujihusisha na siasa...
Watu Wana "escape "kujadili siasa na uchumi ...na kutafuta nafuu ya kisaikolojia Kwa kujadili mpira au udaku....
 
Back
Top Bottom